Uchaguzi 2020 Kamati ya siasa CCM Mkoa wa Dar, acheni maamuzi ya kuangamiza chama jimbo la Ukonga, mnadhalilisha chama na Uongozi wa juu kwa rushwa!

Uchaguzi 2020 Kamati ya siasa CCM Mkoa wa Dar, acheni maamuzi ya kuangamiza chama jimbo la Ukonga, mnadhalilisha chama na Uongozi wa juu kwa rushwa!

Chipoku

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2011
Posts
254
Reaction score
181
Habari wana JF!

Ni dhahili kuwa 2020 rushwa ni kigezo kikuu cha kukubalika katika mchakato wa kupata wagombea wa ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (ccm)! Na hili limelalamikiwa na tumelilalamikia tangu mchakato haujaanza , Ila penye udhia penyeza rupia ndio staili. Mwenyekiti wetu mh rais jpm, katibu mkuu mh bashiru ali na baadhi ya wajumbe waaminifu wa kamati kuu CCM taifa wana kazi sana mwaka huu sababu sarakasi ni nyingi, ni mwendo wa kushindana fedha tu.

Jimboni ukonga kabla ya mchakato wa kura za maoni kuna baadhi ya wagombea waliitwa na takukuru kwa rushwa mara kadhaa, waliitwa na kamati ya maadili wilaya ya ilala mara kadhaa nk.

Wakati na baada ya mchakato malalamiko yamekuwa mengi mno na mengi yamepelekwa ngazi mbali mbali, kuanzia ccm mkoa dsm kwa katibu hadi kwa viongozi wa kitaifa . Shaidi mbalimbali zimewasilishwa mkoani na taifa za rushwa ya wazi wazi , unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na uhusika wa baadhi ya watu wa takukuru na usalama ngazi ya wilaya nk.

Kuanzia namba moja hadi nne (1-4) walikuwa katika tuhuma hizo. Aliyekuwa namba 1 (jerry silaa) , namba 2 (r.Masegese ) na namba 3 (m.Msofe); na nne wote kwa nyakati tofauti walishaitwa na kamati ya maadili kwa rushwa, kuanza kampeni mapema na makosa mengine ya kinidhamu.

Cha kushangaza katika kikao chake cha kutoa mapendekezo kwa kamati kuu ya ccm; kamati ya siasa mkoa kikiongozwa na mama kate kamba kimependekeza namba 2, namba 3 na ndugu a.Tukiko ili waendelee na mmoja wapo apeperushe bendera ya ccm ukonga 2020 kwa nafasi ya ubunge. Hii imevuja sababu wahusika wanalaumiana katika grup sababu aliyehonga mil. 3 kwa wajumbe 11 wa kamati ya siasa mkoa wa dsm amekuwa wa pili (masegese) na aliyetoa mil.2 kwa wajumbe kawa wa 3 na a.Tukiko mmemweka namba 1 ingawa katoa m.1.5 kwa kila mjube.

Kwanza (1) wote wana doa la maadili na rushwa

(2) Mnawaandalia njia ya kushinda wapinzani, sababu hii mizigo haiuziki

(3) Hamkuzingatia jenda,sababu wadada wanaohitajika tuwape jimbo hawana fedha za rushwa wengi wao

(4) Mama kate hata kama unajiandaa kupumzika, hivyo huna cha kupoteza kwa maamuzi haya ya kuangamiza chama, bado umejiharibia sana sana. Ondoka kwa heshima.

(5) Kwa kuwa watu hawa wanatamba washaonana na mwenezi (h.Polepole ) hivyo atawabeba, mwenezi tunza heshima yako... Usije ondoka kwa rushwa za ukonga. Tenda haki.

(6) Kumkata Jerry na kumuacha Masegese na Msuya ni kituko cha karne. Tofauti yao ni majina tu na jinsi walivyopata fedha za kuhonga; wakati masegese kakopa mil.50 ya kuhonga benk, jerry kadondoshewa fedha na ridhwani jk ! Wote ni vinara wa rushwa.

Ukonga inajua kuwa mmetumia ugeni wa katibu wa mkoa ccm (ana wiki ya 2 kazini); mwenezi kuwa bize na harusi na ugeni wa mkuu wa mkoa kufanya rafu na kuendekeza njaa.

Mwisho: acheni kumchosha mwenyekiti wa CCM taifa Mh JPM, ana mengi sio kuangalia rushwa tu.

Msilazimishe kuliweka rehani jimbo la Ukonga.
 
