Juma Wage
Member
- Sep 8, 2023
- 88
- 246
Mnamo mwaka 1976, Mwanamuziki maarufu nchini Kongo Franco Luambo Makiadi aliachia kibao chake "Kamikaze".
Kupitia kibao hicho, Franco ameeleza namna alivyovurugwa kimapenzi na binti mrembo "Kamikaze" aliyemsaliti kisha kwenda kuolewa na mwanaume mwingine.
Alichukulia kitendo hicho kama uasi wa kujitoa muhanga na alijiapiza kuto oa tena maishani mwake.
Kwa nini kamikaze?😊
Kamikaze kilikuwa kikosi cha marubani wa ndege vita za Japan waliokuwa wakijitoa muhanga kujilipua juu ya manowari za jeshi la Marekani wakati wa vita vya pili vya dunia.
Hakika kikosi hiki kilikuwa tishio kwa waingereza na wamarekani.
Miongo ikapita baada ya vita na sasa teknolojia imekuwa na kurudisha upya jina la KAMIKAZE.
Safari hii sio rhumba la Franco bali ni silaha matata ya kuangamiza.
Iran wakaja na KAMIKAZE, hii ndio habari ya sasa kwenye uwanja wa Medani.
Hizi ni ndege nyuki (drone) zenye kubeba milipuko kwa lengo la kumuangamiza adui kwenye eneo lengwa.
KAMIKAZE zimebadili mwenendo wa vita ya Ukraine, kilio sio cha mizinga bali ni drone zenye kumuangamiza adui mafichoni.
KAMIKAZE ndizo zilizomfanya ZELENSKY aichukie IRAN.
KAMIKAZE ndiye aliyemfanya Franco aichukie ndoa maisha yake yote.
Ndimi Juma Wage
Dodoma