Kampuni ya China kupata kandarasi ya kujenga Uwanja Mpya wa Soka Tanzania ni mwendelezo wa ushirikiano katika kuboresha miundombinu

Kampuni ya China kupata kandarasi ya kujenga Uwanja Mpya wa Soka Tanzania ni mwendelezo wa ushirikiano katika kuboresha miundombinu

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1713938763170.png

Katikati ya mwezi Machi serikali ya Tanzania ilitangaza kuwa Kampuni ya Uhandisi wa reli ya China (CRCEG) ilishinda zabuni na kupata kandarasi kujenga uwanja mpya wa soka mkoani Arusha, na kusaini makubaliano na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania. Uwanja huu utakuwa ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania kuwa mwenyeji mwenzi wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Ushirikiano kati ya China na Tanzania kwenye ujenzi wa miundombinu imekuwa ni moja ya maeneo muhimu ya ushirikiano wa kidiplomasia kati ya pande hizo mbili. Kwa wanaofuatilia historia ya ushirikiano kati ya China na Tanzania kwenye ujenzi wa miundo mbinu, bila shaka hili si jambo jipya, kwani wanaweza kukumbuka ujenzi wa reli ya TAZARA na bomba la mafuta la TAZAMA.

Uwepo wa China kwenye ujenzi wa miundombinu nchini Tanzania ni jambo ambalo watanzania wa kawaida na hata serikali ya Tanzania wameona matokeo chanya.

Tukiachia mbali madaraja yanayopunguza changamoto za watu kusafiri katika kipindi chenye hali mbaya ya hewa, au majengo mbalimbali yanayopendezesha miji, miundombinu inayojengwa na China nchini Tanzania imesaidia kuipa sifa Tanzania kimataifa.

Mfano wa hivi karibuni ni ule wa uwanja wa ndege wa Abedi Amani Karume, ambao umetajwa kuwa ni moja ya viwanja bora vya ndege barani Afrika. Mbali na uwanja huo wa ndege Uwanja wa soka wa Benjamin Mkapa wa Dar es salaam, pia umeipatia sifa Tanzania kiasi kwamba mwaka 2010 timu ya soka ya taifa ya Brazil iliridhia kucheza mechi ya kirafiki kwenye uwanja huo na kuitangaza Tanzania kimataifa.

Pamoja na kuwa kandarasi ya ujenzi wa uwanja wa soka wa Arusha ni jambo la kibiashara na sio msaada wala hisani, ukweli ni kwamba kutokana na muundo wa ushirikiano kati ya China na Tanzania, au nchi za Afrika kwa ujumla, mradi kama huo unaambatana na manufaa mengi sana kwa nchi inayopokea mradi kama huo.

Ni wazi kuwa baadhi ya viwanda vya Tanzania vitapata kandarasi ndogo kwenye mchakato wa ujenzi wa uwanja huo, idadi kubwa ya vijana wa Tanzania wanatajaia kupata ajira mbalimbali, na hata suala la kusafirisha teknolojia pia litaonekana kwenye mradi kama huo.

Jambo lingine tunaloweza kuona kwenye suala hili ni kuwa China inaendelea kuthamini na kutambua umuhimu wa soka kwa nchi za Afrika. Kama tukijaribu idadi ya viwanja vya soka barani Afrika, halitakuwa ajabu kuona kuwa China imejenga uwanja wa kisasa wa soka karibu katika kila mji mkuu wa nchi ya Afrika. Viwanja hivyo sio kama tu vimependezesha miji, lakini pia vimekuwa ni alama ya ufahari na chanzo cha mapato kwa nchi hizo.

Kuna kipindi nchi za magharibi zilikuja na maneno “diplomasia ya viwanja vya soka”. Vilitunga maneno haya kwa lengo la kuikatisha tamaa China kujenga viwanja vya soka barani Afrika, kwa madai kuwa nchi za Afrika zina mahitaji muhimu zaidi ya viwanja hivyo.

Pamoja na ukweli kwamba ni kweli nchi za Afrika zinahitaji shule, hospitali, barabara nk, ukweli unabaki palepale kuwa soka ni sehemu muhimu sana ya maisha ya watu wa Afrika, makampuni ya China kujenga viwanja vya soka kwa gharama nafuu ni jambo ambalo kila nchi ya Afrika inapenda na kufurahia.
 
Back
Top Bottom