Hilo ni moja, sasa isome kwa ukamilifu uone. Haina hadhi ya kuandikwa na Mheshimiwa.
Mwanzo tu, kaanza na "I hear" inaonesha ni mtu ambae alikuwa anatafsiri Kiswahili "nnasikia". na lugha hizi zina misamiati yake jamani, msitetee kitu ambacho kinampotezea sifa. Hivi mwanao unaemoenda nyumbani hata akifanya kosa wewe unamwambia ni sawa tu? kama kweli unampenda inabidi umrekebishe asirudie makosa.
Kumbuka huyu ni Mbunge wa Bunge la Tanzania na akiwa kama Mbunge anakuwa ni mwakilishi wa wananchi wote ni si wa "magwanda' tu na mimi kama Mwananchi nna haki ya kumrekebisha Mbunge wetu kwani anatutia aibu tunaonekana wote kama yeye, wakati sivyo, tungejivuna angeandika ujumbe wake kwa Kiswahili tena ukumbuke huo ujumbe walengwa ni Watanzania, hapa sasa mnanikumbusha mswaada mara ya kwana Bungeni, uliwalenga Watanzania ukaambiwa utafsiriwe ukaletwa Kiswahili, na Mheshimiwa Sugu hapa bado ana nafasi ya kuurekebisha huu usemi wale aliyotumia lugha asiyoijuwa vizuri.