Kamisheni ya Utalii Zanzibar: Nguo fupi marufuku kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani

Kamisheni ya Utalii Zanzibar: Nguo fupi marufuku kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kamisheni ya Utalii Zanzibar imewataka Watalii, Wafanyabiashara na Wadau wa utalii Zanzibar kuheshimu maadili ya Dini na Utamaduni uliopo Zanzibar kipindi hiki cha kuelekea mwezi mtukufu wa ramadhani.

Kamisheni imesema ni lazima Migahawa na sehemu za chakula zilizo nje ya Hoteli zifungwe hadi wakati wa jua kuzama (IFTAR) na kupiga marufuku kula, kunywa au kuvuta Sigara hadharani wakati wa mchana na kusisitiza Watu wakiwemo Wageni kuvaa mavazi yenye staha katika maeneo ya Umma.

Kamisheni hiyo imepiga marufuku uvaaji wa mavazi yanayoonesha sehemu za mwili na kuwataka Wadau wa Utalii Visiwani humo kuwakumbusha Wafanyakazi juu ya muongozo huo na kubandika matangazo pale inapobidi.

​
 
Morocco, Uturuki, Tunisia na nchi nyingi za kiislamu hawana ujinga huu wa kulazimisha watu kufuata masharti ya mashehe wachache. Imani ni ya mtu binafsi na kwenda pepo ni kwa mtu binafsi siyo jamii nzima.

Mavazi na vingine havimpereki mtu peponi. Bali Imani na matendo yako. Acheni watu wafanye mambo yao. Dini ni swala la mtu binafsi
 
Back
Top Bottom