Kamishna wa Kudhibiti dawa za Kulevya: Bangi ya Tanzania haifai kwenye Masoko ya Kimataifa

Kamishna wa Kudhibiti dawa za Kulevya: Bangi ya Tanzania haifai kwenye Masoko ya Kimataifa

hana jipya anabwabwaja tu wanakuja watu toka us ukimpa cha arusha anasizi tena anakuambia hii kitu bomba sana iko soomth tatizo kubwa ni bhange ambazo hazijakomaa zinaletwa town kwa biashara ila ukapata kitu from orkokolo ukila kete moja ukatafute sehemu uskilizie stimu
mtaani zimejaa kushabu hizo original kuzipata kipengele!
 
Swali.

Hivi wenzangu mnamuelewa huyu Jamaa?

Yaani bangi ingekuwa haifai watu wangekuwa wanalima na kuisha Kwa Wingi kwenye black market?

Waache ujinga walete sheria ya Kilimo rasmi Cha Bangi na Mirungi Ili Mashamba yawe monitored badala ya kuongea pumba hapa 😆😆.

---
Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Dkt. Peter Mfisi amesema Nchi zilizohalalisha bangi zina utaratibu thabiti ikiwemo kulima bangi hizo kwenye maeneo maalum na kuna kiwango kinachotakiwa ambapo amesema bangi ya Tanzania inayolimwa kwenye mashamba yasiyo rasmi kiholela haifai na haiwezi kukubalika kwenye masoko halali ya nje ya Nchi.

Amesema hayo leo Jijini Dar es salaam baada ya Mwandishi wa @AyoTV_ kumuuliza mtazamo wake kuhusu maoni ya Watu wakiwemo Wabunge kwamba bangi ianze kuuzwa nje ya Nchi ili iongeze pato la Taifa badala ya kuwa inateketezwa.

“Nchi zilizohalalisha bangi wana bangi yao inalimwa kwenye green house inatakiwa iwe na kiwango fulani, tusichukulie tu jambo la rahisi tu kwamba tutachukua tuweke kwenye kiroba kwenda kuwauzuia nje mfano Kenya, Kenya wenyewe bangi haijahalalishwa”

“Hii bangi yetu haifai kwenye kwenye masoko halali hata huko nje, kule wenzetu wametengeneza sehemu maalum za kuuza, kiwango cha kununua na hata umri wa Mtu wa kumuuzia, ukisema uruhusu ya kwetu haiwezi kukubalika, mfano halisi ni miwa, hivi miwa yote inaruhusiwa kutengenezea sukari?, jibu ni hapana, na bangi pia ipo hivyo sio kila bangi inafaa kwa matumizi halali”

Chanzo: Millard Ayo

View: https://twitter.com/millardayo/status/1724390560096473579?t=ht--BdSQpf35r48oE2jlRw&s=19
 
Najiuliza, watu wenye maadili, fikra na maarifa kama haya wanatoka wapi?

Sasa ndio naanza kuamini majina uliyopewa utotoni na hatma ya maisha yako. Yaani fikra zako, matendo yako na hulka zako huwa siku zote zinaendana na Jina lako.
Mfano Rehema, akiitwa Rehema, basi anakuwa wa Rehema rehema, Vivyohivyo, ninaposikia jina Peter, ninafikiria inspiration zake kwenye biblia. Walakin, jina lake la pili, Ati MFISI, mimi nasikia MFILISI.

Kwa matamshi yake hayo, naona ni Mfilisi tu wa Fikra na maarifa chanya. Itoshe, wapo walima bangi Arusha wenye kulima bangi zenye viwango vya kimatifa. Sobai! Asituchanganye.

Hizo fikra zake ni fikra potofu tu, hazina uhalisia.
 
....niongeze tu, wao ukiwauliza wanapata wapi kanuni na weledi wao kwenda kuwakamata walima na wavuta bangi watakuambia wanatumia uweledi wa Kimataifa, mbinu na maarifa za Kimatifa....kwa kutumia hela za Kimataifa!

Sasa unamkamataje mlima bangi na mvuta bangi isiyokuwa na sifa za Kimataifa kwa kanuni za Kimataifa? Si ni kutiana umasikini tu.

Sijui alivuta nini!
 
Wameanza kulegea, sasa ni 50/50 amekiri iko bangi nzuri huko nje ila ya kwetu ndio mbaya, basi sawa tuagize nje mbegu ya hiyo bangi nzuri kisha tulime kwenye greenhouse anazotaka kisha tuvute.

Bangi oyeee!
 
Mnaanza kutekwa kiakili taratibu ooh inayolimwa holela haifai
Nani kasema wananunua bangi ya majani hajui mbegu zinakamuliwa?

