Kampuni inayojenga Uwanja wa ndege Chato, Mayanga Construction inamilikiwa na nani na ilipataje tenda hiyo?

Kampuni inayojenga Uwanja wa ndege Chato, Mayanga Construction inamilikiwa na nani na ilipataje tenda hiyo?

Jee ni kampuni yako? Au una hisa kiasi gani? Kwa nini inapewa miradi mikubwa na kulipwa kisha haikamilishi kazi kama kule Musoma na Geita na haichukuliwi hatua za kisheria?

Kwa nini inapewa miradi ambayo hata uwezo wa kuifanya unatia wasiwasi kama itafanya kwa kiwango kwa mfano Chato Airport?

Na mbona yenyewe inapata miradi ambayo hata tenda zake hazitangazwi?

Kama mgombea urais ambaye unajinasibu kuwa ni muadilifu ni vema ujibu hii issue ya Mayanga Construction maana inakuchafua/inaonyesha kuwa hufai kabisa.

Mbona mengi unajibu haraka au wapambe wako wakiongozwa na Msigwa au Polepole wanajibu, inakuwaje hili linawashinda? Au ni fupa gumu kulijibu?
Natumaini watakujibia hili ili tukuelewe!
Huwezi kupambana na rushwa kwa namnavhii,huu ni ufisadi
 
Jee ni kampuni yako? Au una hisa kiasi gani? Kwa nini inapewa miradi mikubwa na kulipwa kisha haikamilishi kazi kama kule Musoma na Geita na haichukuliwi hatua za kisheria?
wapiga kura hawataki kusikia hayo
 
Ni kwa nini? Hawana elimu ya kujitambua? Au ni nini?
yana muda wake hayo masuala
muda huu watu wanataka kujua utafanya nini ili kuyafanya maisha yao kuwa rahisi
watu wanataka ugali weww unazungumzia sijui mayanga construction ya nani rais aeleze ya nani,kwani BRELA hupajui?ukilipa 22,500 faili linaletwa mezani unafunua kurasa moja baada ya nyingine
 
Washikaji sana

JPM Mwaka 1977 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza.

1623738_Chato.png
 
Haaaaa umenikumbusha mbali Mayanga
Kuna wimbo moja wa zamani unaitwa Mayanga. Mmoja wa ubeti unaimba hivi" Mayanga uliponitoa kwetu sumbawanga ulisema wewe huku mjini ni Meneja kumbe wewe si Meneja, Ona Sasa nateseka Mayanga, Narudi kwetu Sumbawanga" Naupenda Sana wimbo huu.
 
Mkuu wangu, nadhani hilo la uadilifu umemuwekea..yeye ni mnyenyekevu. Pengine uulize swali juu ya unyenyekevu wake.
 
yana muda wake hayo masuala
muda huu watu wanataka kujua utafanya nini ili kuyafanya maisha yao kuwa rahisi
watu wanataka ugali weww unazungumzia sijui mayanga construction ya nani rais aeleze ya nani,kwani BRELA hupajui?ukilipa 22,500 faili linaletwa mezani unafunua kurasa moja baada ya nyingine
Toa Jiwe weka mtu anayeeleweka na mzalendo halisi Mh Lissu. Mwaka huu lazima Jiwe arudi kwao

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Jee ni kampuni yako? Au una hisa kiasi gani? Kwa nini inapewa miradi mikubwa na kulipwa kisha haikamilishi kazi kama kule Musoma na Geita na haichukuliwi hatua za kisheria?

Kwa nini inapewa miradi ambayo hata uwezo wa kuifanya unatia wasiwasi kama itafanya kwa kiwango kwa mfano Chato Airport?

Na mbona yenyewe inapata miradi ambayo hata tenda zake hazitangazwi?

Kama mgombea urais ambaye unajinasibu kuwa ni muadilifu ni vema ujibu hii issue ya Mayanga Construction maana inakuchafua/inaonyesha kuwa hufai kabisa.

