Kama mada inavyojieleza ni kampuni gani nzuri, waaminifu, timely, kwenye kuagiza gari. Maana siku hizi kuna makampuni mengi, lakini tatizo linakuja wengine ni matapeli, wengine ni majizi, wengine utaagiza Fuso unaletewa Canter, wengine gari inakuja vitu vimechomolewa, wengine watakuambia hiyo gari ilishachukuliwa japokuwa wamekutumia invoice na ukalipa kwa wakati. Kwa sahivi kuna makampuni mengi kwa mfano BEFOWARD, SBT JAPAN, CARJUCTION,TRADECAR VIEW, TRUST JAPANIES VEHICLES, n.k
So kumekuwepo na matatizo mbalimbali kadha wa kadha kwenye uagizaji wa magari kutoka kwenye makampuni mbalimbali. Kwahiyo tushirikiane kwenye experience kuhusiana na kampuni ambazo wamekuwa waamifu kwa wakati, mali, pamoja na changamoto tulizopata kwenye uagizaji wa magari na kadhalika.
Kupeana experience itawasidia wengine kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza
Karibuni