Naona wanataka kuhalalisha ila vibali watapewa matajiri wakubwa wafaidi wote

Halafu kumbe hata lile shamba Magu alimpa yule mzee tajiri alimie miwa kwa sukari kwa hiyo haifai pia au mimi ndio nilikuwa naota
 
Si ni harambee kulima bangi Tanzania, hiyo waliyoipima ubora imelimwa na nani? Au walichukua hizihizi wanazokamata wakaenda kupima? Au serikali ina mashamba yake?
 
Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Dkt. Peter Mfisi amesema Nchi zilizohalalisha bangi zina utaratibu thabiti ikiwemo kulima bangi hizo kwenye maeneo maalum na kuna kiwango kinachotakiwa ambapo amesema bangi ya Tanzania inayolimwa kwenye mashamba yasiyo rasmi kiholela haifai na haiwezi kukubalika kwenye masoko halali ya nje ya Nchi.
Alijaribu lini?
Hiyo aliyojaribia alilima wapi?
Alililma kwa kusudi gani?
Na kama ingefaa alifikiria kufanya nini nayo?
 
Amejuaje ubora ?

kwanza kabisa akiri kwamba kashawahi kujaribu kuivuta ila kwa kukosa elimu ya matumizi sahihi ya hui mmea huenda alivuta zile chenga zinazobakia chini kabisa kwenye ndoo mzigo ukiisha.
Wapumbav sana ,hawajui jinsi nchi zinavyoelekeza kwenye hilo zao
Bangi ina matumizi mengi sana ,kuanzia kama malighafi katika uzalishaji wa dawa , kutumika kama stimulant ,kutumika kama malighafi ya kuzalisha fibers Kwa ajili ya uzalishaji wa nguo ,kutumika kama malighafi ya kuzalisha mafuta ya kuendesha mitambo (biodiesel) nk
 
Swali.

Hivi wenzangu mnamuelewa huyu Jamaa?

Yaani bangi ingekuwa haifai watu wangekuwa wanalima na kuisha Kwa Wingi kwenye black market?

Waache ujinga walete sheria ya Kilimo rasmi Cha Bangi na Mirungi Ili Mashamba yawe monitored badala ya kuongea pumba hapa [emoji38][emoji38].

---
Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Dkt. Peter Mfisi amesema Nchi zilizohalalisha bangi zina utaratibu thabiti ikiwemo kulima bangi hizo kwenye maeneo maalum na kuna kiwango kinachotakiwa ambapo amesema bangi ya Tanzania inayolimwa kwenye mashamba yasiyo rasmi kiholela haifai na haiwezi kukubalika kwenye masoko halali ya nje ya Nchi.

Amesema hayo leo Jijini Dar es salaam baada ya Mwandishi wa @AyoTV_ kumuuliza mtazamo wake kuhusu maoni ya Watu wakiwemo Wabunge kwamba bangi ianze kuuzwa nje ya Nchi ili iongeze pato la Taifa badala ya kuwa inateketezwa.

“Nchi zilizohalalisha bangi wana bangi yao inalimwa kwenye green house inatakiwa iwe na kiwango fulani, tusichukulie tu jambo la rahisi tu kwamba tutachukua tuweke kwenye kiroba kwenda kuwauzuia nje mfano Kenya, Kenya wenyewe bangi haijahalalishwa”

“Hii bangi yetu haifai kwenye kwenye masoko halali hata huko nje, kule wenzetu wametengeneza sehemu maalum za kuuza, kiwango cha kununua na hata umri wa Mtu wa kumuuzia, ukisema uruhusu ya kwetu haiwezi kukubalika, mfano halisi ni miwa, hivi miwa yote inaruhusiwa kutengenezea sukari?, jibu ni hapana, na bangi pia ipo hivyo sio kila bangi inafaa kwa matumizi halali”

Chanzo: Millard Ayo
Huyo mpuuzi anayesema bangi ya Tanzania haina ubora yeye anajua mmea wa bangi wa Tanzania ni wa aina gani ?na unafaa katika shughuli gani mpaka. Aseme hauna ubora ?
 
Amejuaje ubora ?

kwanza kabisa akiri kwamba kashawahi kujaribu kuivuta ila kwa kukosa elimu ya matumizi sahihi ya hui mmea huenda alivuta zile chenga zinazobakia chini kabisa kwenye ndoo mzigo ukiisha.
Kamishna alivuta vumbi la bangi,,na sio bangi yenyewe arudi akafanye uchunguzi tena naamini atarudi na majibu tofauti kabisaa!!
 
Bhangi ya Tanzania ni Bush weed, ina THC ndogo kama serengeti light wakati ya greenhouse ni kama Jack Daniels.
Hiyo bush weed bado ina matumizi pia ,kama nilivyoeleza hapo juu ,inaweza tumika katika mojawapo ya matumizi niliyooridhesha hapo juu
 
Back
Top Bottom