Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
KAMATI YA SIASA MKOA WA SIMIYU IMEENDELEA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI WILAYA YA BARIADI, HALMASHAURI YA BARIADI TC
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Simiyu chini ya Mwenyekiti wake Ndg Shemsa Seif Mohammed leo tarehe 04/12/2023 imeendelea na ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020/2025 ndani ya Mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Bariadi, Halmashauri ya Bariadi TC
Katika Halmashauri ya Bariadi TC Jumla ya Miradi 11 yenye thamani ya zaidi ya bilion 10.25 iliyotolewa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mwenyekiti wa CCM ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekaguliwa.
Miradi hiyo ni pamoja na;
1. Ujenzi wa Zahanati ya Gisadi,iliyopo Mtaa wa Bupandagila, kata ya Nyakabindi.
2. Ujenzi wa Mradi wa Maji Mtaa wa Old Maswa kata ya Nyakabindi.
3. Kuona Huduma za Afya zinazotolewa kwenye Kituo Cha Afya Ng'wang'wali
4. Ujenzi wa Jengo la Wagongwa wa Nje(OPD) Hospitali ya Mji Somanda kata ya Somanda.