Kampuni ya Algeria kuwekeza viwanda vya korosho Tanzania

Kampuni ya Algeria kuwekeza viwanda vya korosho Tanzania

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
Kampuni ya Algeria kuwekeza viwanda vya korosho Tanzania

Kampuni ya ubanguaji wa korosho ya Sarl Anacard’Or ya Algeria inatarajia kutanua uwekezaji wake kwa kujenga viwanda vitatu nchini Tanzania ili kuongeza zaidi faida yake katika soko la dunia.

Akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, wakati wa ziara yake kwenye kiwanda cha korosho cha kampuni hiyo jijini Oran, mmiliki na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Walid Dib, alielezea mpango wake wa kuwekeza viwanda vitatu vya kisasa vya ubanguaji wa korosho nchini ili kufaidika na fursa ya korosho ya Tanzania inayosifika kwa ubora wake duniani.

“Korosho ya Tanzania ina ubora wa kipekee na tumeamua tujenge viwanda vitatu tukianzia na cha Masasi mkoani Mtwara kitakachotumia mashine za kisasa kutoka Vietnam,” alisema Bw. Dib ambaye tayari kwa kushirikiana na mbia wa ndani anakamilisha usajili wa kampuni ya kwanza itakayoitwa Kilimanjaro Nuts Limited.

Akimpongeza Bw. Dib kwa kuanza mchakato wa uwekezaji nchini Tanzania, Balozi Matinyi alimuahidi kwamba serikali itampatia ushirikiano wote anaohitaji ili atimize ndoto yake ambayo itaongeza ajira na mapato kwa serikali pamoja na kuleta ujuzi zaidi na fedha za kigeni nchini.

“Ni nia ya serikali kuhakikisha kuwa uwekezaji wa viwanda vya ubanguaji unaongezeka nchini ili kulipa thamani zaidi zao hili kabla ya kuuzwa nje na kupunguza uuzaji wa korosho ambazo hazijabanguliwa,” alisema Balozi Matinyi.

Bw. Dib aliongeza zaidi kwamba hivi sasa anaandaa maghala ya kuhifadhia korosho wilayani Masasi mkoani Mtwara, na mwezi Septemba ataagiza mashine kutoka Vietnam ambazo zitawasili nchini na wataalamu wa kuwapa mafunzo wenzao wa Tanzania kuanzia mwezi Januari 2027.

Akielezea mafanikio yake ya kuagiza korosho ya Tanzania, Bw. Dib alimwonesha Balozi Matinyi korosho za Tanzania zilizopitia hatua 11 za uzalishaji kiwandani hapo hadi kufungashwa na kuwa tayari kwa mauzo, akisisitiza kwamba sasa ameamua kununua korosho za Tanzania pekee.

“Nilipokea makontena sita mwezi uliopita; sasa hivi nina mengine sita bandarini Oran huku saba yakiwa njiani baharini na mengine saba bandarini Dar es Salaam yakisubiri kuanza safari, na kila kontena limebeba tani 27 za korosho,” alisema Bw. Dib.

Akihitimisha ziara yake kiwandani hapo, Balozi Matinyi alisema juhudi za serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), zimefanikisha uzalishaji wa zao hilo hadi kufikia tani 617,683 kwa mwaka katika kipindi cha mwaka 2025/26 zilizoingiza Shilingi trilioni 1.25 na kuifanya Tanzania iendelee kuwa moja ya wazalishaji wakubwa duniani baada ya Cote d’Ivoire, Vietnam na India.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania
Algiers, Algeria, Agosti 20, 2026.






Algerian firm to invest in cashew nut factories in Tanzania

Algerian cashew nut processor, Sarl Anacard’Or cashew, is looking to expand its investment by establishing three factories in Tanzania in an endeavour to enhance profitability on the global market.

Speaking to the Tanzanian Ambassador to Algeria, His Excellency Mobhare Matinyi, during his visit to the company’s facility in the city of Oran, the company’s owner and CEO, Walid Dib, expounded on his plan to invest in three modern cashew nut processing plants in the country to benefit from the renowned quality of Tanzanian cashew nuts.

“Tanzanian cashew nuts are of exceptional quality and we have resolved to build three plants first establishing one in Masasi, Mtwara region, where we will install modern machinery from Vietnam,” said Dib, who is already working with a local partner to finalise the formalisation of an inaugural company, Kilimanjaro Nuts Limited.

Congratulating Dib for commencing the investment process in Tanzania, Ambassador Matinyi assured him of the government’s support towards the fulfillment of his dream, which will expand employment and increase government revenue, as well as bring more skills and foreign revenue into the country.

“It is the government’s intent to support investment in local cashew nut processing to boost the percentage of value-added exports to the global market, and significantly reduce the sale of in-shell raw cashew nuts,” said Ambassador Matinyi.

Dib further added that he is currently readying storage warehouses in Masasi district in Mtwara, and that in September he will order equipment from Vietnam, expected to arrive in the country with experts to train their Tanzanian counterparts from January 2027.

Describing his success in importing Tanzanian cashews, Dib showed Ambassador Matinyi Tanzanian cashew nuts that went through 11 stages of production at the Oran factory before being packaged ready for sale, stressing that he has now chosen to stick with Tanzanian cashews.

“I received six containers last month; I have six more at the port of Oran while seven are on their way in, with another seven at the port in Dar es Salaam waiting to be shipped, and each container is packed with 27 tonnes of cashews nuts,” he said.

Concluding the visit, Ambassador Matinyi said the government's efforts through the Tanzania Cashew Board (CBT) increased production of the crop to 617,683 tonnes in the year 2025/26, which brought in Sh.1.25 trillion, makingTanzania one of the largest global producers after Cote d'Ivoire, Vietnam and India.

Issued by the Embassy of Tanzania
Algiers, Algeria, August 20, 2026.
 

Attachments

  • IMG-20260820-WA0051.jpg
    IMG-20260820-WA0051.jpg
    302.3 KB · Views: 5
  • IMG-20260820-WA0050.jpg
    IMG-20260820-WA0050.jpg
    308.4 KB · Views: 8
  • IMG-20260820-WA0049.jpg
    IMG-20260820-WA0049.jpg
    169.5 KB · Views: 10
Back
Top Bottom