Kampeni dhidi ya Mkapa asishinde Tuzo ya uongozi bora

Kampeni dhidi ya Mkapa asishinde Tuzo ya uongozi bora

Wala hamtafanikiwa maana dua zenu ni za kuku haliwezi kumpata kunguru!

BWM amefanya mengi sana hapa bongo, amerekebisha uchumi, ameacha ma fedha kibao hazina sijui mnataka nini hasa!

Yaani wewe naona hujui hata unachoandika! Hivi Watanzania wana sababu gani ya kumchukia Mkapa kiasi hicho!? Mbona Mwalimua aliyeng'atuka tangu 1985 miaka 22 iliyopita mpaka leo ni kipenzi kikubwa cha Watanzania walio wengi. Watanzania sio wapumbavu, Mkapa ndio aliongeza kwa kiasi kikubwa makusanyo ya kodi lakini Watanzania hawakunufaika na lolote kutokana na makusanyo hayo.

Ni kama baba anayetamba mtaani kwamba yeye ndio mwenye mshahara mkubwa pale mtaani, lakini pesa zake zote zinaishia nyumba ndogo, nyama choma na moja moto moja baridi na watoto wake wamedhoofu kwa kukosa lishe bora. Kuna ushahidi wa kutosha unaonyesha kwamba hakuwa Mr Clean kama alivyotaka Watanzania waamini.
 
Sitashangaa sana kama Mkapa ndiyo atanyakua tuzo hiyo, wakiangalia makaratasi Tanzania ilifanya vizuri chini ya uongozi wake, na zaidi ya yote kati ya wote waliomo kwenye hiyo orodha ni yeye peke yake amejijenga katika majukwaa ya kimataifa. So, ingawa sipendi apewe tuzo hiyo kwa sababu amewadharau watu waliompa nafasi hiyo kuangaza na ametumia madaraka yake vibaya.. ukweli ni kuwa atashinda tuzo hiyo na kutunyanyulia kidole cha kati!!

Thubutu.....Akifanya hivyo, nami nitanyanyua 'viwili vya kati' kumjibu na ikiwezekana 'dole gumba la mguuni'!!

SteveD.
 
Yaani wewe naona hujui hata unachoandika! Hivi Watanzania wana sababu gani ya kumchukia Mkapa kiasi hicho!? Mbona Mwalimua aliyeg'atuka tanngu 1985 miaka 22 iliyopita mpaka leo ni kipenzi kikubwa cha Watanzania walio wengi. Watanzania sio wapumbavu, Mkapa ndio aliongeza kwa kiasi kikubwa makusanyo ya kodi lakini Watanzania hawakunufaika na llolote kutokana na makusanyo hayo.

Ni kama baba anayetamba mtaani kwamba yeye ndio mwenye mshahara mkubwa pale mtaani, lakini pesa zake zote zinaishia nyumba ndogo, nyama choma na moja moto moja baridi na watoto wake wamedhoofu kwa kukosa lishe bora. Kuna ushahidi wa kutosha unaonyesha kwamba hakuwa Mr Clean kama alivyotaka Watanzania waamini.

Bubu, nisingependa iwe hivyo, ila inawezekana kabisa huo ndiyo ukawa 'upande wa pili' wa shilingi ya FD. Kutetea bila sababu yenye msingi wala vigezo vinavyoridhisha.

SteveD.
 
Binafsi, nikiangalia aliyoyafanya Mkapa na kiwango cha wizi wake nafikiri kwamba, kwa standard za Africa bado ana nafasi na pengine anastahili kupata hiyo zawadi kuliko viongozi wengine wa Africa. Yes, hili li jamaa lliiba kwelikweli na lilijaribu sana kuua demokrasia ya vyama vingi kwa kuhakikisha linatumia kila njia kuviua vyama vya upinzani, lakini bado kwa kiwango cha Afrika yetu lilifanya vizuri kuliko viongozi wengi wa bara hili. Halafu ulimlinganisha na huyu mtalii wetu wa sasa hivi ndio kabisa lijamaa linakuwa kwenye chati. In fact hata huyu Joachim Chisano hawezi kumfikia Mkapa. kwa wale ambao wamepata nafasi ya kwenda Msumbiji utashangaa jinsi wanaharakati wa huko wanavyomlalamika Chisano katika kukandamiza demokrasia na kuporomosha majumba ya kifahari.

