kwa upande wangu yako mambo mengi, labda ningejibiwa ningeweza kushauri mwemwele -
1. Ushauri wa kwanza waende kanisani wakamwombe Mungu, wakatubu dhambi zao kwa kumaanisha kuziacha na kuokolewa,kisha waombewe watapata amani
2. akili ya kawaida waangalie uwezekano wa kuishi pamoja kwani huenda upweke unamsumbua mumewe
3. wasameheane na kuanza upya, kwani binadamu wanakosea
4. kuhusu watoto waende kanisani kwa walokole wakaombewe, nawahakikishia upungufu wao utaondolewa na watapata watoto wengi mpaka watakataa
5. wakati mwingine mumewe huenda anajaribu kutembea na wanawake wengine akidhani anaweza kupata watoto kutoka kwao na kusahau kuwa watoto wanatoka kwa Mungu, ni zawadi, hivyo hili nalo linaweza kuwa tatizo kwa mumewe, usisahau soma kipengele 4 hapo juu. Tafadhali usilipuuze hili kwasababu sifa ya mwanaume yeyote ni kuwa na watoto wake wa kuwazaa.
6. je hapo awali alikuwa ana tabia hizo au kama sivyo tabia hizo zimeanza kujitokeza lini
7. ubakaji wa hg, kisheria hata kama angekubali ni ubakaji, je aliijua tabia ya huyo HG wake kabla ya kumuajiri au ameletewa tu na mtu
8. Ndoa za Kikristo hazina talaka, na Mungu anachukia kuachana kwao, na ww ukishiriki kuvunja ndoa yao, Mungu mwenyewe atakuadhibu mpaka utashangaa na kujuta kwanini ulizaliwa
usiwe mtu avunjaye ndoa za watu bali awashaurio kuendelea kudumu katika ndoa zao kwa kuwakumbusha upendo wao wa kwanza
nikipata MAJIBU ninaweza kuchangia zaidi