Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Wakuu,
Ni mara chache sana kusikia mtu mwenye cheo huko Polisi ku-advocate masuala ya haki za binadamu na utawala bora
Tunaelekea pazuri?
==========
Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Kombo Khamis Kombo, ametoa wito kwa askari polisi kufanya kazi kwa kuzingatia haki za binadamu.
CP Kombo ametoa ujumbe huo wakati akifunga Mafunzo ya Uongozi Mdogo kwa askari Polisi wa vyeo vya Sajini Meja (SM), Sajini Staff (SSGT) na Sajini (SGT) yaliyofanyika Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu, mkoani Morogoro, tarehe 27 Februari, 2026.
Katika hafla hiyo, Kamishna Kombo alikagua gwaride la wahitimu, kisha kutoa zawadi kwa askari waliofanya vizuri zaidi katika mafunzo hayo, pamoja na kushuhudia maonesho mbalimbali yaliyoandaliwa na pia aliwasisitiza wahitimu kufanya kazi kwa kuzingatia pia utawala bora na kuepuka vitendo vya rushwa, wakati wa majukumu yao ya kazi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dustan Kyoba, amewashauri askari kuzingatia misingi minne ya Jeshi la Polisi, ambayo ni nidhamu, haki, weledi na uadilifu.
Mapema akitoa taarifa ya mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo cha Polisi Kidatu, SACP Zarau Mpangule, amesema jumla ya wahiitimu wote ni 758 ambapo wanawake 124 na wanaume 634 wamepata mafunzo kwa muda wa miezi mitatu, wakifundishwa masomo ya sheria, uongozi, Polisi jamii, huduma bora kwa mteja na medani za kivita.