Kamishna wa Ardhi Msaidizi - Dodoma Godfrey Mwamsojo amesema mgogoro wa Kiwanja Plot no 42 Kitalu B kilichopo katika Mtaa wa Image, Kata Kikuyu Kusini (South extension) Jijini Dodoma ni kwamba uhakiki umeonesha mmiliki halali ni Adelaide Henry Mkoko na si mama Exaud Sudda ambaye alikuwa akilalamika kuwa kiwanja hicho ni mali yake na nyumba yake imebomolewa.