Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Pambano la Mwakinyo na bondia kutoka Ghana limeshindwa kufanyika kwa kuwa Rais wa WBO, Samir Captan hakuwepo uwanjani kuleta mkanda. Maelezo ya Hassan Mwakinyo ni kuwa jamaa hajalipwa hela za mchezo huo.
Kwa kushindwa kuwepo kwa mkanda uliokuwa unashindaniwa pambano limeshindwa kuchezwa.
Fedha za mchezo hutolewa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa(TPBRC) ni jambo la ajabu kusema kuwa ameshindwa kulipwa kutokana na uhaba wa dola kwa kuwa hili pambano limepangwa muda mrefu.
Aidha taarifa za ndaani zinasema WBO haijakubaliana na refa aliyepangwa kuchezesha mechi hiyo, sababu iliyomfanya Rais wa WBO-Afrika aondoke na mkanda akarudi hotelini kwake.
Hata hivyo, TPBRC watatuambia nini tuelewe sisi tuliouza usingizi ili kumuona Mwakinyo?
Aibu yetu kwa mgeni kutoka Ghana aliyesafiri kuja kupambana kama taifa tunaipanguaje kwa kuonekana wahuni?
Pia soma: Je, Mwakinyo atatuwakilisha vyema dhidi ya Patrick kutoka Ghana?