Kampuni ya BioNTech kuwasilisha vifaa vya uzalishaji chanjo Afrika kwa nchi ya Senegal, Rwanda na Afrika Kusini

Kampuni ya BioNTech kuwasilisha vifaa vya uzalishaji chanjo Afrika kwa nchi ya Senegal, Rwanda na Afrika Kusini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1645092434364.png

Kampuni ya kutengeneza chanjo ya Ujerumani BioNTech leo imetangaza mpango wa kupeleka vifaa vya kutengeneza chanjo zake barani Afrika.

Kampuni hiyo ambayo pamoja na kampuni kubwa ya madawa ya Pfizer ilitengeneza chanjo ya kwanza ya virusi vya corona iliyoidhinishwa na Umoja wa Ulaya na Marekani, imesema inapanga kuwasilisha vifaa hivyo vya kutengeneza chanjo nchini Rwanda, Senegal na Afrika Kusini.

Vifaa hivyo vitawezesha utengenezaji wa chanjo za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona na katika siku zijazo, pamoja na chanjo za malaria na kifua kikuu. BioNTech imesema awamu ya kwanza ya vifaa hivyo inatarajiwa kuwasili katika nusu ya pili ya mwaka huu wa 2022 na utengenezaji wa chanjo utaanza miezi 12 baada ya kuwasilishwa kwa vifaa hivyo.

Chanzo: DW Swahili
 
Back
Top Bottom