Ajabu sana kwa viongozi wetu wa Afrika; sijui inakuwaje wananchi wao wanawasuta lakini wakati huohuo wanasifiwa sana nje ya nchi zao.

Kwa hiyo binafsi sina kinyongo kama hili jamaa litaibuka na hii zawadi. Sema tu hawa wanamtandao watajaribu sana kutumia hiyo zawadi kujibu credit na kuiponya CCM na makombora inayasukumiziwa sasa hivi kama kawaida yao. Na msisahau ile kuwa mjumbe wa Africa Commission ya Tony Blair kuliongeza chati ya Mkapa sana na kwenye report yao ya mwisho amesifiuwa sana tu!
 
...pamoja na mabaya yaliyojitokeza dakika za majeruhi lakini tusisahau mazuri yake. Yeye ndiye aliyerejesha heshima ya hela, heshima ya civil servants, accountability, proper taxation, taming of inflation, etc

Mabaya yake ni mangapi?
- ANBEM - Ethics conflict.
- Kiwira - Opportunistic last minute approach.
- etc?

Labda tuweke mazuri yake upande mmoja na mabaya yake upande wa pili na tuangalie kama tumtreat on extreme au midway. Binadamu kwa kawaida hukumbuka mabaya tu...tuangalie the other side of the coin basi.

Je tukijumlisha mabaya kama -ve na mazuri kama +ve atabakia kwenye -ve au +ve OR yatacancel each other abakie kuwa amefanya 0?
 
Insurgent, I like the way you present your arguments, ingenious!

Yata cancel na kubakia kwenye anga za -ve! kwa sababu ya kutojibu au kutoomba msamaha. Kanikatisha tamaa mimi kwani naamini ni mkristo na muumini mzuri tu wa dini yake. Angekubali kujieleza au pia kuomba msamaha kama 'ucha Mungu' unavyo hitaji, miye ninge msamehe na kumuunga mkono apokee tuzo. Tatizo anazidi kuchelewa na kukomaa zaidi katika ubishi!

SteveD.
 
"Tuzo HAITAKUA NA MAANA KABISA KAMA MKAPA ATAPEWA" ........
 
Mi nadhani nianze na Mo Ibrahim, as a Businessman, yeye ni NANI hadi apate nafasi ya 'kuwapanga mstari' viongozi wa Afrika katika misingi sijui ya demokrasia na nini?

I mean, huyo mfanyabiashara binafsi ni msafi kiasi gani hadi athubutu kutoa hiyo tuzo? maana mimi sioni kingine zaidi ya ubeberu tu hapa, asiwadanganye mtu, siasa zinatofautiana, from one place to another, and what democracy means, pia ni tofauti,

Na je, kwa nini zikatolewa London na sio makao makuu ya AU kwa mfano? hizo bilioni tano si angeanzia kwao Darfur ambako watu wanateseka, huena zingewasaidia hata maji ya kunywa, kuliko kumpa mtu mmoja ambaye tayari yuko better off? Raisi gani kastaafu masikini ukiacha wale wa enzi ya Nyerere?
Mi naona hapo kuna ubeberu wa kifikra tu, 'wakubwa' wanaendelea kutufundiha nini maana ya demokrasia, huku wao wenyewe utekelezaji wao wa demokrasia ukitia shaka....
 
Sitashangaa sana kama Mkapa ndiyo atanyakua tuzo hiyo, wakiangalia makaratasi Tanzania ilifanya vizuri chini ya uongozi wake, na zaidi ya yote kati ya wote waliomo kwenye hiyo orodha ni yeye peke yake amejijenga katika majukwaa ya kimataifa. So, ingawa sipendi apewe tuzo hiyo kwa sababu amewadharau watu waliompa nafasi hiyo kuangaza na ametumia madaraka yake vibaya.. ukweli ni kuwa atashinda tuzo hiyo na kutunyanyulia kidole cha kati!!

apo mkuu umenena, ila ndo kama ivo huku nyumbani 'anamulikwa' kinoma, sasa sijui kama hii 'tochi' ya Butiku inaweza kumchoma?

kp_118.jpg

picha kwa hisani ya Kipanya, http://www.kipanya.co.tz/
 
Mi nadhani nianze na Mo Ibrahim, as a Businessman, yeye ni NANI hadi apate nafasi ya 'kuwapanga mstari' viongozi wa Afrika katika misingi sijui ya demokrasia na nini?

