Tangopori
JF-Expert Member
- May 11, 2012
- 1,628
- 1,285
Chuo kikuu cha Kampala tawi la Tanzania (KIU) kimefungiwa na TCU kutoa mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kwa kutokuwa na sifa stahiki za wahadhiri wa kutoa mafunzo hayo.
TUESDAY, MAY 07, 2013
probably TCU walianzia hapa Jf na kuamua kufuatilia!
TUESDAY, MAY 07, 2013
kama mnakumbuka kuna kipindi uliletwa mtihani wa hiki chuo hapa JF wa somo la computer ambao ulikuwa unasikitisha kweli ulikuwa kule jamii photosCHUO CHA KIU-DCC KUSIMAMISHWA KUTOA MAFUNZO YA SHAHADA ZA UZAMILI NA UZAMIVU
Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam (KIU-DCC) kilichopo Gongo la Mboto, Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Kufuatia kuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili, Tume katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam ifuatayo;
1. KIU isimamishe mara moja mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya Dar-es-Salaam.
2. KIU ishirikiane na wanafunzi wote iliyowadahili katika programu zilizotajwa hapo juu waweze kuhamia kwenye vyuo vingine vyenye idhibati ya kutoa mafunzo hayo.
Tume haitatambua shahada yeyote ya Uzamiili au Uzamivu itakayotolewa na chuo hicho kwa watakaosoma katika kampasi ya Dar-es-Salaam. Angalizo:
Chuo cha KIU Kampasi ya Dar-es-Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa mafunzo ya shahada ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti zilizopitishwa na TCU kwa mujibu wa Ithibati husika tuu.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
probably TCU walianzia hapa Jf na kuamua kufuatilia!