Kamera kubwa zaidi duniani ilivyopiga picha za kushangaza zaidi

Kamera kubwa zaidi duniani ilivyopiga picha za kushangaza zaidi

Excel VBA

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2025
Posts
966
Reaction score
2,211
8ed1c4c0-bcc4-11f1-874a-09d072a27eab.jpg.webp

Juu katika Milima ya Andes nchini Chile, Kituo cha Uchunguzi cha Vera C. Rubin kina kamera kubwa zaidi ya kidigitali kuwahi kujengwa duniani, mashine iliyoundwa kunasa picha za Ulimwengu kwa undani ambao haujawahi kufikiwa hapo awali. Ujenzi wa kituo hicho ulianza mwaka 2015, na kilitoa picha zake za kwanza mwezi Juni 2025, hatua iliyoashiria mwanzo wa misheni yake ya miaka kumi ya kuchunguza anga.

Darubini yake yenye kipenyo cha mita 8.4 (futi 28) imebeba kamera yenye ukubwa unaokaribiana na wa gari dogo na uzito wa takribani tani tatu. Kamera hiyo hunasa picha zenye megapikseli 3,200, zikiwa na kiwango cha maelezo cha hali ya juu kiasi kwamba picha moja pekee inahitaji takribani televisheni 400 za Ultra HD ili kuoneshwa katika ubora wake kamili.

Kwa hiyo, darubini hiyo itapiga picha za nini hasa?

Kila baada ya usiku tatu, kituo hicho cha uchunguzi kitachanganua anga lote la kusini, kikipiga picha za kila galaksi, nyota na asteroidi inayoonekana.

Kwa kurudia uchunguzi huu kwa kipindi cha miaka kumi, wanaastronomia wataunda rekodi ya kina zaidi kuwahi kufanywa ya mabadiliko ya Ulimwengu, kama filamu ya muda mrefu (time-lapse) inayoonesha jinsi anga linavyobadilika kwa muda.

Kwa kukusanya takribani terabaiti 10 za data kila usiku, kituo hicho kitawasaidia wanasayansi:

Kuchora ramani ya athari zisizoonekana.
Kugundua asteroidi ambazo hazijawahi kuonekana hapo awali.
Kushuhudia nyota za mbali zikilipuka na kuwa supernova kwa wakati halisi.
Huu hapa ni muhtasari wa picha na matokeo ambayo kituo hicho kimekusanya katika mwaka wake wa kwanza wa shughuli.
CC: BBC
 
Back
Top Bottom