Kamgogoro baridi kati ya Kenya na Tanzania, nani yuko sahihi?

EAC haina mashiko. Historia tunaijuia. EAC 1967-1977 ilidumu miaka kumi tu. Kenya hawajachange. EAC mpya haina maana. Nakuunga mkono bora tujikite kwenye SADC tu.
Serikali ijiandae vilivyo hakuna faida ya kudumu na EAC.
 
Wanasema eti kama mgonjwa wa Upungufu wa kinga mwilini anatumia ARV, basi ni nadra sana kusambaza utapiamlo huo kwa mtu mwenye afya njema.

Pengine KQ wanatumia ARV, au labda majirani mbuzi jike na sisi hatuna unasaba na madume yao.

Labda labda hizi, ni KUFUNGA tu biashara na wao, wakarushe hizo ndege kwenye nchi walizoziorozesha
 
Mimi nadhan ipo haja ya kuchapana kidogo ili mwenye nguvu apewe heshima yake.
 
Kuna mambo ya hovyo yanayofanywa na wakenya dhidi ya watanzania, hii iko hivyo tangu miaka ya 70 kwa kujiona kuwa wako bora zaidi kuliko watanzania. Mpango wa kuifufua upya Jumuia ya Afrika Mashariki ulianza mwaka 1999 kwa juhudi za Rais Ben Mkapa na Rais Dan Arap Moi. Hata hivyo tabia za wakenya za dharau na ujuvuni hazijabadilika hadi siku ya leo.

Kitendo cha Kenya kuwanyanyapaa watanzania, ni endelevu hasa ukiangalia kile kinachoendelea kwenye mipaka yetu na kenya;.. Mipaka ya Lunga Lunga, Rombo, Namanga na Sirali yote imegubikwa na unyanyasaji dhidi ya madereva wa kitanzania wanaopeleka bidhaa huko. Kama hiyo haitoshi licha ya uvumilivu wetu, bado wameamua kuhamia kwenye eneo jipya la anga huku wakijua kuwa wao ndio wanufaika zaidi yetu.

Hatua zilizokwisha kuchukuliwa na kutangazwa na Mamlaka yetu ya anga zisiondolewe haraka kama huyo afisa wa Kenya ananyojishaua kuwa wameyamaliza. Kwa jinsi alivyokuwa anaelezea inaonekana kuwa hawajutii kitendo chao cha kijinga cha kuitenga Tanzania wakati ndiyo soko lao kuu. Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kulaani na kupinga kitendo cha kuruhusu ndege za Kenya kuingia Tanzani........ TCAA isitoe kibali hata kwa miezi mitatu na hata watakapotoa kibali safari zipunguzwe hadi moja au mbili kwa wiki. 😡 😡
 
Nakazia tu kuwa, hata baada ya kufufua upya EAC, kuna wakati walianzisha mgogoro wa kutaka makao makuu ya Jumuia ya Afrika Mashariki yawe Nairobi badala ya Arusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…