Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Sweden,
Kampuni ya DSurptive Subdemals nchini Sweden imetengeneza chip itakayoingizwa mwilini mwa binadamu ili kuweza kuhifadhi na kuhakiki taarifa za muhusika kuhusu kupokea chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19. Teknolojia hiyo inatumia NFC, ambayo pia hutumika kwenye mifumo mbali mbali ya malipo bila ya kugusa (contactless payments).
Kampuni hiyo imewatoa watu hofu, kuwa technolojia hiyo haihatarishi usalama wao na wa taarifa zao, kwani hufanyaba kazi pale tu mtu anapotumia kifaa maalumu kusoma kilichomo kwenye chip hiyo.
Aidha kampuni hiyo imesema chip hiyo itakuwa na uwezo wa kusoma joto la mwili wa binadamu ili kuweza kuzungua mabadiliko ya mwili wa binadamu, hali inayoweza kuzuia mlipuko wa magonjwa mengine hapo baadaye.