Kampeni ya kusafisha jiji la Dar es Salaam

Kampeni ya kusafisha jiji la Dar es Salaam

Tipstipstor

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2021
Posts
1,528
Reaction score
3,352
Poleni wahanga wa kampeni hii ya kuliweka "JIJI" katika hali ya "usafi".

Tumeshuhudia masoko yaliyopo katikati ya jiji letu pendwa yakiondoka moja baada ya moja ..Tulianza na

Soko la kariakoo🔥

Soko la mitumba karume 🔥

Wats next?

Ilala kwa wauza mitumba ?

Poleni wahanga hususani wale waliolaza mizigo yao ndani ya soko.Sidhani kama kuna mtu aliyefanikiwa kutoka hata na kiatu.

Uzi tayari
 
Machinga wanapigwa vita bure wakuu wale watu wa kwetu, mipango miji imekaa kiulayaulaya
 
kuna watu wanamuhujumu kiongozi mkuu, bila kujua wanamtengenezea chuki kwa wananchi masikini.Lets wait, time will tell.
 
Asijaribu soko la Mapinduzi Mwananyamala!
Huko vijijini hakuna ishu..hao jamaa wa Karume ilikuwa haina jinsi kila walivyoambiwa watoke hapo kupisha mradi wa ujenzi wa mwendokasi wanajifanya vichwa maji...ona sasa kilichotokea tena ni mita chache tu kutoka kwa Mkuu wa mkoa. Vibaka wanaenda kuongezeka mitaani...Wito wangu kwa serikali ni kuwa wasafishe hilo eneo halafu lijengwe soko la ghorofa then wamachinga wapewe vizimba ambavyo watalipia kodi kila siku ili kuingizia mapato serikali.
 
"KAMA MNATAKA MALI MTAIPATA SHAMBANI";

1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...
 
Sukuma gang naona mnafurahia sana
Uko dilemma kamanda, unataka kumshangilia "mama" ila ukikumbuka kuwa Mwenyekiti yupo korokoroni unanywea, ukitaka umkosoe " mama" unajikuta uko pamoja na sukuma gang [emoji51][emoji51][emoji51][emoji51][emoji51]
 
Uko dilemma kamanda, unataka kumshangilia "mama" ila ukikumbuka kuwa Mwenyekiti yupo korokoroni unanywea, ukitaka umkosoe " mama" unajikuta uko pamoja na sukuma gang [emoji51][emoji51][emoji51][emoji51][emoji51]
Siwezi kuwa na uswahiba na sukuma gang kwani walichowatendea watanzania ni Mungu tu atatoa hukumu juu yao.
 
Back
Top Bottom