Kamishna Camillus Wambura ateuliwa kuwa IGP Mpya. Sirro apewa Ubalozi Zimbabwe, Kingai ateuliwa kuwa DCI

Sukuma gang imekomeshwa[emoji23][emoji23][emoji23]
Sina hakika na ulicholenga hapa; lakini sioni "kukomeshwa" kwa yeyote katika uteuzi uliofanyika. Na siyo kwa huyo Kingai pekee, bali hata kwa hao wengine.
 
Wambura hakuwa kipenzi cha IGP
Sababu Wamhura alikuwa mtu wa misimamo mikali kwenye Proffession yake
Lakini nje utendaji wake ulionekana na wenye macho makali ndio maana kapata U IGP

Somo kutoka kwa Wambura ni kuwa mchapa kazi azingatie tu maadili ya kazi na mtu achape kazi yako vizuri iko siku uaminifu na kuchapa kazi na kuzingatia maadili kutalipa. Ujanja ujanja na uchawa huwa hauna future sana
 
Mbona mapolisi wote wanatoka Mara?!
 
Ndugu Rudi Shule. RAIS ndo boss wa majeshi yote na anaweza kumuamlisha IGP amteue fulan katika nafas fulan, na hkuna kuvunja Katiba. Kinachoangaliwa ni utawala bora. Kma MTU umemteua MTU mpe nafas atekeleze wajib bila interfearance
 
Akumbushwe kuwa huko zimba....aendako asijejisahau akatuzalia mtoto aina ya HAMZA!!!!
 
Takwa la katiba ni la Dola Sio matakwa ya mbowe wala samia!!

Bunge la katiba linapoteuliwa halitoingiza WABUNGE Hao WOTE wa CCM Bali wa kimkakati hasa waliopo nje ya Bunge hili!!

Vichwa vitaingia na Sio Hao watoto wa uchafuzi!!
Kasome sheri ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011. Tusibishane sana.
 
Ndugu Rudi Shule. RAIS ndo boss wa majeshi yote na anaweza kumuamlisha IGP amteue fulan katika nafas fulan, na hkuna kuvunja Katiba. Kinachoangaliwa ni utawala bora. Kma MTU umemteua MTU mpe nafas atekeleze wajib bila interfearance
Watanzania tuna kazi sana kusoma kitu na kuelewa nini kimeandikwa kabla ya kujibu nacho ni kipaji.
 
Polepole malawi huyu Siro zimbabwe yaani kama ni mimi nakataa uteuzi kutoka IGP wa nchi mpaka unaenda kufanya kazi Zimbabwe, Anyway nampongeza mama ameupiga mwingi sana,
Sijui kama unajua nguvu za Rais wa Nchi.
 
Hasira na komoa ya mama tunaoumia ni watoto
 
Nani kakuambia siro amestaafu upolisi? Katumbuliwa
Kwa umri wake Mimi naamini amestaafu,pia iliwahi kusemwa wakati wa awamu ya 5 aliongezewa muda tu.

Ila hata Kama ametumbuliwa bado anaenjoy Sana huyo, mshahara wa ubalozi siujui ila naamini Ni pesa nzuri
 
Kasome sheri ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011. Tusibishane sana.
Mchakato unarudi nyuma, tunaanza pale kwenye RASIMU kabla haijaenda hatua ya kupiga kura Bunge la Katiba

Tutaweka mbinyo vyama vya siasa vitoe idadi sawa ya wawakilishi, makundi mengine pia yatoe watu wao Kwa Umakini mkubwa wasiokuwa mapandikizi.

Hatutakosea kama mwanzo maana ujinga ni wakati wa kwenda tu, Si wakat unarudi.

Amini, Muda wa KATIBA mpya ni sasa.

Ameeeeen.
 
Ni kweli kabisa, katiba hiyo mpya ikipitishwa kwa utashi wa CCM itakuwa mbaya kuliko hii iliyopo. Inatakiwa machafuko au mapinduzi ndio katiba ya rasimu ya Warioba ipite.
 
Kingai kaulaa Naona IGP katoka kanda pendwa tena!

Soon tutasikia wakili Robert kidando yule alikua kiongozi wa jopo la mawakili wa serikali kwenye kesi ya mbowe nae kateuliwa kuwa jaji.

Kidando anaenda kuwa jaji mkuu.
 
Unaongea tu bila facts. Utaweka mbinyo wewe nani? Kisheria wabunge wote wa bunge la jamhuri ya Muungano wanakuwa wabunge wa bunge la katiba moja kwa moja... jiulize katika hao kuna wapinzani wangapi kwa sasa? Pia kisheria Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM akishirikiana na rais wa Zanzibar wanateua wajumbe 203 kuwa wabunge wa bunge la mabadiliko ya katiba. Hao marais wote wawili ni wajumbe wa kamati kuu ya CCM. Unadhani watafanya makosa ya kuteua watu walio kinyume nao kiitikadi? Vijana wa upinzani msiwe wapumbavu muwe mnajisomea mambo madogo madogo badala ya kutoka mapovu kama wehu.
 
Ni kweli kabisa, katiba hiyo mpya ikipitishwa kwa utashi wa CCM itakuwa mbaya kuliko hii iliyopo. Inatakiwa machafuko au mapinduzi ndio katiba ya rasimu ya Warioba ipite.
Rasimu ya Warioba itapitaje wakati lazima ijadiliwe na bunge la mabadiliko ya katiba? Yaani viongozi wa upinzani kuna John Pumbulu hawawafafanulii mambo mengi muhimu na kuishia tu kutaja rasimu ya Warioba.
 
Ni kweli kabisa, kama hiyo rasimu itajadiliwa na wabunge wa CCM waliopatikana kwa wizi wa kura, hapo itakuwa mbaya. Hayo mahesabu ya kujadiliwa na bunge hili la majizi ya kura hatuko nayo boss.
 
We ndo punguza mihemko.

Hakuna wa kuzuia ujio wa KATIBA mpya muda umefika.

Hizo Sheria zitatungwa upya, idadi ya wabunge itakuwa sawa kulingana na makundi husika.

2026 ni mwaka wa kukamilika KATIBA mpya.
 
Ni kweli kabisa, kama hiyo rasimu itajadiliwa na wabunge wa CCM waliopatikana kwa wizi wa kura, hapo itakuwa mbaya. Hayo mahesabu ya kujadiliwa na bunge hili la majizi ya kura hatuko nayo boss.
Mimi nashauri wapinzani wapambanie tume huru ya uchaguzi kwanza. Tume ikiwa huru watapata wabunge wengi hivyo kwa baadae itasaidia kupata katiba mpya. Tukilazimisha sasa hivi itakuwa haina maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…