Mkuu
Chakaza, natumbua ufuasi wako uliotukuka upande unahoji hilo unalotaka lijibiwe. Bahati mbaya huyo unayemshabikia, kama wewe, hamjui ni lipi la kufikisha mbele ya wapiga kura, wakati wa kampeni.
Hilo unalotaka lijibiwe siyo la kisera ni la kiutendaji. Iwapo anayetuhumu akiingia madaraka, basi anayo mamlaka ya kulishughulikia. Kukomaa nalo kwenye kampeni ni ushahidi kuwa hakuna Sera mbadala za kuwashawishi wapiga kura.
Kama ambavyo nimekuwa nikihoji humu JF, je, huyo mgombea anatambua kuwa hayuko mahakamani bali kwenye jukwaa la kisiasa tena kwenye kampeni.
Lengo lake ni kumchafua Magufuli. Huu ndio mtiririko wa lengo hilo:
√ Alirejea nchini kwa mikwara akitarajia angezuiwa au kukamatwa, ikabuma;
√ Kwa makusudi akavunja protokali ya kumwaga marehemu Mkapa uwanjani, ili aingiapo aamshe shangwe, akakwama;
√ Akamwekea Magufuli pingamizi, ikashindikana;
√ Badala ya kutafuta wadhamini akamua kwa makusudi kufanya kampeni akitarajia Tume ingemchukulia hatu, nalo likapita; na
√ Sasa ameshindwa kueleza Sera ya Uhuru, Haki na maendeleo ya watu hivyo anatafuta njia itayoilazimisha Tume imchukulie hatua ili azima yake ya mawakili wake kumchukulia hatua Magufuli itimie. Nalo limekwama.
Amethibitisha ni mtu jeuri, mwenye dharau na mnafiki wa hali ya juu