PreGE2025 Kamati ya Ushauri Mkoa wa Dar waridhia jimbo la Ukonga ligawanywe mara mbili

PreGE2025 Kamati ya Ushauri Mkoa wa Dar waridhia jimbo la Ukonga ligawanywe mara mbili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) ikiongozwa Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila leo Machi 24, 2024 imepokea na kuridhia mapendekezo ya Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Ilala (DCC) ya kuligawa jimbo la Ukonga lililopo Wilaya ya Ilala kuwa majimbo mawili ambayo ni jimbo la Ukonga na jimbo Kivule ambapo mchakato unaofuata ni kuwasilisha mapendekezo hayo kwenye mamlaka husika ikiwemo OR-TAMISEMI ili kupata ridhaa.

MADAI YA TUNDU LISSU KUHUSU UWIANO WA IDADI YA WATU NA WABUNGE ITAZINGATIWA ?

Tundu Lissu No Reforms No Election, moja wapo ya reforms ni kuhakikisha uwiano wa watu wanaowakilishwa na wabunge urekebishwe :

"DAR ES SALAAM ILITAKIWA KUWA NA MAJIMBO 25 SIO KUMI" - TUNDU LISSU

View: https://m.youtube.com/watch?v=s4OofpFoCr4

Gerrymandering ni kutengeneza mipaka ya majimbo bunge mengi, mitaa, vitongoji kwa kuweka mipaka / au wingi lengo ili kuhakikishia kupata wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa, vitongoji na vijiji wengi na kushinda uchaguzi.

MICHEZO MICHAFU YA KUHONGA NA KUGAWA MIPAKA YA MAJIMBO

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu kwa mifano hai ya michezo ngazi ya jimbo akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo

Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya wapiga kura .

Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.

Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania

Huko nchini Kenya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi yaani IEBC ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza mipaka ya majimbo ktk Kenya yote inayotumia formula ya idadi ya watu ktk sehemu ndiyo itatoa mwangaza kutakuwepo wabunge wangapi. Sababu ni kuwa nchini Kenya demokrasia inaangazia kuwa wabunge wanawakilisha watu kwa kura na siyo eneo.

Tofauti na Tanzania ambapo ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC haina nguvu kikatiba kutengeneza majimbo kwa kufuatana na idadi ya wapiga kura.

Mfumo huo wa kuangalia eneo hata kama lina wapiga kura wachache na kuwapatia idadi kubwa ya wabunge huku mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza yenye idadi kubwa ya wapiga kura inapewa wabunge wachache sana.

Sababu ni kuwa imeonekana maeneo yenye watu wengi ambao ni wapiga kura huwa wana tabia au mazoea ya kuchagua wapinzani hivyo kwa Tanzania wengi hao wanapewa wabunge wachache ili kudhibiti idadi ya wabunge wa upinzani wanaoweza kuchaguliwa . Parliament of Tanzania

Wawakilishi wa waangalizi wa chaguzi toka ndani na nje wameona mapungufu haya ya kuwa kuna maeneo yana wapiga kura wachache sana lakini ina wabunge wengi, huku kuna maeneo yenye wapiga kura wengi inawakilishwa na wabunge wachache sana na hii Indonesia kukosekana uwiano kati ya idadi ya wabunge na wapiga kura wao.

Source : Forbs Media
Tume ya Uhusiano na Uratibu Rasimu ya Warioba ililenga kuhakikisha ... Warioba alisema idadi ya wabunge isizidi 75, Bunge Maalum likasema..... soma zaidi : source : Hotuba ya Jaji Josefu Warioba kuhusu Rasimu ya Katiba ya Tanzania
Gerrymandering is to manipulate district boundaries, for political advantage.
 
Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa RCC mara baada ya kupokea mapendekezo hayo, RC Chalamila amesema mapendekezo hayo yamelenga kuboresha huduma kwa kuzingatia jimbo hilo ni kubwa na lina idadi kubwa ya watu hivyo kamati imepokea mapendekezo hayo na yatawasilishwa ngazi zingine kwa maamuzi zaidi
:FIRE: BREAKING NEWS :
26 February 2025

Tume Huru ya Uchaguzi Yaanza Mchakato Kupitia Tena Majimbo ya Kiuchaguzi, Vigezo 10 Kutumika

​


View: https://m.youtube.com/watch?v=n-EefdSzJ9Q
Ameyasema hayo leo mkoani Morogoro Jaji Jacobs Mwambegele Mwenyekiti Tume Huru ya Uchaguzi wakati akieleza namna ambavyo mchakato wa ugawaji wa majimbo unazingatia vigezo mbalimbali ikiwemo, wastani wa idadi ya watu.

