Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Kwa Mtanzania mzalendo anayeipenda nchi yake, wala haihitaji akili nyingi wala 'D' mbili kuweza kutambua jinsi nchi ilivyorudi nyuma tangu awamu hii iingie madarakani. Tukiacha suala lililopo mezani la utekaji na mauaji makubwa ya kutisha linalopelekea raia na watanzania kuishi kwa hofu na kikosa amani, Hali ya maisha kwa watanzania kiujumla imekuwa ngumu mno! Huku serikali ikionekana kukosa nipamgo madhubuti kusaidia watanzania. Kila mtanzania analia ugumu wa maisha. ajira zimekuwa ngumu, vitu vimepanda bei, huduma za afya zimekosa muelekeo huku tukishuhudia bima muhimu za afya zikiondolewa.
Haya yote yanafanyika huku tukimshuhudia kiongozi mkuu wa nchi akizurura huku na huko na kutegemea mikopo na hisani za mataifa yanayokuja na masharti mabaya kwa taifa! Hakuna mikakati na mipango mingine inayoonekana katika kusaidia watanzania kijikwamua na umasikini, maradhi na ujinga huku uwezo wa kiongozi mkuu wa serikali ukijidhihirisha kuwa mdogo na viatu kumpwaya!
Kwa hayo machache nadhani 'SAMIA MUST GO' inapaswa kuwa wimbo wa kila Mtanzania mzalendo anayeipenda nchi yake.