I mean, huyo mfanyabiashara binafsi ni msafi kiasi gani hadi athubutu kutoa hiyo tuzo? maana mimi sioni kingine zaidi ya ubeberu tu hapa, asiwadanganye mtu, siasa zinatofautiana, from one place to another, and what democracy means, pia ni tofauti,

Na je, kwa nini zikatolewa London na sio makao makuu ya AU kwa mfano? hizo bilioni tano si angeanzia kwao Darfur ambako watu wanateseka, huena zingewasaidia hata maji ya kunywa, kuliko kumpa mtu mmoja ambaye tayari yuko better off? Raisi gani kastaafu masikini ukiacha wale wa enzi ya Nyerere?
Mi naona hapo kuna ubeberu wa kifikra tu, 'wakubwa' wanaendelea kutufundiha nini maana ya demokrasia, huku wao wenyewe utekelezaji wao wa demokrasia ukitia shaka....

Kama unakubaliana nami kwamba wwith money you can do anything you want--So huyo MO anaweza kuchezea vichwa vya watu jinsi anavyotaka yeye. Kwanza MO akili yake ni bure kabisa--kwanini utoe pesa yote kwa Rais? kwanini asifanye ku-finance matatizo ambayo yanalikumba bara la Africa kama MAlaria na umasikini mwingine. Mfano mzuri ni bill gates-- kaweka chakula kwenye midomo.

Kwa hiyo mimi ambao mnamshambulia Mkapa badala ya kumshambulia MO mjinga wa kwanza nawashangaa. Huyu MO anaonekana akili ni bure hata kama ana pesa. Haya ni mambo ya ukoloni mamboleo kwamba anaweza kununua ma-rais wa Africa jinsi anavyotaka.
 
Nafikiri kabla ya ku-discuss nani apewe ni better kudiscuss kwa nini apewe na je hata kama akipewa Mkapa, watz na waaafrika kwa ujumla wanafaidika vipi na hii zawadi za kishenzi. I do support the argument of Nakulilia Tz kwamba--huyu MO ni msudani na kwao ndo kuna watu wengi wanakufa kwa njaa--kwanini asiwe na project ya food security yaani kuchangia kupunguza utapia mlo kwao lakini anaishia kupenda sifa za kijinga eti anazawadia ma-rais.

Nafikiri we need kupinga hii zawadi kwani mtoa zawadi akili haimtoshi sababu hajajikomboa mwenyewe na fikra zake ni za kitoto.
 
Kama unakubaliana nami kwamba wwith money you can do anything you want--So huyo MO anaweza kuchezea vichwa vya watu jinsi anavyotaka yeye. Kwanza MO akili yake ni bure kabisa--kwanini utoe pesa yote kwa Rais? kwanini asifanye ku-finance matatizo ambayo yanalikumba bara la Africa kama MAlaria na umasikini mwingine. Mfano mzuri ni bill gates-- kaweka chakula kwenye midomo.

Kwa hiyo mimi ambao mnamshambulia Mkapa badala ya kumshambulia MO mjinga wa kwanza nawashangaa. Huyu MO anaonekana akili ni bure hata kama ana pesa. Haya ni mambo ya ukoloni mamboleo kwamba anaweza kununua ma-rais wa Africa jinsi anavyotaka.

Yeah thats what I mean...tuanze na mantiki yenyewe kabla hatujamgusa kabisa 'mzee wetu' manake kijana wake kasema'tumwache apumzike', LOL
 
Haya Jamani,

Ninajua kuna mengi mazuri Mkapa ameifanyia Tanzania ila vitendo vyake na tabia zake za kipindi cha pili cha utawala wake vinatia aibu. Haya majibu yake ya dharau yanasononesha mioyo.

Mkapa, haufai kupewa tuzo ya uongozi bora Afrika. Umeitia aibu nchi yako na umemsaliti Nyerere aliyekuweka madarakani.

Tuache uchoyo na wivu wa kijinga. Mkapa akipata tuzo hiyo ni sifa kwa Tanzania pia. Na amefanya mengi mazuri kwa ajili ya nchi hii, wasioona hilo wana husuda na chuki binafsi. Hizi tabia za chuki binafsi na husda zinatuharibia hata kwenye mpira, ikija timu ngeni kucheza na Simba uwanja wa taifa, mashabiki wa Yanga wanakosa uzalendo kabisa, kisa tu hasimu wao asichukue ushindi. Ninyi msiotaka Mkapa ashinde tuzo hiyo mnakosa uzalendo kwa ajili ya kundi gani? Kwa hiyo akikosa hiyo tuzo ninyi mtafaidika? Ukisikia wivu wa kijinga na husda za dhahiri ndio hizi kabisa, hatuhitaji mfano mwingine!
 
