Kambi ya Mbowe kumeguka CHADEMA inaweza kuwa utakaso kwa dhambi ya Lowassa?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Huwa inasemwa CHADEMA ilisaliti msimamo wake ilipomchukua Lowassa na kmfanya mgombea urais mwaka 2015 kama hii ni kweli basi kuondoka kwa kundi la Mbowe CHADEMA inaweza kuwa sawa na utakaso kwa dhambi hiyo.

Ikumbukwe Mbowe na timu yake ndiye alikuwa kinara wa kumleta Lowassa CHADEMA mpaka akapewa jina la utani kamanda wa kubadili gia hewani, yeye pia ndiye aliyekuja na kauli mbiu ya Lowassa Mabadiliko, Mabadiliko Lowassa.

Sehemu kubwa ya walioondoka mpaka sasa walikuwa sehemu ya mafuriko ya Lowassa!
 
kwasabb hiyo,
Chadema imebaki crepa tu saivi dah!🐒
 
Yaani Mbowe akiondoka cdm pamoja na genge lake, kilio changu cha toka 2015 kuwa Mbowe hakustahili tena kuwa mwenyekiti wa cdm kwa kumuokota Lowassa, na kumpa nafasi adhimu ya kugombea rais. Kitendo cha kushindwa juzi kilinifurahisha mno, maana yalikuwa maamuzi sahihi ya wanacdm. Fundi Mchundo TrueVoter Retired Yericko Nyerere
 
Niseme, kabla ya kusoma yaliyomo ndani ya mada; mkuu 'Yoda' ni fundi mzuri wa kutengeneza vichwa vya mada aziwasilishazo humu; hata kama hukubaliani na maudhui ya mada zenyewe.

Sasa nakwenda kusoma mada.
 
Huwa inasemwa CHADEMA ilisaliti msimamo wake ilipomchukua Lowassa na kmfanya mgombea urais mwaka 2015 kama hii ni kweli basi kuondoka kwa kundi la Mbowe CHADEMA inaweza kuwa sawa na utakaso kwa dhambi hiyo.

Ikumbukwe Mbowe na timu yake ndiye alikuwa kinara wa kumleta Lowassa CHADEMA mpaka akapewa jina la utani kamanda wa kubadili gia hewani, yeye pia ndiye aliyekuja na kauli mbiu ya Lowassa Mabadiliko, Mabadiliko Lowassa.

Sehemu kubwa ya walioondoka mpaka sasa walikuwa sehemu ya mafuriko ya Lowassa!
Ukifanya dhambi tangu kale lazima utoe kafara ili Mungu akusamehe😀
 
Mpaka paka wa kufuga mtawasingizia safari hii kisa CHADEMA.
Yani No reform No election ni zaidi ya uume unavyo wasumbua CCM makalioni mkipiga makelele
Duh!
Yamekuwaje haya tena!
Sijui kama mkuu 'Yoda' anao uhusiano wowote na hao " wanaosumbuliwa makalioni"!
 
Yaani Mbowe akiondoka cdm pamoja na genge lake, kilio changu cha toka 2015 kuwa Mbowe hakustahili tena kuwa mwenyekiti wa cdm kwa kumuokota Lowassa, na kumpa nafasi adhimu ya kugombea rais. Kitendo cha kushindwa juzi kilinifurahisha mno, maana yalikuwa maamuzi sahihi ya wanacdm. Fundi Mchundo TrueVoter Retired Yericko Nyerere
Mkuu uliwaza mbali sana
 
Ukimaliza uje kutusimulia
Ukiwa na maana kuwa nami nilikuwemo kwenye mpango huo,au vipi, mkuu 'Bush Doktori'?

Wewe unaijuwa kambi yangu ni moja tu basi; Tanzania.

Msimamo wangu kwa ujio wa Lowassa CHADEMA wakati huo ulikuwa wazi. Lowassa alikuwa anavuma kwelikweli enzi hizo; na CHADEMA, kama ilivyo kwa chama chochote kinachofanya siasa za kweli, lengo lilikuwa ni kushika madaraka; "kuiondoa CCM madarakani", lengo ambalo mimi kila siku nasema, hata kama Mzee Rungwe angeamka siku moja na kuwa na uwezo huo, ningemuunga mkono; na baada ya CCM kuondoka, tunatafuta njia nyingine ya kusimamia maslahi ya waTanzania.

Kwa hiyo, kiufupi, niliunga mkono Lowassa kuingia CHADEMA kwa matumaini hayo, na sivinginevyo.
Lowassa wa wakati huo na kabla; hasa akiwa waziri mkuu; alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo; kuiondoa CCM madarakani, na CHADEMA kushika hatamu.

Lakini Lowassa aliyepiga Kampeni, akatokea kuwa ni tofauti kabisa na matarajio. Ndoto iliishia hapo.

Sasa nakwenda kusoma mada ya mkuu Yoda.
 
binaadamu wanafiki sana, si ndio nyie muliokua munapiga deki barabara lowasa kabla ya kupita?
 
Back
Top Bottom