Kamfumania mumewe na housegirl!!!!!



timu ya yanga imekataa kucheza mcheo na esticom ya malawi tatizo halisi waandaji walishindwa kuweka sawa kinachoendelea..yanga wamesema awawezi kuhakikisha mechi wakati timu yenyewe aijafik ..leo nimesoma gazeti waandaji wamesogeza mechi mpaka wiki ijayo

kwako mpwa kwanza naomba anikupe pole sana sana sanaaaaa ingawa siyo wewe ila damu ni nzito.
Pili samahni kwa kuchelewa kujibu nionavyo maoni yako yameshamfikia kutokana na maandishi yako kianachofanyika hapa ni uhalalisho tu kwamba ulipata mawazo haya alakini haya ndio halisi kayafanyie kazi yaani achape lapa

ndugu yangu siwezi kutoa maoni kwa maana sijui wamefunga ndoa ama lah na kama bado walikuwa ni wazinzi na huyo mdogo wako ni hjaki yake kupata alichovuna aijalishi amezaa wangapi ameishi nae muda gani
kumuokoa mdogo wako sio kuvunja ndoa ama kuachana nae..zipo ndoa nyingi za ushahidi mpwa watu walizikimblia kutoa maoni yao wengine leo hii wameama hadi na makanisa na mitaaa waliokuwa nayo wakikaa na wanandoa baada ya kuachana kwa muda na kurudiana nakuanza kuwachamba waliokuwa wanashadadia

onyo tu ama angalizo
usiwe mwamuzi wa ndoa za watu kama awajafunga ndoa basi asilalamike amakukulalamikia maana anakulalamikia kama nani ??shemeji no...kaka ulipokea mahari no..........nakumbuka mdogo wangu mmoja alimfumania hawara yake miaka 3 ingawa alimwita mke kisa kazaa nae,,ndoa ingekuwa kuzaa wangapi wanaenda makanisani wakiwa na vitumbo vimesheni makontena ya kufyatulia matofali??

Kuwa makini na utakachotoa wazo lako ni muhimu ila maamuzi yao binfsi ni muhimu zaidi

wape happy new yr na nakuhakkikishia kwa maneno haya usishangae wakikuribisha nyumban kwao mwaka mpya nakwambia
 
Hapa kuna tatizo, iweje wote wawili wawe na kasoro?: matatizo katika mirija, low sperm count. Any way, najua ni katika kujua chanzo cha kutokupata mtoto ambaye ni muhimu katika kuleta furaha na amani katika ndoa. Muulizi mdogo wako kama aliwahi kumfumania kabla ya tukio hili, na kama ni mara ya kwanza, tafadhaali linaongeleka na kufiikia ufumbuzi. Ndoa ni heshima hata kama hamna mtoto kuna haki nyingi zinaambatana na ndoa, kuvunja ndoa kwangu mimi katika hatua hiyo itakuwa ni jambo la haraka sana, kila mtu ana mapungufu yake, kila mara ni kutoipitisha ajioni bila kutafuta ufumbuzi katika yale yaliyoonekana kasoro. Ushauri kwako: Umefanya vizuri kumuita mdogo wako, mshauri aache hasira, atulie, mwite shemeji yako aje hapo washauri kwa pamoja, na lamaana Msamaha utolewe kama huyo bwana atakiri kosa lake, ingawa pengine watu wa inteligensi watasoma hili lakini nadhani kumpeleka mbele ya sherika kama mbakaji inabidi kwanza kukaa na kushauriana na kuona mfanyaje bila kutumia hasira. Tunakutegemea kulimaliza na kutujulisha.
 
jamani kama watu wa jf ambao by average
unaweza sema wana access na legal advice
but still watu'hawaelewi'
'kubaka' ni nini.....

je ma house girl watalindwa na nani???????

hii inatisha
Mi nilipoelewa hivo ndio niliamua kuacha kwanza kuchangia!
 

unaona mambo yalivyo? Huwezi niambia mwanaume anayebaka kusitokee michubuko,labda kama anakabamia. Huyo mdogo wake alipanic tu,na hizo kelele zitakuwa ni miguno ya kunogewa. Lakn sperm zinatafutwa kwenye urine? Sperm huwa tunacheki kwenye k,nguo na near by structures kama hajaoga. Cjawahi ckia kwenye mkojo,huko ni upt
 

wewe upomakini sana
 
mhhh hapa kuna ugumu sana kati ya kanisa na sheria, ila kwa upande wa sheria huyu bwana ni mbakaji na anaonekana hajutii kosa lake hatua alofikia ya kuwafukuza wote imeniuma zaidi,hebu binti mpelekeni kituoni mripoti mtepewa pf3 akapimwe though siku zimepita but lazima kutaonekana michubuko na mikwaruzo. lapili huyo dada ana ground zote za kudai talaka ikiwemo hii ya uzinzi na ubakaji ni jambo lisiloweza kuvumilika,tatu aende mapema kwenye baraza la uzuluhishi wana procedure zao atapewa barua ya kwenda mahakani bila hiyo hataweza kufungua shauri la talaka.
huyo bwana hafai hata kuishi duniani lol...
kanisa wanasema ndoa haivunjwi lakin sheria za nchi ziko juu ya kanisa na hata yesu mwenywe alitamka wazi kuhusu uzinzi kama chanzo cha kutengana.
 
Kwahiyo BAK wewe binti akikudanganya ana umri wa miaka 15 na ukaamini, ukamchukua hivyo hivyo alafu ikaubuka kesi na kwenye process ikagundulika kwamba alikua na 18, utaona maamuzi yako uliyofanya kwa wakati ule yalikua SAWA?

