Kampeni chafu zaanza UVCCM

Mkuu nimeamini ikiwa na mihela uwe karibu na viongozi na kutoa toa viposho hata kama 5000 kwa kila mjumbe basi utalindwa balaa.Hata ukitaka kugombea ujumbe wa NEC hutumii nguvu nyingi kama wengine.

Sumaye wakati fulani aliwahi kuwaambia wananchi sehemu fulani kuwa "ukitaka kufanikiwa kwa lolote fanya biashara na CCM", Hata kuuza mirungi, gongo etc!
 
Huyo ametoa pesa kwa niaba ya akina Jeetu Patel ili mambo yao yasiende vibaya mahakamani. Rushwa hiyo jamani. Jamani hicho ni Chama Cha Matajiri (CCM) , msishangae.
 
Kwa wasiomjua TANIL ndio huyu, katika KULIKONI na THISDAY, tutafakari hatima ya CCM kuelekea 2010.


Source: KULIKONI Na.484, Jumatatu Novemba 10, 2008
SOURCE: Thisday No. 814, Monday 10, November, 2008

ThisDay

Picha inayoonekana imepigwa na Mpiga Picha wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Amour Nassor.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SHIVACOM GROUP iliyodhamini utengenezajia wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa umoja wa vijana wa CCM ndugu TANIL SOMAIYA, akimkabidhi baazi ya vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 400 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete Makamo Makuu ya CCM Dodoma.
 

Attachments

  • Tanil.jpg
    169 KB · Views: 188
400m. Halafu huyu mtathubutu kumwambia kitu? Mtu akikufadhili kwa kiwango hiki unakuwa huna ubavu wa kusema chochote, hata akisema chochote lazima ukenue meno hata kama inakuuma vipi! haya na tuone. Kina Fisadi Shah wengine hao!

Kwani Jeetu alichanga kiasi gani wakati wa kampeni za CCM/JK 2005? Sasa hivi yuko wapi? JK ni zaidi ya tunavyomfahamu!
 
Kinachofurahisha ni Mzee Pius kuchekelea na Nchimbi kukaba Penati,hachezi mbali na za hivi
 
Nimeipenda hiyo Picha,

Pale kuna moja viongozi wakubwa wote wa chama na serikali hii mpya na ya zamani

1.Rostam
2.kigoda
3.mama meghji
4.Msekwa
5.Waziri kiongozi
..............................

Jamiiforums lini tuakwachangie CHADEMA au CCM?
 
Sasa tukisema kwamba CCM maanake ni chama cha mafisadi si tunakuwa tumesema kweli tupu?, Tena fisadi anajigamba kwa nguvu zote kwamba ni ukereketwa ndo....

Yaani mtakumbatiaje pesa za mafisadi kama nyie si mafisadi? Tena mna washadadia eti wanajitangaza?

ILA YANA MWISHO HAYA, TENA MWISHO WAKE U KARIBU SANA!
 




Naona vigogo wote wamejazana na mkuu mwenyewe anapokea furushi!Halafu akijulikana amechota mahali mkuu ataunda tume ya mwaka mzima kumchunguza!!!!!
 
Huyu anatafuta nini kufutiwa kodi?
Tulisha ambiwa hawalipi kodi hawa jamaa ndo kulipa fadhira nini?
Ameacha kuchangia maendeleo huko vijijini kwa kutoa madawati yeye anafadhili ufisadi.
Anajitengenezea jina..

Hili jina ni kama la yule Mfanyabiashara wa Goldberg scandal kule Kenya ambaye amefungwa au ni yeye?

Achangie maendeleo ili iweje? Salama yake ni CCM kuendelea kutawala vinginevyo ni ???
 
Kweli hawa wahindi wamewashika pabaya viongozi wetu wa chama.
Ukitaka usibughudhiwe katika biashara yako njia pekee ni kujikomba komba kwa akina Makamba kama hivi utaona hata siku moja TRA hawaji kukubughi unakuwa mtu wao.
Hata wale wenye malori au mabus ya wafadhili wa CCM hayapigwi pigwi mkono barabarani Trafic akisimamisha labda kama haitaki kazi yake.
 
Hili jina ni kama la yule Mfanyabiashara wa Goldberg scandal kule Kenya ambaye amefungwa au ni yeye?

Achangie maendeleo ili iweje? Salama yake ni CCM kuendelea kutawala vinginevyo ni ???

Mkuu hii inathibitisha ule usemi usemao.
"Nimewaweka mfukoni au kiganjani viongozi wote wa nchi hii"
Utasikia nenda kashitaki popote pale......ukienda kushitaki utatendewa haki kweli? kama mnavyo ona jamaa wamepokea fuko la mihela hiyo huku wakicheka teh! teh! teh!..
Hivi mababu zetu wa enzi hizo walio kuwa wakiuza ardhi kwa kioo au chuba ya mvinyo na hawa viongozi wetu wanatofauti gani??????
 
