Kampuni ya Bajaj imetoa toleo jipya la pikipiki aina ya Boxer 125 HD

Kampuni ya Bajaj imetoa toleo jipya la pikipiki aina ya Boxer 125 HD

Tatizo kubwa la pikipiki za boxer ni( ring piston na block )
Hata uzingatie kubadilisha oil kila baada wiki mbili au baada km 1000 kuna siku itazingua tu.
Last time kuwa na boxer ni lini mkuu mbona jamaa wanafanya improvement.
Mathalani zile rough road hasa X125 zile bike zina block mbovu sijapata kuona.
Baada ya kuwasema kwenye pages zao wakafanya improvements kwa kuleta toleo jipya almaarufu kijora hizi zenye block na cylinder rangi nyeusi.
And now ndio wamekuja na hili toleo jipya la kijora ambacho hakina paper oil filter hebu tuone zitakuaje.
 
Halafu shida hizi boxer mafundi wanabahatisha bahatisha tuu, walau serikali imezigawa kwa watendaji na maafisa ugani sasa hata ndani ndani huku tunapata spare
Hilo likowazi mafundi sio wengi maana asilimia kubwa kuanzia kibaha kwendea huko mikoani bike pendwa ni zile za kichina kwahiyo mafundi wengi hawazijulii na hawana uzoefu nazo
 
Mi nawasubiria TVS wajibu mapigo. Tatizo wamewekeza sana kwenye izo za bodaboda.

Kuna pikipiki ya TVS inaitwa TVS Apache RR 310. Aisee shikamoo.

1000112170.jpg
 
Kwa Tanzani naenda wapi? Maana niliona zile Apache 160 na 180 sikuzipenda.
Kwa hapa Dar sijajua hasa nani ni importer na dealer mkubwa wa TVS.
Hivyo ni suala la kufuatilia tu kufahamu dealer na kwenda kuongea nao hakuna kinacho shindikana boss
 
Kwa Tanzani naenda wapi? Maana niliona zile Apache 160 na 180 sikuzipenda.
Dealers wa Tvs wapo pale Azikiwe karibu na Posta office wanaitwa Car& General traders wahindi hawa na wanashow room hapohapo kuna brand kadhaa za pikipiki ila hayo ma Apache sijaona.

Nilikuta hizi automatic za bila gear kama Honda zile wanauza 4.2M
 
Wadau mimi nimetoka kujifunza pikipiki juzi nataka ninunue mpya niwe bodaboda.
Naomba ushauri wenu ninunue chombo ipi kati ya TVS au BoXer
 
Back
Top Bottom