Kampuni ipi ya kuandaa Movie inakukosha?

Kampuni ipi ya kuandaa Movie inakukosha?

Kwa mfano hapo ameorodhesha Lionsgate, Warner Bros, colombia Picture kwamba ni waandaaji Kafanya mchanganyo balaa..

Lionsgate ni kampuni ya uandaaji na sio usambazaji ipo chini ya Warner Bros. WB ndio wasambazaji wa muvi za Lionsgate. Warner Bros wanamiliki Dc Comics/Film... Kwasasa kampuni ya WB. Inaitwa Warner Bro. Discovery maana iliungwa na kampuni ya Discovery na kua moja...

Kataja Colombia Picture but hao ni wasambazaji waandaaji hua ni Sony. Colombia picture ipo chini ya Sony. Ndio maana muvi zote za Spiderman lazima zisambazwe na Colombia Pictures maana Spider-Man character inamilikiwa na Sony!
Lionsgate haiko chini ya WB. Ni kampuni tanzu ya Lionsgate Entertainment Corp. Inafanya production na pia inafanya distribution. Major studios zote huwa zinafanya production na pia distribution. Kuna movies zinatengenezwa na studio zenyewe na kuna movies zinazotengenezwa na kampuni ndogo halafu wanaingia deals za distribution na major studios.
 
Mm napenda horror and thriller movies, sasa nikijua ni Warner Bros wamehusika kwa namna yoyote ile bc Sina haja ya kufuatilia story wala kuangalia trailer Mimi hapo ni kuweka salio na kupakua hiyo movie.
Mimi na wewe tuko kundi moja.
Hizi haunting, horror, sijui thriller na za kutisha zile zenyewe.
Nikiona nembo ya BLUMHOUSE.....nakaa jicho moja nimefumba, BLUMHOUSE wakali wa horror, hatari sana.
Screenshot_20240125-203624.jpg
 
Kampuni ya CCM hasa ile movie ya "TUMESHINDA KWA KISHINDO" Ya mwaka 2020 ilitisha sana
 
Back
Top Bottom