Kampala International University (KIU) chafungiwa na TCU

Tangopori

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Posts
1,628
Reaction score
1,285
Chuo kikuu cha Kampala tawi la Tanzania (KIU) kimefungiwa na TCU kutoa mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kwa kutokuwa na sifa stahiki za wahadhiri wa kutoa mafunzo hayo.

TUESDAY, MAY 07, 2013
CHUO CHA KIU-DCC KUSIMAMISHWA KUTOA MAFUNZO YA SHAHADA ZA UZAMILI NA UZAMIVU

Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam (KIU-DCC) kilichopo Gongo la Mboto, Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Kufuatia kuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili, Tume katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam ifuatayo;

1. KIU isimamishe mara moja mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya Dar-es-Salaam.

2. KIU ishirikiane na wanafunzi wote iliyowadahili katika programu zilizotajwa hapo juu waweze kuhamia kwenye vyuo vingine vyenye idhibati ya kutoa mafunzo hayo.

Tume haitatambua shahada yeyote ya Uzamiili au Uzamivu itakayotolewa na chuo hicho kwa watakaosoma katika kampasi ya Dar-es-Salaam. Angalizo:

Chuo cha KIU Kampasi ya Dar-es-Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa mafunzo ya shahada ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti zilizopitishwa na TCU kwa mujibu wa Ithibati husika tuu.

Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
kama mnakumbuka kuna kipindi uliletwa mtihani wa hiki chuo hapa JF wa somo la computer ambao ulikuwa unasikitisha kweli ulikuwa kule jamii photos

probably TCU walianzia hapa Jf na kuamua kufuatilia!
 
....bora wakifungie...na sitashangaa share holders wenye kumiliki hiki chuo ni vigogo serikalini....Hivi ndio vyuo vilivyoanzishwa kama uyoga ili kubeba ma feki yanayotokana na shule zetu....Chuo kinawezaje kutoa masters/PhD kwa kuwa na waalimu wenye masters tu??..au PhD za kuunga??.....The quality of university education can also be measured by the quality of university itself...but this fact seems to be taken differently by some universities in TZ....this one being among....
 
dah hiki chuo ni balaa.. nilijoin pale for MBA mwaka 2010 nilioanza kusoma mh nilipagawa maana eti lecturers waliokuwa wanatufundisha first year wengine walikuwa wanasoma 2nd year..dah nilitimka nikajikuta nimepoteza almost USD 1200.. bora wakifungie tu maana bado sanaa ..
 
nilipikua nasoma pale mba waliokua wanatufundisha wengi ndo walikuwa wanasoma masters second year...nilitimuaje mbiooooo...
 
We endelea kuwadanganya wasiojua tu.MBA ya miaka miwili? Mtaala wa china au urusi huo.
 
dah hiki chuo ni balaa.. nilijoin pale for MBA mwaka 2010 nilioanza kusoma mh nilipagawa maana eti lecturers waliokuwa wanatufundisha first year wengine walikuwa wanasoma 2nd year..dah nilitimka nikajikuta nimepoteza almost USD 1200.. bora wakifungie tu maana bado sanaa ..

Hahahahaaah! mbavu zangu. duuh!!
 
nilipikua nasoma pale mba waliokua wanatufundisha wengi ndo walikuwa wanasoma masters second year...nilitimuaje mbiooooo...
..hilo wala sishangai...infact hata ukienda kwenye baadhi ya vyuo (matawi ya vyuo)...kama saut (kule Mtwara mfano)utakuta ma lecturers wenye masters(wengine bado wanasoma)....Tumeng'ang'ania kushughulikia ubora wa elimu TZ kwenye level ya secondary school....lakini tumesahau huko kwenye vyuo vikuu vilivyoanzishwa kama uyoga nako kuna bomu linalosubiri kulipuka......Mfano...huwezi sasa hivi kumfananisha daktari wa binadamu aliyetoka IMTU...ukamlinganisha na aliyetoka Bugando au MUCHS au KCMC....Nimewahi kukutana na daktari graduate wa IMTU hajui hata kuandika history ya mgonjwa....alafu eti wanakiita International University....wamekua hata wakati fulani wanawatoza wanafunzi ada kwa dola...na haya yalikua yanafanyika na serikali ipo inaona.....Inasikitisha sana.....Nimewahi kukutana na mwalimu...eti lecturer pale duce....loh!!yaani mwalimu hata kuongea kwa kupanga logic hawezi....matokeo yake tunawaona ma graduate wengine wa ajabu ajabu mitaani......wanahangaika kutafta ajira hawapati.....wengi unakuta uwezo wala hawana....Haya yote ni matokeo ya hivi vyuo uyoga....vilivyoanzishwa kwa kasi ya ajabu kama shule za kata.....Tujipe miaka 10 kuanzia sasa...tutakua tunalia kuhusu aina za graduates wa vyuo vyetu.....kama tunavyolia sasa kuhusu watoto kufeli.....Hawa wanaofanyiwa standardization (wakati wamefeli)unategemeaje???
 
kwakweli this government inabidi i take masuala ya elimu seriously..huko tunapokwenda hata sijui watoto wetu watakuja kuwa na maisha gani kwa mfumo huu wa elimu..

nobody cares kila mwenye nafasi anaangalia atafaidika vipi yy kama yy kupitia nafasi aliyonayo.. mh so sad..
 
Mm nmesoma kiu ila nmeona kile chuo kwa diploma na certificate kinafaa sana.
 
Back
Top Bottom