Kwa majimbo ya mijini ni kuanzia wastani wa watu 600,000, majimbo ya vijijini kuanzia wastani wa idadi ya watu 400,000.

Idadi ya watu itakayo tumika ni iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS, kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

Mara ya mwisho tume ya uchaguzi ilichunguza na kugawa mipaka na kugawa majimbo ya uchaguzi mwaka 2015, ambapo majimbo mapya 26 yalianzishwa.
 
Dar es Salaam

RCC YATUMIA KIGEZO CHA SENSA YA TAIFA YA MWAKA 2022

View: https://m.youtube.com/watch?v=SuQHyWah25s
malengo ya kugawa jimbo ni kutoa huduma kwa wananchi

Katika kikao cha Kamati ya RCC ya mkoa wa Dar es Salaam inasema Wilaya pia ziongezeke mkoani Dar es Salaam kwa maslahi mapana kwa wananchi
Jimbo la Ukonga kata 7 na jimbo la Kivule kata 6 ..
 
Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) ikiongozwa Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila leo Machi 24, 2024 imepokea na kuridhia mapendekezo ya Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Ilala (DCC) ya kuligawa jimbo la Ukonga lililopo Wilaya ya Ilala kuwa majimbo mawili ambayo ni jimbo la Ukonga na jimbo Kivule ambapo mchakato unaofuata ni kuwasilisha mapendekezo hayo kwenye mamlaka husika ikiwemo OR-TAMISEMI ili kupata ridhaa.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa RCC mara baada ya kupokea mapendekezo hayo, RC Chalamila amesema mapendekezo hayo yamelenga kuboresha huduma kwa kuzingatia jimbo hilo ni kubwa na lina idadi kubwa ya watu hivyo kamati imepokea mapendekezo hayo na yatawasilishwa ngazi zingine kwa maamuzi zaidi

Soma pia: Shinyanga: Madiwani wapitisha pendekezo la Jimbo la Solwa kugawanywa mara mbili

Aidha RC Chalamila amesema baada ya kugawanywa jimbo jipya la Kivule litakua na kata sita ambazo ni Kipunguni, Mzinga, Msongola, Kitunda, Kivule na Majohe, jimbo hilo lina kilometa za mraba 128, idadi ya watu 431,736 na Jimbo la ukonga likibaki na Kata saba ambazo ni Ukonga, Chanika, Gongo la Mboto, Zingiziwa, Buyuni na Pugu Station likiwa na idadi ya watu 490,121.

Kawe Vipi???
Maana idadi ya watu ni kubwa
Kata ni nyingi +Eneo kubwa sana.
 
Ukonga imestahili ndilo jimbo lwenye wapiga kura wengi Tanzania.
 
Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) ikiongozwa Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila leo Machi 24, 2024 imepokea na kuridhia mapendekezo ya Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Ilala (DCC) ya kuligawa jimbo la Ukonga lililopo Wilaya ya Ilala kuwa majimbo mawili ambayo ni jimbo la Ukonga na jimbo Kivule ambapo mchakato unaofuata ni kuwasilisha mapendekezo hayo kwenye mamlaka husika ikiwemo OR-TAMISEMI ili kupata ridhaa.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa RCC mara baada ya kupokea mapendekezo hayo, RC Chalamila amesema mapendekezo hayo yamelenga kuboresha huduma kwa kuzingatia jimbo hilo ni kubwa na lina idadi kubwa ya watu hivyo kamati imepokea mapendekezo hayo na yatawasilishwa ngazi zingine kwa maamuzi zaidi

Soma pia: Shinyanga: Madiwani wapitisha pendekezo la Jimbo la Solwa kugawanywa mara mbili

Aidha RC Chalamila amesema baada ya kugawanywa jimbo jipya la Kivule litakua na kata sita ambazo ni Kipunguni, Mzinga, Msongola, Kitunda, Kivule na Majohe, jimbo hilo lina kilometa za mraba 128, idadi ya watu 431,736 na Jimbo la ukonga likibaki na Kata saba ambazo ni Ukonga, Chanika, Gongo la Mboto, Zingiziwa, Buyuni na Pugu Station likiwa na idadi ya watu 490,121.

Mnapoongeza majimbo itakuwaje. Wabunge wakiongezeka mtavunja ukumbi wa Bunge mjenge mkubwa kuliko wa sasa ? Sababu uliopo inatosha idadi ya sasa tu.
 
Back
Top Bottom