Kampuni kutotoa nafasi za Madereva wapya wa malori kuchangamana na wazoefu, watatoa wapi uzoefu?

Kampuni kutotoa nafasi za Madereva wapya wa malori kuchangamana na wazoefu, watatoa wapi uzoefu?

FRJ255

Member
Joined
Oct 11, 2024
Posts
23
Reaction score
21
Kwa sasa kumekuwa na ongezeko la mahitaji ya madereva katika kampuni za usafirishaji, hususan madereva wa malori yanayofanya safari za ndani na nje ya nchi. Hata hivyo, kampuni nyingi zinahitaji madereva wenye uzoefu wa angalau miaka 3 hadi 5.

Kero yangu ni kwamba baadhi ya kampuni hizi zimeondoa utaratibu wa madereva wapya kuandamana na madereva wenye uzoefu (turnboy) ili kujifunza na kupata uzoefu wa kazi. Sasa tunajiuliza, madereva hawa wapya na wachanga watapata wapi uzoefu unaohitajika ikiwa hawapewi nafasi ya kujifunza kwa vitendo?

Mafunzo na mazoezi wanayopewa wanafunzi wa HGV katika VETA ni muhimu, lakini hayatoshi pekee yake. Mara nyingi mafunzo hufanyika mijini na gari likiwa tupu, hivyo mwanafunzi hapati nafasi ya kukabiliana na changamoto halisi za barabarani, kama vile milima mikali, miteremko, kona kali, uzito wa mizigo, mifumo ya breki, mizani na changamoto nyingine zinazojitokeza katika safari za masafa marefu.

Tunaomba kampuni za usafirishaji na mamlaka husika zitafakari upya utaratibu huu na kuweka mfumo wa kuwawezesha madereva wapya kupata uzoefu wa vitendo chini ya usimamizi wa madereva wenye uzoefu. Hii itasaidia kujenga madereva wenye ujuzi na pia kuongeza usalama barabarani.
 
Back
Top Bottom