Kamfumania mumewe na housegirl!!!!!

Two mistakes do not make one right. Funzo hili ni muhimu sana kwenye maisha...hata hivyo tuangalie tunasaidiaje ndoa hii kuliko kukimbilia kwenye quick fixes. Inachoonyesha hapa kuna tatizo kwenye ndoa au kina tatizo la kimaadili kwa huyu bwana. Lakini maji yameshamwagika ni lazima tutafute a very good clear cut solution. Kama ni mkristo au anaamini mafundisho ya biblia ningemshauri biblically, jambo la kwanza huyu bibie amsamehe mumewe. Akumbuke ni mara ngapi yeye amekosea wengine, je, ingekuwa solution ya haraka kwenye kila kosa ni kiachana basi hata yeye huenda angeshafukuzwa kazi, angesha kanwa na wazazi nk. Asamehe. Kwa binti mtendwa naye anapaswa kusamehe na kiwasamehe wanaume wote. Wengi wamebaki na uchungu wa ndani kwa wanau,e wote kwa ajili ya mwanaume mmoja aliyemtenda vibaya. Hii haitamtendea mema. Binti anapaswa kuondoka hapo nyumbani ili kupunguza msongo wa mawazo na kuanza maisha mengine na kuwapa mume na mke nafasi ya kutengeneza ndoa yao upya. Mama mwenye ndoa yake a-revisit priorities zake. Anao muda wa kutosha na mumewe au amekuwa mama Bsy? Anamuda wa kuzungumza na mumewe na kufanya recreations za kutosha au ni mama na jiko, mama na kazi na kuyaacha majukumu mengine kwa wasaidizi? Ni yeye anayeandaa chakula na kumtengea mumewe au ni wasaidizi? Biblia inasema mke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Kutafuta kunapozidi vipimo lazima tujiulize ili nani aje avifaidi? Lini? Mnaweza mkatafuta at the expense of your relationship mkaishia kupoteza vyote. Kumbuka unaweza ukapata kazi na biashara nyingine wakati wowote lakini hakuna mbadala wa ndoa. Kwa mwanaume anahitaji kuonyeshwa amesamehewa tu atajirudi mwenyewe. Aidha mngepata spiritual counsellor kwa watu hao ingesaidia sana. Mungu wa amani na kupe amani ili uwe sehemu ya suluhisho na si kiwa sehemu ya tatizo. Nawasilisha kwa ufupi toka simu ya mkononi
 
Kwahiyo watu wanataka wamuibe kwa matumaini kwamba atajirekebisha na kuanza "kuplay mume mwema" ipasavyo?

mpaka sasa naamini kishajirekibisha so atakua ni mume bora, nadhan waendeletu na mamsapu wake wale raha ati!
 

@mkulima wa kuku.
Kiukweli unachukua namba ya juu kabisa kwa kua na ushauri makini na wenye manufaa tena waonyesha ni muelewa wa hali ya juu na unaona mbali,
nadhani"kaunga" akipata ushauri huu utamsaidia sana na utamfanya awe na utu.
Big up!
 
Hapa tu ndio huwa pananikatisha tamaa mie kuendeleza mijadala!! Sasa jazba zinahusiana nini na nilichokiandika my dear, au umejisikia tu kunisemea hayo??

it's ok.kapipi, labda ni mtazamo wangu tu mkuu, haya tuendele na mjadala.......!
 
lizzy
naomba utizame hili jambo kwa umakini jaman.

Nimetazama sana.Sema sitaki kuwa mmoja wa wale wanawake wanaoishi na wanaume wanaoMOLEST watoto wao, kisa mapenzi.
 
mpaka sasa naamini kishajirekibisha so atakua ni mume bora, nadhan waendeletu na mamsapu wake wale raha ati!

Kwa uhakika gani ndugu?? Kuna wanaume wanafiki balaa, yaani hajutii kosa alilolifanya bali anajuta na kujilaumu kwa 'nini amekamatwa'!!! Kwa huyu wa hivi wala usitarajie kujirekebisha, bali tarajia kwamba atatafuta njia mbadala ya kumfanya asifumaniwe tena!
 
Nimetazama sana.Sema sitaki kuwa mmoja wa wale wanawake wanaoishi na wanaume wanaoMOLEST watoto wao, kisa mapenzi.
lizzy
Wadhani unapanga kua na wanaume wa aina hiyo, hilo nijambo laweza tokea wakati wowote ata kwa yule unayemwamini sana.
Ndo ujue binadamu ni binadamu tu, yuko na mapungufu kadhaa ambayo yanasubiri muda wake wa kujidhihirisha.
Binadamu si malaika ndugu
 

ha ha ha usinchekeshe usiku jaman!
Ila ujue ni baadhi tena wachache ingawa sina takwimu kwa sasa lakini wengi wana regret na kujirud haraka.
 
Kwahiyo ukishajua huyo mtu ni wa ajabu unatolerate kwasababu hukuchagua kua na mtu wa aina hiyo?
Kwasababu una mapungufu yako utamwacha mwanaume aonyeshe yake kwa mwanao?
 
it's ok.kapipi, labda ni mtazamo wangu tu mkuu, haya tuendele na mjadala.......!

Mpaka hapa nimeshapoteza nilichokuwa nahitaji kukijadili, naomba tuelendelee kwa reply tu!! Ila kusema kweli hujanitendea haki, ningefurahi kama ungenikosoa ili nipate kuiona point na sio kusema ni jazba tu, kwa sababu mambo kama haya si machanga sana kwangu!!
 

Hivi swala la kuibiwa kale ka keki mnadhani ni rahisi hivyo? Kweli kuvunja ndoa shuguli,lakin je huyo mke ana play part yake kama mke vilivyo kumlidhisha mmewe?
 
Kwahiyo ukishajua huyo mtu ni wa ajabu unatolerate kwasababu hukuchagua kua na mtu wa aina hiyo?
Kwasababu una mapungufu yako utamwacha mwanaume aonyeshe yake kwa mwanao?

Kwani kiapo cha ndoa kinavo sema ntavumilia kwa shida na raha {for better for worse} we ulidhaniaje?
Ndo mana leo hii ndoa hazidumu coz wanandoa wanataka raha tu,nakusahau upande wa matatizo hivyo kukosa uvumilivu kama unavoonyesha wewe, si kitu kizuri ndugu.
 
Hivi swala la kuibiwa kale ka keki mnadhani ni rahisi hivyo? Kweli kuvunja ndoa shuguli,lakin je huyo mke ana play part yake kama mke vilivyo kumlidhisha mmewe?

Huyo mume yeye ANALIDHIKA?
 
Wengine tunafanya kila kitu kwa kiasi.Hongera wewe mwenye uvumilivu bila huruma.
 

kama si machanga kwako basi natarajia kuona mchango wa maana ambao ni
" balanced" na sio kulalia pande moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…