Uchaguzi 2020 Kampeni Nzega: Dkt. Magufuli asema wanaomshangaa kununua ndege 11 wamepungukiwa

Uchaguzi 2020 Kampeni Nzega: Dkt. Magufuli asema wanaomshangaa kununua ndege 11 wamepungukiwa

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Leo kampeni zinaendelea na mwenyekiti na mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi, John Magufuli yupo Nzega mkoani Tabora akinadi sera na ahadi ya nini atafanya katika kipindi chake cha pili endapo atachaguliwa.

Kuwa nami kukujuza kitachojiri kutoka wilayani Nzega.
=======



7:50 Mchana: Wananchi wameshajaa na zinatoka salamu za utangulizi kutoka wilaya na mkoa.

Kigwangala: Umenipa heshma kuwa waziri wa kwanza kutoka wilaya ya Nzega tangu nchi ya uhuru tena ninaetokea katika familia dhalili kabisa ya Kinyonge. Watu wengi hukuzungumzia kama kiongozi mchapakazi, mambo magumu magumu umeyafanya, hawakuzungumzii soft part, umegusa maisha yangu. Umekuwa kiongozi mwenye huruma, mwenye kujali maisha ya watu wa chini.

Kwa kuwa tumeliamsha tutazunguka kukutafutia kuhakikisha unashinda kwa zaidi ya asilimia 95.

Bashe: Mheshimiwa Rais, sisi wananchi wa Nzega tulishafanya maamuzi na jana nilivyosikia kwamba unapita, tumepata taarifa jana saa saba tukasema lazima uwasalimie wananchi wote wa Nzega na hali leo ni wewe kupita kwa salamu tu, hakukua na maandalizi ya mkutano na nyomi ndio umeiona.

Sisi wananchi wa Nzega tumejipanga kuhakikisha tunakuchagua kwa zaidi ya asilimia 90 kwa sababu kuna mambo umetufanyia kwa kipindi cha miaka 5.

Polepole: Miaka miwili iliyopita alikwenda kwa ndugu zenu mkoa wa Manyara ambapo wanachimba madini ya Tanzanite ambako hayapatikani pengine kokote duniani. Kwa takwimu za mwaka 2015, Tanzanite iliyokuwa ikizalishwa ni kiloram 300 kwa mwaka mmoja yaani gunia tatu za mahindi zilizojaa.

Akamuelekeza mkuu wa JKT, piga ukuta kuzunguka mgodi wote zaidi ya kilomita 24. Mimi nilikuwa mmojawapo ya watu walioshangaa sana kwa sababu duniani hatujawahi kuzungusha ukuta mgodi.

Watani wa jadi wakatubeza sana, wakasema wapi wamezungusha ukuta mgodi, tukafikiria mimi huwa naamini kwamba imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo usiyoyaona. Kwenye chama chetu tunamuamini ndugu John Magufuli.

Baada ya muda mchache ukuta ukakamilika, nilienda 2019 nikauliza Tanzanite kiasi gani imezalishwa na mwaka huu nimepita. Takwimu za mwezi wa sita mwaka huu tanzanite iliyochimbwa ni zaidi ya kilogram 4,000 kutoka kilogram 300 kwa mwaka mzima.

Magufuli: Tumenunua ndege 11 kwa mpigo mpya, sisi ni masikini? Wapo watakaosema ndege za nini? Nyinyi mnapanda ndege? Wale wamepungukiwa kwelikweli. Kwa sababu ukishakuwa na ndege ndio itakayoleta madawa, watalii wakija hapa wataletwa na ndege ndio maana makusanyo ya fedha zilizopatikana kwenye utalii zimetoka bilioni na ushee mpaka 2.6 ni kwa sababu watalii wanaletwa na ndege. Ndege ni matunda ya kunesha nyinyi ni matajiri.

Hatukununua ndege tu, tumeanza kujenga reli ya umeme, vinavyopatikana ulaya tunavileta Tanzania, tumejenga mpaka Morogoro tunaendelea mpaka Dodoma Makutupora.

Tumeshatangaza juzi kuanza kujenga kutoka Mwanza mpaka Isaka, fedha zipo na tukimaliza, tunaanza Isaka mpaka Makutupora kwa fedha zetu.

Matusi ninayotukanwa mimi ninayafurahia kwa sababu hili ni jibu zuri kwa sadaka ya watanzania na ndio maana nimekuwa niwaomba muendelee kuniombea kwa sababu wale tuliowanyima nafasi ya kuiibia hii Tanzania hawatafurahia.

Mimi matusi niyapate lakini nyinyi mpate maendeleo ya kweli. Mimi nipo kwa niaba ya watanzania wote ndio maana ninawaomba kwa upendo mkubwa sana mturudishe tena katika miaka mitano myaone maajabu yale tutakayoyafanya.

Nitashangaa kama yote haya mazuri tuliyoyafanya katika awamu ya tano, shukrani yake iwe kunyimwa kura.
 
Tuvushe Baba upande wa pili hawataki kusikia maendeleo ya miundombinu hawajui hata nchi zilizoendelea zilianza na mageuzi ya miundombinu ndio vikaja viwanda. Watanzania tuna imani na wewe miaka tano kwako Mh. Rais John Pombe Magufuli.
 
Hapo Magufuli na Lisu wakipigana tena vijembe wataishia kutwangana ngumi za kweli kweli maana wapo kwenye mikoa iliyo karibu sana
 
Mlisema TBC inawahujumu na hapa mbona sauti inakoroma vilevile?
 
117195765_3213508722074131_2911542144163865371_n.jpg

Mods nimeweka post mmefuta. mna maana gani
 
Hapo sijasikia chochote kile kutoka ktk ilani ya mwaka huu zaidi majisifu yaleyale tuliyazoea kuyasikia. Nini yawe matarajio ya sekta binafsi, wafanyakazi, wakulima na makundi mengine ya kisekta kutokana na umuhimu wake?

Mtazamo wa mgombea uraisi wa CCM na kuona hoja kinzani kuwa ni matusi kwake ni jambo la kushangaza mno. Hoja kinzani ni lazima zijibiwe kwa hoja zenye mantiki na kueleweka, kama mgombea anaanza kulalamika mapema hivi kuwa anatukanwa sijui hadi tunafika mwisho wa muda wa kampeni sijui itakuwaje.

CCM leteni timu ya wanamkakati wa kampeni zenu kwa kuweka mbele watu kama Kamarade Kinana. Hawa vilaza aina ya Polepole wanachokiweza ni kuleta wasanii tu, ila mbinu sahihi za kujibu hoja ni sufuri kabisa. Yaani mwanzo kabisa wa kampeni za uchaguzi, inafikia kiwango cha Rais anayemaliza kipindi chake kuanza kulalamika kuwa anatukanwa na kuvumilia!

Hii ngoma ya kiutu uzima, hakuna kulala bali mwendo ni kukesha. Ebu acheni michezo ya kitoto ktk matukio muhimu ya watu wazima na wenye kustaarabika. Jibuni hoja kinzani, acheni visingizio visivyokuwa na mashiko yoyote yale.
 
Matusi ninayotukanwa mimi ninayafurahia kwa sababu hili ni jibu zuri kwa sadaka ya watanzania na ndio maana nimekuwa niwaomba muendelee kuniombea kwa sababu wale tuliowanyima nafasi ya kuiibia hii Tanzania hawatafurahia.
Mi matusi gani na nani amewahi kumtukana huyu Mzee wetu!? Let's be honest, hivi kwa kamatakamata ili na kupotezwa na kufungia media kuna mtu alithubutu hata kukohoa? Sikumbuki
 
Back
Top Bottom