Mkuu Lizzy, hii kesi haimhusu kabisa BAK kwa hiyo naomba tujadili kesi iliyoletwa na Kaunga. Kaunga kasema wazi kwamba hana uthibitisho wa huyu HG kama kweli ni under age au la. Kaunga pia ameandika hapa kwamba pamoja na majirani kusikia binti anapiga kelele lakini mdogo wa Kaunga ambaye ni mke wa mtuhumiwa anadhani kwamba HG kwa kukataa kumpa ushirikiano (anataka tu kulipwa mshahara wake ili arudi kwao) basi inawezekana kabisa huyu HG na Shemeji wa Kaunga hizi shughuli wamezianza siku nyingi sana. Je kuna facts za kutosha za kumtia Shemeji wa Kaunga hatiani? BAK anasema hakuna facts kama hizo inawezekana kabisa huyu binti si under age na pia inawezekana kabisa alishiriki katika tendo la ndoa kwa ridhaa yake mwenyewe na hivyo hapa kosa la Shemejiye Kaunga ni kusaliti ndoa yake na kutembea na huyo HG.

Tusubiri labda Kaunga anaweza kuja na ushahidi zaidi ambao utasaidia ama kumtia hatiani Shemejiye au kumnusuru ila kwa sasa hakuna ushahidi wa kuhitimisha kwamba binti ni under age au alibakwa. Hilo ndio neno la BAK. Tuwe na subira ili kuweza kufikia hitimisho la haki badala ya kufikia hitimisho huku kukiwa bado kuna utata chungu nzima kuhusu tukio halisi.

 

nakubaliana nawe Kolelo.
Unajua tatizo ni kwamba watu humu wamelalia upande mmojatu wa house G bila kubalance pande zote ,
Naamini mtoa maada atachukua ushauri huu kwa nia njema kabisa,
ndoa ni kitu nyeti.
 
Watu mnacomplicate tu hapa. In ideal condition huyu mwanaume amekosa sana. But in real condition sio makosa ya kusababisha kuvunja ndoa haya. Wengi mnaoshabikia ndoa ivunjwe najua hampo ndoani.
 
Watu mnacomplicate tu hapa. In ideal condition huyu mwanaume amekosa sana. But in real condition sio makosa ya kusababisha kuvunja ndoa haya. Wengi mnaoshabikia ndoa ivunjwe najua hampo ndoani.

Kwa mujibu wa maneno yako ndoa ni show tu kwa watu wa nje wajue mmeoana, wakati wenyewe ndani ubaradhuli kama huu wa kubaka vitoto visivyo sauti ni kitu cha kawaida tu hata sio cha kushangaza sana, au vipi?
 
Watu mnacomplicate tu hapa. In ideal condition huyu mwanaume amekosa sana. But in real condition sio makosa ya kusababisha kuvunja ndoa haya. Wengi mnaoshabikia ndoa ivunjwe najua hampo ndoani.

nami nlishaona toka mwanzo, wengi wasio na ndoa ndo wanaona kuvunja ndoa ni kitu rahisi,nadhani ni mpango wao mahususi wakutaka kumwiba mume wawatu.
Hekima ikitumika yataisha kwa uzuri kabisa, na amani itarudi na ndoa itapona na binti hatapatashida kisaikolojia.
 
Kwa mujibu wa maneno yako ndoa ni show tu kwa watu wa nje wajue mmeoana, wakati wenyewe ndani ubaradhuli kama huu wa kubaka vitoto visivyo sauti ni kitu cha kawaida tu hata sio cha kushangaza sana, au vipi?

nani kakwambia kila ndoa mume ni mbakaji,
hio imetoka tena ni nadra mno,
ndoa ni taasisi ya amani ,furaha na kuvumiliana inapobidi.
 

This is called complacency, which goes hand in hand with enabling and justification.
 
Mpe muda na nafasi atafakari na kuamua yeye mwenyewe. Usitumie hasira zako (ref. AshaDii's post) kumshauri avunje ndoa yake, anaweza kuja kukulaumu baadae.
 
Kwa mujibu wa maneno yako ndoa ni show tu kwa watu wa nje wajue mmeoana, wakati wenyewe ndani ubaradhuli kama huu wa kubaka vitoto visivyo sauti ni kitu cha kawaida tu hata sio cha kushangaza sana, au vipi?

Nilisema tokea mwanzo kuwa ndoa ni ful package ya matam na machungu. hayatenganishiki. Lililotokea kwenye ndoa hii ni dogo sana ukifananisha na machungu mengine. huu unaouita ubakaji ni subjective. kwangu sion ubakaj hapa, na kwa kubase kwenye stor ya huyu dada, sion hatia kwa mwanaume huyu.
 
Kaunga:
Tafadhali nikuombetena mtulie hasira zipungue na kuvunja ndoa isiwe chaguo la kwanza,
kwani maisha yanaweza kuendelea na tatizo likatatuliwa kwa amani bila kupelekana mahakamani na kupelekea ndoa kuvunjika.
 
nani kakwambia kila ndoa mume ni mbakaji,
hio imetoka tena ni nadra mno,
ndoa ni taasisi ya amani ,furaha na kuvumiliana inapobidi.

the idea kwamba ndoa ni taasisi muhimu sana
kiasi hata 'wahalifu' wasamehewe kwa kuwa wapo kwenye ndoa is absurd....to say the least.....
 
Mpe muda na nafasi atafakari na kuamua yeye mwenyewe. Usitumie hasira zako (ref. AshaDii's post) kumshauri avunje ndoa yake, anaweza kuja kukulaumu baadae.

Nimeupenda mchango wako, yaonyesha unauwezo mzuri sana wa kuona mbali.
 

Wajuaji watakuletea ligi tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…