Kampeni ya "Piga kazi, Boresha Makazi" yasaidia nyumba bora na za kisasa kujengwa Koromije, Mondo Misungwi Mwanza

Kampeni ya "Piga kazi, Boresha Makazi" yasaidia nyumba bora na za kisasa kujengwa Koromije, Mondo Misungwi Mwanza

Nyanswe Nsame

Senior Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
165
Reaction score
181
Kampeni ya Piga kazi boresha Makazi yasaidia nyumba bora na za kisasa kujengwa Koromije, Mondo Misungwi Mwanza

Nyumba bora na za Kisasa zimejengwa katika vijiji viwili vya Koromije na Mondo Wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Wakazi wa vijiji hivyo vya Mondo na Koromije wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza, wameamua kuondokaa na umasikini wa kuishi kwenye nyumba za nyasi baada ya kuunda vikundi vidogo vya kusaidiana kujengeana nyumba bora.

Nyumba hizo zimejengwa ikiwa ni katika kampeni inayoendelea wilayani humo ya Piga kazi boresha Makazi inayosimamiwa na shirika lisilo la kiserikali la kutetea Haki za wanawake na watoto la Kivulini na Serikali wilaya ya Misungwi.

Mmoja wa wana kikundi cha Witogwa, Getruda Luchangula amesema awali walikuwa wanaishi maisha duni, ambapo yeye pamoja na watoto wake saba walikuwa wakilala chumba kimoja.

Amesema jitihada zao za kuanza kujikwamua kiuchumi walizianza mwaka 2016 kwa kuanzisha kikundi kilichofahamika Witogwa na kufanikiwa kujenga nyumba 12 za wana kikundi.

Amesema kikundi chao kilichopo kijiji na kata ya Mondo, wamekuwa na utaratibu wa kuchangiana Tsh. 12,000 kila mwezi ambapo alibainisha kuwa kikundi chao wapo watu 18.

" Sisi kila mwaka tumekuwa na utaratibu wa kuwajengea wana kikundi wawili na mipango yetu ni kutaka kuondokana na nyumba za nyasi.

"Sasa hivi kama unavyoona nyumba zetu ni nzuri na bora ukilinganisha ni zile za zamani ambazo mvua ilipokuwa ikinyesha tulipata shida," amesema Getruda.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mondo, Nestory Malaya amesema kijiji hicho kina kaya 400 na kati ya hizo kaya 150 zina nyumba bora na za kisasa.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea Haki za wanawake na watoto la KIVULINI, Yasin Ally amesema katika kuhakikisha maendeleo yoyote yale yanafikiwa lazima nguvu ya uhamasishaji na ushawishi inakuwepo, kama walivyofanya wao iliyosaidia kuleta hamasa kwa wananchi hususani wana kikundi wa vijiji hivyo vya Koromije na Mondo.

Ally amesema harakati za kujenga nyumba bora na za kisasa katika wilaya ya Misungwi na vijiji hivyo vikianza Kama mfano, ilianza mwaka 2015, kwa kutoa elimu iliyosaidia kuleta mafanikio hayo.

"Hii kazi pamoja na kutumia ushawishi mkubwa na kuleta mafanikio haya tunayoyaona leo, lakini haikuwa kazi rahisi kuwashawishi kujiunga kwenye vikundi na kuanza kuchangiana," amesema Ally.

Mkuu wa wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Juma Sweda amesema wilaya yake imejipanga kuondoa nyumba za nyasi kwa kuwapa mbinu za kujikwamua wao wenyewe.

Sweda amesema lengo la wilaya hiyo ni kutaka kuona vijiji vyote zinajengwa nyumba za bati na kuachana na zile za nyasi huku akiwataka wananchi wengine kuiga mfano wa wana kikundi wa vijiji hivyo.

Akizungumza jana wakati akizindua kampeni ya Piga kazi boresha Makazi, Katibu Mkuu Wizara ya afya kutoka Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, DK. John Jingu amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuleta mageuzi kifikra na mtazamo wa jamii kuwa na moyo wa kujitegemea, uzalendo na kushika hatamu kujiletea maendeleo.

Pia Serikali imejipanga kuamsha ari ya jamii ya kusaidiana na kushirikiana katika shughuli za maeneleo ya jamii na ya mtu mmoja mmoja kwa kutumia mifumo ya asili iliyopo katika jamii.

Jingu amesema kupitia kampeni hiyo ya "Piga kazi boresha Makazi inachochea jamii kutumia mifumo, fursa na nguvu kazi kama vile vikundi vya kusaidiana VICOBA, SACCOS, Benki za kijamii na vyama vya ushirika wa nyumba na asasi za kiraia katika kuboresha Makazi yao.

IMG_20200822_091811.jpg


IMG_20200822_091842.jpg

IMG_20200822_091910.jpg


IMG_20200822_092037.jpg




Mwisho
 
Back
Top Bottom