Kuna mambo ya hovyo yanayofanywa na wakenya dhidi ya watanzania, hii iko hivyo tangu miaka ya 70 kwa kujiona kuwa wako bora zaidi kuliko watanzania. Mpango wa kuifufua upya Jumuia ya Afrika Mashariki ulianza mwaka 1999 kwa juhudi za Rais Ben Mkapa na Rais Dan Arap Moi. Hata hivyo tabia za wakenya za dharau na ujuvuni hazijabadilika hadi siku ya leo.
Kitendo cha Kenya kuwanyanyapaa watanzania, ni endelevu hasa ukiangalia kile kinachoendelea kwenye mipaka yetu na kenya;.. Mipaka ya Lunga Lunga, Rombo, Namanga na Sirali yote imegubikwa na unyanyasaji dhidi ya madereva wa kitanzania wanaopeleka bidhaa huko. Kama hiyo haitoshi licha ya uvumilivu wetu, bado wameamua kuhamia kwenye eneo jipya la anga huku wakijua kuwa wao ndio wanufaika zaidi yetu.
Hatua zilizokwisha kuchukuliwa na kutangazwa na Mamlaka yetu ya anga zisiondolewe haraka kama huyo afisa wa Kenya ananyojishaua kuwa wameyamaliza. Kwa jinsi alivyokuwa anaelezea inaonekana kuwa hawajutii kitendo chao cha kijinga cha kuitenga Tanzania wakati ndiyo soko lao kuu. Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kulaani na kupinga kitendo cha kuruhusu ndege za Kenya kuingia Tanzani........ TCAA isitoe kibali hata kwa miezi mitatu na hata watakapotoa kibali safari zipunguzwe hadi moja au mbili kwa wiki. 😡 😡