Kampala: Leo kati ya Vijana kumi, sita wamelegea. Vijana wetu tumewaacha

Kampala: Leo kati ya Vijana kumi, sita wamelegea. Vijana wetu tumewaacha

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079

​
Mbunge wa Katavi, Thomas Maganga Kampala, wakati akichangia hoja bungeni jana Oktoba 30, 2026, amesisitiza kuwa ili nchi iweze kutekeleza mipango yake ya maendeleo kwa mafanikio, inapaswa kuwekeza kwa dhati na kulinda nguvu kazi ya vijana ambao ndio asilimia 70 ya wananchi wote wa Tanzania.

Katika mchango wake huo, Mbunge Kampala ameeleza kusikitishwa na wimbi la mmomonyoko wa maadili na changamoto zinazowakumba vijana wengi mitaani, akionya kuwa bila kuwa na mkakati thabiti wa kuwalinda na kuwaweka katika mazingira mazuri, taifa linaweza kukosa mwelekeo thabiti katika miaka ijayo.

Aidha, amegusia suala la vitendo vya kikatili vya ulawiti na ubakaji vinavyowakumba watoto na vijana, akitoa wazo la kuwepo kwa sheria kali ya kuwahasi wahusika ili kukomesha vitendo hivyo viovu ambavyo vinazidi kulitia taifa katika mkanganyiko.
 
Kwanza huyu naye ni mpuuzi.
Angekuwa serious angeanza na walio ua ndugu zetu kipindi wao wanagombania kuingia bungeni.

Hao wabunge walifaa wachomwe moto wote na majivu yao yakamwagwe baharini
 
Kwanza huyu naye ni mpuuzi.
Angekuwa serious angeanza na walio ua ndugu zetu kipindi wao wanagombania kuingia bungeni.

Hao wabunge walifaa wachomwe moto wote na majivu yao yakamwagwe baharini
Hakuna serikali inayopenda kuua raia wake. Mtu anapoteuliwa kuwa CDF au IGP, huyo ni Mzalendo kweli kweli. Kulikuwa na tishio la usalama wa nchi/taifa ndio maana kikatokea kile kilichotokea ndugu yangu.

I'm sincerely sorry for the collateral damages caused by the crackdown on coup plotters and executors.
 
Mkuu umeona kilichotokea huko ulaya? Wameua waandamanaji? Au october ndiyo ilikuwa mara ya kwanza watanzania kuandamana?
Unataka kusema kama kulikuwa na tishio la usalama hivyo vyombo vya usalama vinalipwa kodi zetu za nini iwapo walishindwa kulizuia mapema? Intelejensia ilikuwa wapi?
Unahalalisha kuua kama njia pekee? Kulikosekana njia nyingine?

Kama msomi unajenga hoja yako hivyo nakuwana wasiwasi na Elimu yako haijakusaidia.

Msingi wa kwanza wa kiongozi ni kulinda Watu wake maana Taifa ni watu siyo mali au vitu.

Kulikuwa na njia nyingi sana kuwashugulikia watu kuliko kuwaua!

hata mwovu anahaki ya kuishi maana kila mtu anakose! Hukumu ya kifo ni ya mola pekee.

NB. Usirudie kutetea hoja ya kishenzi na kipuuzi kama hiyo. Au we ndo wahusika?
 
Back
Top Bottom