Hii ni aibu tena ya mwaka 2020 kwa CCM MKOA WA DSM KUPITIA JIMBO LA UKONGA. Mungu kawaumbua. Ripoti kabla haijafika wanakoipeleka CC kwa Honorable J P Magufuli na jopo lake ishavuja. Aibu sana sana kwa CCM Mkoa wa DSM, wajitafakari sana. Huyo Tukiko hata mtaani kwake hawamfahamu imembeba hela tuu ya watoa maamuzi, ndi maana alipata kura 0. Huyo masegese ni majohe tu na fedha inambeba pamoja na tuhuma nyingi. Huyo msofe naye kadhalika, amalize fedha anazolipa TAKUKURU za ujenzi wa zahanati alizokula alipokuwa diwani.

Kwa nini tunajidhalilisha CCM hadi tunaonekana vilaza ?

Tuleteeni vituko tuwape wapinzani tena; AU MMETUSAHAU VIONGOZI WETU TULICHOFANYA 2015?
 
MH POLEPOLE ANATAJWA SEHEMU NYINGI. KAKANGU UNAKOSA UHALALI WA KUWA KIONGOZI. JITAFAKARI. RUSHWA NA KUBEBA WAGOMBEA KUTAKUCHAFUA SANA BRO.
Akiongea utadhani kweli ni mzalendo , muadilifu !Kumbe lol, ukijipeleka tu kama dada utatoa mzigo kama kwaHeri James au rushwa ya kutosha. Hana huruma kabisa
 
Hii ni aibu tena ya mwaka 2020 kwa CCM MKOA WA DSM KUPITIA JIMBO LA UKONGA. Mungu kawaumbua. Ripoti kabla haijafika wanakoipeleka CC kwa Honorable J P Magufuli na jopo lake ishavuja. Aibu sana sana kwa CCM Mkoa wa DSM, wajitafakari sana. Huyo Tukiko hata mtaani kwake hawamfahamu imembeba hela tuu ya watoa maamuzi, ndi maana alipata kura 0. Huyo masegese ni majohe tu na fedha inambeba pamoja na tuhuma nyingi. Huyo msofe naye kadhalika, amalize fedha anazolipa TAKUKURU za ujenzi wa zahanati alizokula alipokuwa diwani.
Kwa nini tunajidhalilisha CCM hadi tunaonekana vilaza ?
Tuleteeni vituko tuwape wapinzani tena; AU MMETUSAHAU VIONGOZI WETU TULICHOFANYA 2015?
Kama vipi kataneni mapanga nyote mpotee hamna faida yoyote kwa jamii
 
Ukonga Tunamtaka Mr Masegese. Tunamjua hapa ni mkaazi mwenzetu. Kijana wa kawaida kabisa hizo Rushwa lambda mmemsaidia kutoa maana hata hizo hela hatujui Kama anazo.

Tunachojua ni mtu wa watu. Mpenda maendeleo na kwa kweli huyu anaijua Ukonga.
 
Tazama jinsi tunavyoteswa na matendo yetu wenyewe, sisi sote tu walafi, Bali twamlalamikia yeye aliyekula zaidi, na huku twajua ya kuwa tamaa yetu inatutaka nasi tule kama yeye au zaidi ya yeye.

NENO LINASEMA:

2 Wakoritho : Mlango 10
11 Mtu kama huyo na afikiri hivi, ya kwamba jinsi tulivyo kwa maneno katika nyaraka tusipokuwapo, ndivyo tulivyo kwa matendo tukiwapo.
 
Ukonga Tunamtaka Mr Masegese. Tunamjua hapa ni mkaazi mwenzetu. Kijana wa kawaida kabisa hizo Rushwa lambda mmemsaidia kutoa maana hata hizo hela hatujui Kama anazo.

Tunachojua ni mtu wa watu. Mpenda maendeleo na kwa kweli huyu anaijua Ukonga.
AFADHALI USHASEMA HUJUI KAMA ANAZO MKUU SABABU HUMJUI ! TAKUKURU KAITWA MARA NGAPI ? MAADILI JE ? SARE ALIZOWASHONEA WANA MAJOHE NI SADAKA ? USITAKE TUMVUE NGUO ZAIDI ? KWANINI ALIPATA KURA KWENYE SANDUKU LA KATA YA MAJOHE TUU ?!?
 
jerry bwana, umeamua kumwagia ugali mchanga.
well, kimsingi siwaombei jema lolote lile nyie watu, hivyo nafurahi sana kuzisikia tabu na manung'uniko yenu, tena dua zangu ni kwamba shida hizi ziwafuate bila kikomo, zikiamua kuwafuateni mpaka makaburini mwenu ziwafuate tu sababu hamna namna sasa.
 
Back
Top Bottom