Kampeni ya Kumshawishi Rais Magufuli Ajiunge JF

Kampeni ya Kumshawishi Rais Magufuli Ajiunge JF

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,303
Reaction score
23,064
Wana Jukwaa, sasa tuanzishe kampeni ya kuhakikisha Rais wetu JPM anakuwa verified member humu Jamii forum

Haiwezekani Rais atumie mtandao wa Twitter pekee wakati kuna mtandao wa kizalendo ambao ndio Mtandao unaokusanya kero na matatizo ya watanzania.

Hivyo popote Msaidizi wa Rais, au uliyekaribu na Rais tunakuomba umweleze Mh Rais kwamba Wana Great Thinker wanamhitaji humu, na humu ndio sehemu pekee tunaweza tukadiscuss mambo yetu.

Karibu Mh Rais Dr. John Magufuli

Cc Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye, Paul Makonda hk kigwangala, Msigwa, Rithiwan Kikwete, Humphrey Polepole

0c92947f29c6d6ee1debb18056af919a.jpg
 
Huku hawez kuja maana hana madaraka ya kuamuru nani apigwe ban km anavyofanya anapoamuru kule kwa watendaj wake....
Pia atakula za uso hadi aione dunia chungu ...... we unafanya masikhara had kutaman kufungia mitandao
 
Yaani itapendeza kwa kweli.Maana atapata dondoo nyingi zenye tija..vijana tumejaa madini vichwani lakini hatujapatiwa fursa.

Akiyafanyia kazi basi sina shaka nchi itafika mahala inatakiwa.Umoja ni nguvu.

Uzalendo kwanza...mambo mengine baadae.
 
Ili mumuandikie haya mnayoandikaga humu yasiyo na heshima na maneno machafu juu yake.

Mnataka JF ifungiwe kwenye mengi au!?

Jibadilisheni kwanza.... ndio mumuombe

Ila yeye kuwa msomaji ni vizuri tu, tabu wengi mnaandika upupwu juu yake hadi hawezi kuitaja forum hii.
 
wazo jema ila tushauri mambo ya maana kwake
 
alivyomuoga kukosolewa atakuwa anachungulia tu alishaagiza malaika waizime mitandao
 
Mtu mwenye uwezo mkubwa wa kukariri, kusoma na kuweka kumbukumbu kama JPM hawezi kukosa humu ninachotamani ni yeye kuingia kwa jina lake halisi na akaanzisha uzi wa :KATIKA UTAWALA WA AWAMU HII NINI UNGEPENDA NIFANYE, hapa angepata mawazo sahihi yasiyo ya woga
 
Back
Top Bottom