Kampuni gani hutengeneza betri imara za Magari madogo ukiachana na Cloride exide?

Kampuni gani hutengeneza betri imara za Magari madogo ukiachana na Cloride exide?

King_Villa

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2012
Posts
575
Reaction score
380
Habari wakuu,

Nahitaji kununua betri mpya kwa ajili ya gari yangu ila ningependelea kampuni tofauti na hiyo chloride exide maana nimeitumia muda mchache sana ,kiufupi sijaipenda (au ni matumizi yangu).

Bila shaka nataka kubalisha kampuni nione kama naweza kupata kampuni tofauti na hii

Na kama kuna mtu anajua mahali wananunua betri mbovu anaweza nielekeza.

Sasa naomba ushauri wenu maana
 
Umeitumia kwa muda gani?

Typically battery ina last 6 years.
 
Battery gani hiyo ina last for 6 years? Viwanda vya battery si vingefungwa[emoji28][emoji28]
Anafanya masihara huyo 😅!!!

The best batteries ikivumilia sana ni 2 good years before it starts to be problematic! Mie natumia MaxxBat ni la Kikorea liko bomba tu.

Nilinunua mwaka juzi nikapewa warranty ya mwaka mpaka sasa linapiga kazi vizuri tu!
 
betry ya gari yangu n50,nimemwaga maji yote,nikaweka maji makali upya na kuichaji,baada ya siku 2 tu,haiwezi hata kupiga start kwe nye noah,najipanga ninunue betri mpya tu,ingawa kampuni nzuri sizifahamu...
Betri za kuweka maji achana nazo. Nunua maintenance free. Kwa wale wenye gari za diesel za betri mbili. moja ikifa ondoa zote weka mpya.
 
Battery gani hiyo ina last for 6 years? Viwanda vya battery si vingefungwa[emoji28][emoji28]

Battery nyingi tu zinaweza kulast 5 to 6 years.....

Shida ni moja zipo sababu nyingi ambazo zinachangia kufa kwa battery.

Kuna toyota Fielder ya 2012 imenunuliwa 2016 toka Japan ila mpaka dakika hii battery inagonga kazi kama kawaida... Haina hata dalili ya kufa. Hiyo ni miaka mingapi?

Mtu unanunua battery mwezi tu ishaanza kuweka maungaunga, unadhani itamaliza hata miaka miwili?
 
Kuna brand mpya inaitwa Rhino nilinunua January bei yake ni laki 1 na elfu 30. Hadi sasa haijasumbua. Jaribu kuitafuta hiyo mkuu. Ila kiukweli hizi betri za bei ya chini ya laki 2 na nusu matumizi yake sio zaidi ya miaka miwili kwasababu zinakuwa sio za Viwango sahihi. Kifaa cha gari cha kukaa muda mrefu lazima kiwe cha bei ghali.
 
Varta ukinunua kwa Dealer Warranty miezi 24. N 70 inaenda Laki 8
Varta N95 ni laki nne na elfu 18

hapo ni superdoll si kwa mawakala wengine.

ila hizi ni betri za uhakika mimi ninazo natumia kwa vyombo tofauti miaka mitatu kingine miwili na kimoja nimenunua kwenye tarehe 15/16 mwezi wa tisa.

Sent from my M2006C3LI using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom