ya 2015
Hivi majuzi nilibahatika kuzunguka baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara/Tanganyika kwa kutumia usafiri wa mabasi ya abiria.
Cha kusikitisha basi moja la kampuni fulani nililopanda lilikuwa na kungunguni wengi ajabu. Kunguni wale hawakuwa na aibu walikuwa wanatoka kwenye ma'cover'/foronya ya/za viti vya basi hilo na kung'ata mchana kweupe.
Wakati tunaanza safari hiyo basi lilikuwa halijajaa, Baada ya kuwastukia kunguni wale kwenye siti yangu nikaamia kwenye kiti/siti nyingine, kule ndo nikakumbana na kunguni watoto lakini 'barubaru' kwa kung'ata, Nikarudi kwenye siti yangu ya awali.
Sikuvumilia kung'atwa na kunguni wale bila kulalamika, nilimuita konda kumueleza kero ya kunguni kwenye basi lake. Kwa siri , konda, nikamuonyesha kikosi cha kwanza cha kunguni kilichokuwa kwenye egemo la mgongo wangu waliojibanza karibu na tobo la foronya la siti yangu. Akashtuka 'kiana', alichosema nikuwa basi lile alikabidhiwa jana yake.
Na jana hiyo kazi aliyoanza nayo ni kupambana na mende kwenye basi hilo waliokuwa wengi kiasi cha kutishia abiria kususia basi. Akanihakikishia kuwa na hao mende hakuwamaliza vizuri.
Mwisho wa mazungumzo yetu alimrudikia konda aliyekuwa anasimamia basi hilo hapo awali kwa usumbufu huo. Nilichokifanya, tulipofika sehemu ya kuchimba dawa, mimi nilishuka kwenye basi hilo na kwenda kuchimba namba za gari/basi hilo maana walikuwa hawajaandika namba za basi hilo kwenye tiketi/risiti ya nauli ya basi.
Nilisafiri kwenye basi hilo nikiwa roho juu, ingawa haikuwa mara yangu ya kwanza kuumwa/ng'atwa na kunguni! Niliwahi kungatwa nilipokuwa shule ya Bweni enzi hizo.
SWALI KWA WADAU:
1. Ni nani anahusika kuwawajibisha, wamiliki, makonda, hata madereva wa mabasi yenye kuhatarisha afya za wasafiri?
2. Mimi kama abira sikunyingine nikikumbania na kadhia ya namna hiyo nikashtaki wapi ili wawajibishwe wahusika kwa uzembe huo?
USHAURI:
Abira wote wa vyombo vya usafiri kuweni makini mnapopanda vyombo hivyo kwa kuhakikisha havina vihataraishi vya afya zenu kama, kunguni, mende, nakadhalika.
Update:
=======
Kama nilivyoahidi: ZUBE TRANS (Moshi-Mwanza), siti namba F1, T954 AHH: nauli 35,000/=
we
Kunguni na Mende ndani ya basi la abiria!