Lakini Tajiri Soros mbona amewahi kutumia dola millioni 20 kusaidia Democrats huko USA, hasa kwenye uchaguzi dhidi ya Bush kwenye term ya pili?

Hapa sidhani kama tatizo ni kutolewa kwa hela, au kwa CCM kupokea hizo hela, labda tatizo ni mtoaji anataka nini au amewahi kutaka nini au amewahi kupewa nini na watawala wetu, kama yanafahamika yawekwe wazi hapa otherwise tusiwakatishe tamaa wananchi wenye nia ya kutoa misaada kusaidia vyama vyetu vya siasa.

Kutoa misaada kwa vyama vyetu vya siasa sio kuvunja sheria ya jamhuri yetu, au?
 

Ni kweli si kuvunja sheria, lakini kuna sheria yoyote inayo-guide michango/zawadi za wafanyabiashara, raia wengine wa Tanzania au wasio raia kwa vyama? CCM wanajua 'status quo' iliyopo inawa-favour wao kupokea michango na fedha kutoka kwa wafanyabiashra, raia na wasio raia ili waendelee kuwa madarakani. Kikwete alizungumzia muda mrefu kupeleka muswaada bungeni ili itungwe sheria ya kufuatilia hii michango na zawadi kwa vyama vya siasa lakini mpaka sasa ni kimya. Kwa maoni yangu suala hili ni mojawapo linalofanya uwanja wa siasa Tanzania usiwe 'fair ground to all players'
 

Tanzania hatuna sheria inayo-guide misaada ya wananchi kwa vyama vyetu vya siasa, sasa sina uhakika kama ni vyema kuanza kushambulia CCM au chama chochote cha siasa nchini kikipokea msaada, maana ninajua kuna wakati Mrema, alipokea msaada flani wa kusaidia umeme kutoka nje mpaka leo sielewi aliishia wapi, na vyama vyetu vingi vya siasa vimekua vikipata misaada toka nje na ndani, ingawa sio wakati wote hizo habari husemwa to the public kama CCM,

Sasa ninafahamu kuwa ni kawaida ya siasa kwamba the incumbent hupata misaada mingi zaidi kuliko the challenger, unless you are Obama, sasa in the absence of sheria ya kuzuia wananchi kusaidia vyama vyetu vya siasa, tunalaumu huu msaada kwa mantiki ipi hasa?
 
This is an embarrasment kwa kweli.CCM inaongozwa na genge la wahuni maana huu ni uhuni wa kupindukia.Yaani mtu anachangia CCM 400M leo tukisikia kafanya ufisadi kweli atakamatwa huyu?
 

Mantiki ya mchango wangu si kulaumu msaada, bali kuelezea unfairness ya uwanja wa kisiasa ulivyo na kwa CCM wakijua hilo hawajataka kuweka fair ground. Pili tunajua kutokana na maelezo ya viongozi waliopita CCM/serikalini kuwa ili mfanyabiashara mambo yako yakuendee vizuri inabidi uwapigie magoti hawa waheshimiwa wa CCM ....kama tunayoona kwenye hili na hiyo statement haijawahi kukanushwa na yoyote ndani ya CCM. Mind you also CCM ndio wanaouchukua ruzuku kubwa kuliko vyama vyote, wana wanachama wengi kuliko vyama vyote, wana vitega uchumu lukuki nchi nzima na bado kuandaa mikutano yao inabidi kuwaabudia wafanyabiashara. This says alot of the party itself na watu wanaokiongoza na kwa nini Tanzania ipo hapa ilipo.
 
This is an embarrasment kwa kweli.CCM inaongozwa na genge la wahuni maana huu ni uhuni wa kupindukia.Yaani mtu anachangia CCM 400M leo tukisikia kafanya ufisadi kweli atakamatwa huyu?

Kumbe so far hatujasikia? Mimi nilifikiri tumesikia tayari, au?
 

Mkuu unless kuna zaidi ya haya ya kuhisi na kusikia, hata siku moja hakujawahi kuwa na fairness kwenye siasa za dunia between the incumbent na the challenger, nafikiri hiyo ni kwa siasa za dunia nzima inapokuja kwenye uchaguzi,

Sasa unasema kwamba biashara za Mwenyekiti wa sasa wa
Chadema zinanyooka wka sababu anawapigia magoti viongozi wa CCM, au? Mbunge wa Chadema Ndesamburo, naye anawapigia magoti CCM au?

I mean kwa maneno ya kusikia na kuhisi, yes kuna hoja ya kulaumu huu msaada, lakini kwa mjadala wa kisomi na kutraka kuisaidia jamii yetu ninashindwa kuona hoja ya msingi against hii misaada kwa vyma vyetu vya siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…