Kambi ya Mbowe kumeguka CHADEMA inaweza kuwa utakaso kwa dhambi ya Lowassa?

Kambi ya Mbowe kumeguka CHADEMA inaweza kuwa utakaso kwa dhambi ya Lowassa?

Ukiwa na maana kuwa nami nilikuwemo kwenye mpango huo,au vipi, mkuu 'Bush Doktori'?

Wewe unaijuwa kambi yangu ni moja tu basi; Tanzania.

Msimamo wangu kwa ujio wa Lowassa CHADEMA wakati huo ulikuwa wazi. Lowassa alikuwa anavuma kwelikweli enzi hizo; na CHADEMA, kama ilivyo kwa chama chochote kinachofanya siasa za kweli, lengo lilikuwa ni kushika madaraka; "kuiondoa CCM madarakani", lengo ambalo mimi kila siku nasema, hata kama Mzee Rungwe angeamka siku moja na kuwa na uwezo huo, ningemuunga mkono; na baada ya CCM kuondoka, tunatafuta njia nyingine ya kusimamia maslahi ya waTanzania.

Kwa hiyo, kiufupi, niliunga mkono Lowassa kuingia CHADEMA kwa matumaini hayo, na sivinginevyo.
Lowassa wa wakati huo na kabla; hasa akiwa waziri mkuu; alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo; kuiondoa CCM madarakani, na CHADEMA kushika hatamu.

Lakini Lowassa aliyepiga Kampeni, akatokea kuwa ni tofauti kabisa na matarajio. Ndoto iliishia hapo.

Sasa nakwenda kusoma mada ya mkuu Yoda.
Ila Kalamu bana, yaani Lowassa ashindwe kwenye uchaguzi wa ndani wa ccm, ila aweze kuishinda ccm nje ya ccm? Lowassa yule ambaye hata kusimama dakika tano jukwaani alikuwa hawezi?
 
Back
Top Bottom