Mheshimiwa Kithuku, kufichua uozo siyo kukosa uzalendo, uzalendo tulio onyesha miaka nenda rudi hauna maana tena kama ni wa 'kuficha uvundo ndani ya nyumba' zetu eti kwa sababu tu tunaishi humo... uvundo hubadilika kuwa uozo na uozo huleta madhara kiafya; madhara haya tuyaongeleayo ni maisha duni kwa wengine na abuse of office hali kile viongozi hawa wanacho preach kwenye majukwaa ya siasa na makongamano mengineyo ni 'uwajibikaji na transparency' only that they don't practice what they preach, don't you see that it is about high time we hit hard where it hurts?! well, unless it hurts you too....

SteveD.
 
Insurgent, I like the way you present your arguments, ingenious!

Yata cancel na kubakia kwenye anga za -ve! kwa sababu ya kutojibu au kutoomba msamaha. Kanikatisha tamaa mimi kwani naamini ni mkristo na muumini mzuri tu wa dini yake. Angekubali kujieleza au pia kuomba msamaha kama 'ucha Mungu' unavyo hitaji, miye ninge msamehe na kumuunga mkono apokee tuzo. Tatizo anazidi kuchelewa na kukomaa zaidi katika ubishi!

SteveD.

Aombe msamaha? Kwa kosa lipi? Kama kwa dhamira yake haoni kosa alilolifanya kwa nini aombe msamaha. Yeye anaona hana makosa. Anayedhani ana makosa apeleke hoja kwenye chombo kinachoweza kuthibitisha kama ana makosa au la. Hii habari ya kila mtu kujipachika uhakimu na kuanza kuhukumu watu ndio JK aliikataa hivi karibuni, na inavyoelekea, kuna wakati utafika hizi tuhuma zitazoeleka hadi zile za kweli zitaanza kuonekana pia ni za uongo, na zote zitapuuzwa. Watu wamekalia kuhukumu tu huyu fisadi huyu fisadi, this is ridiculous! Inanikumbusha hadithi niliyosoma nikiwa mtoto mdogo ya mtoto aliyekuwa anachunga mbuzi nyikani, alipoona upweke umemzidia, akaona afanye ujanja aite watu kwa namna ambayo lazima wangekuja tu. Akapiga kelele "wolf, wolf!", watu wakajazana pale kwa kuelewa mtoto anaomba msaada anakabiliwa na mbwa mwitu. Akaulizwa "mbwa mwitu yuko wapi?", akawa anajichekelesha tu, wakaondoka. Baada ya muda akapiga kelele tena, "wolf, wolf!" watu wakajaa tena kama mwanzo, lakini hakukuwa na mbwa mwitu. Wakajua sasa huu kumbe ndio mchezo wake. Baada ya muda kidogo akaja mbwa mwitu kweli, akaanza kumshambulia mtoto. Kapiga kelele weeeee, hakuna aliyekuja maana walishazoea huyu huwa anajipigia tu mikelele hovyo. Akararuliwa na mbwa mwitu.
Sasa nanyi ndugu zangu msije kutufanya turaruliwe na mbwa mwitu hivi hivi kwa sababu ya kutuzoesha kelele. Tupige kelele kukiwa na suala la kweli, na si tu kujaza watu kwenye forum. Maana tukiendelea hivi, baadae watu watazoea, hata tukiandika nini watasema, aah wamezoea hawa kujiandikia!

Licha ya mapungufu fulanifulani tena madogo aliyoonesha wakati wa uongozi wake, ninaamini Mkapa aliitumikia nchi hii kwa uadilifu wa kupigiwa mfano (hasa kama atalinganishwa na viongozi wengine wa Afrika), na anastahili kutuzwa si tu na huo mpango wa Mo Ibrahim, bali pia hata sisi watanzania tunapaswa kumuenzi. Yes, Mkapa for the prize.
 
Kisa cha joka la mdumuni, yeye hali ndimu lakini amekaa anazuia watu wasile ndimu! Ndio hawa wanaomsakama Mkapa....
 
Back
Top Bottom