Mbona mengi unajibu haraka au wapambe wako wakiongozwa na Msigwa au Polepole wanajibu, inakuwaje hili linawashinda? Au ni fupa gumu kulijibu?
Natumaini watakujibia hili ili tukuelewe!
Mkuu Chakaza, natumbua ufuasi wako uliotukuka upande unahoji hilo unalotaka lijibiwe. Bahati mbaya huyo unayemshabikia, kama wewe, hamjui ni lipi la kufikisha mbele ya wapiga kura, wakati wa kampeni.

Hilo unalotaka lijibiwe siyo la kisera ni la kiutendaji. Iwapo anayetuhumu akiingia madaraka, basi anayo mamlaka ya kulishughulikia. Kukomaa nalo kwenye kampeni ni ushahidi kuwa hakuna Sera mbadala za kuwashawishi wapiga kura.

Kama ambavyo nimekuwa nikihoji humu JF, je, huyo mgombea anatambua kuwa hayuko mahakamani bali kwenye jukwaa la kisiasa tena kwenye kampeni.

Lengo lake ni kumchafua Magufuli. Huu ndio mtiririko wa lengo hilo:
√ Alirejea nchini kwa mikwara akitarajia angezuiwa au kukamatwa, ikabuma;
√ Kwa makusudi akavunja protokali ya kumwaga marehemu Mkapa uwanjani, ili aingiapo aamshe shangwe, akakwama;
√ Akamwekea Magufuli pingamizi, ikashindikana;
√ Badala ya kutafuta wadhamini akamua kwa makusudi kufanya kampeni akitarajia Tume ingemchukulia hatu, nalo likapita; na
√ Sasa ameshindwa kueleza Sera ya Uhuru, Haki na maendeleo ya watu hivyo anatafuta njia itayoilazimisha Tume imchukulie hatua ili azima yake ya mawakili wake kumchukulia hatua Magufuli itimie. Nalo limekwama.

Amethibitisha ni mtu jeuri, mwenye dharau na mnafiki wa hali ya juu
 
wapiga kura hawataki kusikia hayo
Hivi hao mnaowaita wapiga kura ni kina nani? Kwani mleta mada siyo mpiga kura? Mimi hapa napiga kura na nataka kujua kuhusu Mayanga kwa sasa ni nani kwa Magufuli na kwa nini tenda anazopewa hazitangazwi na Magufuli kakaa kimya? Nafahamu ukaribu wao maana Mayanga alikuwa mfadhili wa Magufuli tangu akiwa Nyanza. Huyu tangu enzi za Mzee wake ni mlezi wa Magufuli kiuchumi mpaka akapata Ubunge Chato na kisha Uwaziri. Aliyenacho huongezewa na mdivyo ilivyotokea kwa Mayanga baada ya Magufuli kupewa wizara inayohusiana na biashara ya Mayanga. Baada ya Kuonja utamu wa wizara hiyo Magufuli hakutaka wizara nyingine. Huku akijifanya mkali na mfuatiliaji, ghafla akagusa ulaji wa wakubwa zake kwa kuzuia malori. Ikazuka Songombingo kubwa hadi kutaka kujiuzulu baada ya Pinda kwenda kutema mbovu jimboni kwake Chato mbele ya wapiga kura wake, lakini akazuiwa na Mkapa na kuahidiwa makubwa huko mbele. Baada ya hapo akahamishiwa Wizara ya uvuvi ambayo hakuipenda akidhani miradi yake na ya marafiki zake itachokonolewa lakini Kikwete alijua kula na vipofu akamwacha.
Sasa atuambie analipa fadhila au anaendeleza miradi yake?
 
Hii kampuni kule kanda ya Ziwa pekee amepewa tenda ya Tshs Trilioni moja kwa miradi miwili! Nilitamani nione bond yao waliyoweka hadi wakapewa miradi mikubwa namna hiyo hasa kwa huu utawala wa Magufuli!

Ilianza Ghana pale miaka ileeeee
 
Back
Top Bottom