Kampuni ya China JinkoSolar jana Jumatano ilizindua paneli zake mpya za jua aina ya photovoltaic “Tiger Neo” zenye uwezo wa kuzalisha megawati 410 hadi 620 za umeme kwenye soko la Kenya ili kuhimiza upatikanaji wa umeme nchini humo.
Meneja wa maendeleo ya biashara wa kampuni hiyo kanda ya Kusini mwa Sahara Bw. Sammy Borothi, amesema mjini Nairobi kuwa paneli hizo zinafaa kwa matumizi ya nyumbani na viwandani.
Amesema paneli hizo zimetumia teknolojia za kisasa ili kuhakikisha Kenya inaweza kutumia raslimali zake nyingi za nishati ya juu kwenye usambazaji wa umeme nchini kote.