Dr Mathew Togolani Mndeme
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 201
- 810
UTANGULIZI:
Kwa mara nyingine tena kumejitokeza “kamgogoro baridi” kati ya Kenya na Tanzania kanakofikirisha sana. Nimeona baadhi yetu tumekua wepesi kuilaumu serikali yetu kwa uharaka kutokana na kwa uamuzi "wa kibabe" wa kuifutia Kenya Airways kibali cha kuingia kwenye anga la Tanzania.
Nikiri kwamba hata mimi nilipoona barua ile kwa mara ya kwanza, niliwaza kwa haraka kuwa huenda tumekosea na tume-react kwa haraka bila kutumia diplomasia. Ila asubuhi nikiwa najadiliana na mmoja wa marafiki zangu juu ya jambo hili, tulipata swali ambalo lilinihamisha kwenye mtizamo wa awali. Kwa nini?
MOJA:
Kenya wamefungua anga lao leo kuruhusu safari za kimataifa. Katika kufanya hivyo, juzi walitoa orodha ya nchi 11 ambazo ndege zao na raia wake wanaruhusiwa kuingia Kenya na jana wakaongeza nchi kadhaa za Ulaya. Katika orodha hii sisi hatupo kwa maelezo kwamba sio moja ya nchi ambazo zimeoneshe kufanikiwa kudhibiri korona. Kwamba mtazamo huu ni sahihi au vinginevyo, sio hoja yangu kwa sasa. Wanajua wenyewe kwa nini wametuona hivyo.
MBILI
Wakati sisi haturuhusiwi kuingia anga la Kenya, shirika la Kenya Airways ambalo nalo limeanza safari za kimataifa leo, liliomba kibali cha kufanya safari za kuja Dar, Zanzibar na KIA. Safari za kuja Tanzania ni moja ya safari zenye faida kubwa kwa shirika la Kenya Airways. Bila choyo wala husuda sisi tukawaruhusu “kwa kuwapa cheti, hati na certificate”. Ndiyo, hata kama unadhani nimekosea kutumia maneno haya. Sisi ni wafugaji bwana: hatumnyimi jirani kupita nje kwetu akiwa anaswaga mbuzi kuelekea au kurudi toka malishoni.
UTATA
Ukiwaza vema hoja ya kwanza na ya pili hapo juu utaona kuna maswali kadhaa yanajitokeza na kuibua utata. Moja, kama sisi ni moja ya nchi ambazo bado kuna shida kubwa ya korona na raia wetu hawaruhusiwi kuingia Kenya, sasa kwa nini Kenya Airways ije Tanzania? Mbili, Kenya Airways inataka kuja Tanzania kumleta au kumchukua nani wakati Watanzania wana korona? Tatu, kwa nini ndege zao ziende kwenye nchi ambayo ina hatari ya kuwaambukiza korona? Hawawapendi watu wao?
Maswali haya yenye utata yanaibua SWALI LA MSINGI: Je, ni kweli kwamba Kenya wametubania kuingia kwao kwa sababu ya korona pekee au kuna jambo jingine?
Dakika chache zilizopita, waziri wa usafiri wa Kenya katangaza kwamba wametafuta suluhu kwa kuaongea na viongozi wa Tanzania na uamuzi wa kuifuingia Kenya Airways utabadilishwa leo. Hongera sana kwa pande zote. Huu ndio undugu na ujirani.
Ila pamoja na furaha ya suluhu hii kuna SWALI LA NYONGEZA LINAJITOKEZA. Kama wamekomalia kuhakikisha hawapotezi soko la ndege zao lenye faida kwao, watatuondolea pia kigezo cha kuwa nchi ambayo ina hatari ya kuwaambukiza Korona?
Nakuachia kazi nawe uendelee tafakari.
Mathew Mndeme
([email protected])