Kampuni ya Elsewedy ipo katika mazungumzo kuwekeza katika reli na kiwanda cha mbolea

Kampuni ya Elsewedy ipo katika mazungumzo kuwekeza katika reli na kiwanda cha mbolea

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Wanaposema kuwekeza katika reli wanamaanisha sekta gani haswa yaani wanajenga Nini au kutoa huduma gani kuhusiana na reli

..Na reli ya sgr kwa mikoa ya kusini.

..reli hiyo itafika mpaka ulipo mradi wa chuma na makaa.

..Elsewedy ndio watakaojenga na kuendesha reli hiyo, kama nimemuelewa vizuri waziri wa uwekezaji.

..kiwanda cha mbolea kitakuwa ni sehemu ya mradi wa gesi asilia.
 
ingekuwa bwana yule saa hizi mnasifia tu, lakini kwakuwa ni huyu mama hamuishi kutoa maneno yenye kulenga kuwatia watu wasiwasi
Mimi naona Mama ana PR nzuri kwa wapinzani kuliko bwana yule! Angekuwa bwana yule hapa watu wangeshaanza kuporomosheana matusi, wengine wangeitana wachaga, wengine wasukuma! Mama kawatibua wapinzani kidogo kwenye suala la ustaadhi abubakar, ila litakaa sawa soon
 
ingekuwa bwana yule saa hizi mnasifia tu, lakini kwakuwa ni huyu mama hamuishi kutoa maneno yenye kulenga kuwatia watu wasiwasi
Mkuu 'NIMEONA', naomba unioneshe katika maandiko yangu mengi humu JF ulipoona nikimsifia unayemwita 'bwana yule'. Siyo vizuri kuandika juu ya jambo usilokuwa na ushahidi nalo..

Hata hivyo, ni kipi katika niliyoyaandika hapo yanayoonyesha kwamba ninamhusisha mama? Naomba unionyeshe hilo, kwa sababu ni rahisi kufanya hivyo kama umeona ndivyo nilivyofanya.
 
Mimi naona Mama ana PR nzuri kwa wapinzani kuliko bwana yule! Angekuwa bwana yule hapa watu wangeshaanza kuporomosheana matusi, wengine wangeitana wachaga, wengine wasukuma! Mama kawatibua wapinzani kidogo kwenye suala la ustaadhi abubakar, ila litakaa sawa soon

..Rais hataki kukutana na wapinzani.

..Raisi pia hataki wapinzani wakutane ktk vikao na makongamano yao.
 
..Na reli ya sgr kwa mikoa ya kusini.

..reli hiyo itafika mpaka ulipo mradi wa chuma na makaa.

..Elsewedy ndio watakaojenga na kuendesha reli hiyo, kama nimemuelewa vizuri waziri wa uwekezaji.

..kiwanda cha mbolea kitakuwa ni sehemu ya mradi wa gesi asilia.
Ukitaka kuona ubabaishaji ulivyo, anza funzo la kwanza hapo kwa huyo waziri.

Hiyo zungumza yake tu anakuonyesha wazi kwamba hakuna kitu anachokiamini wala kukielewa. Anajivimbisha tu na kukaza sauti, lakini hajui na wala jali lolote kuhusu matokeo ya hayo anayoyasimulia hapo kwa taifa analolitumikia.

Hawa ndani ya serikali hii wamekwishaamua kuiuza nchi hii kwa vipande vya shaba, bila kujali watakacho kiambulia wananchi.
 
..Rais hataki kukutana na wapinzani.

..Raisi pia hataki wapinzani wakutane ktk vikao na makongamano yao.
Rais hajakataa kukutana na wapinzani, tatizo ni pale CDM wanapotaka kuhodhi upinzani TZ. Rais anataka akutane na vyama vyote vya upinzani vikiwemo hivyo mnavyovidharau, ila ninyi ndugu mnasema hatuwezi kukaa na CCM B pamoja na kila aina ya kejeli. Hilo suala la pili naamini kama mkikutana na Mama mtaliweka sawa.
 
..kama chadema ni tatizo, raisi angeweza kukutana na vyama vingine, badala yake anadai anataka kurekebisha uchumi kwanza.

..sio lazima raisi mwenyewe akutane na vyama vya siasa ktk hatua ya awali.

..Mkutano na raisi ungeweza kutanguliwa na vikao kati ya waziri asiyekuwa na wizara maalum na vyama vya upinzani.

..muhimu kuliko yote ni kuweka mazingira yanayotoa haki sawa kwa vyama vyote vya siasa hapa nchini.
 
Kama hatuwezi kuikamilisha hiyo miradi wenyewe kwa wakati bora tuwape wawekezaji, muhimu tuangalie maslahi yetu kama taifa baada ya miradi kukamilika.

Kama patakuwepo na exemption kwa kusafirisha bidhaa zetu (makaa ya mawe) na serikali ipate kodi kiasi kwa miaka kadhaa but isifike ile 100 ya bandari ya Bagamoyo.

Hao jamaa wapewe huo mradi kuliko kuendelea kusubiri mpaka tukiwa tayari kwa pesa zetu wenyewe wakati kila siku tunazidi kuwa masikini kwa kuendelea kukopa.
 
..kama chadema ni tatizo, raisi angeweza kukutana na vyama vingine, badala yake anadai anataka kurekebisha uchumi kwanza.

..sio lazima raisi mwenyewe akutane na vyama vya siasa ktk hatua ya awali.

..Mkutano na raisi ungeweza kutanguliwa na vikao kati ya waziri asiyekuwa na wizara maalum na vyama vya upinzani.

..muhimu kuliko yote ni kuweka mazingira yanayotoa haki sawa kwa vyama vyote vya siasa hapa nchini.
Kwenye mahojiano na Kikeke alisema alikuwa anasubiri vyama vya siasa vijipange, na sasa kataarifiwa vimejipanga hivyo atakutana nao soon! Nafikiri kikao hicho ndicho kinapaswa kutumiwa na wapinzani kutoa nyongo zao. CDM nao waache arrogance, waende wakaudhurie kikao na wenzao, hii mambo ya kusema hawawezi kukaa na TLP meza moja inabomoa na si kujenga
 
Back
Top Bottom