BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Wala hamtafanikiwa maana dua zenu ni za kuku haliwezi kumpata kunguru!
BWM amefanya mengi sana hapa bongo, amerekebisha uchumi, ameacha ma fedha kibao hazina sijui mnataka nini hasa!
Yaani wewe naona hujui hata unachoandika! Hivi Watanzania wana sababu gani ya kumchukia Mkapa kiasi hicho!? Mbona Mwalimua aliyeng'atuka tangu 1985 miaka 22 iliyopita mpaka leo ni kipenzi kikubwa cha Watanzania walio wengi. Watanzania sio wapumbavu, Mkapa ndio aliongeza kwa kiasi kikubwa makusanyo ya kodi lakini Watanzania hawakunufaika na lolote kutokana na makusanyo hayo.
Ni kama baba anayetamba mtaani kwamba yeye ndio mwenye mshahara mkubwa pale mtaani, lakini pesa zake zote zinaishia nyumba ndogo, nyama choma na moja moto moja baridi na watoto wake wamedhoofu kwa kukosa lishe bora. Kuna ushahidi wa kutosha unaonyesha kwamba hakuwa Mr Clean kama alivyotaka Watanzania waamini.