Kampuni ya FIC imenitapeli. Naombeni Ushauri

Kampuni ya FIC imenitapeli. Naombeni Ushauri

Kuna jamaa aliweka 7.5M yaani ile kidogokidogo halafu huko ndio wanamsaka kiongozi wa FIC
 
Kuna moja imeanzishwa inaitwa Brain Master Investment iko na ofisi Masaki. Unaweka kianzio 25000/= unavuna 5% kila siku.Masharti usitoe mpaka muda wa mwezi mmoja.Wanawekeza kwenye bonds za serikali.Unarhusiwa kuwekeza zaidi ya 25000/=
 
Sasa si angekula. 😁
Mkuu umewahi kupata hasara kubwa ya biashara ya mazao au wanyama? Kila ukiwaona unasikia hasira Kali. Kuna jamaa yangu alipata hasara kubwa ya vitunguu, alimpiga marufuku mke wake kuunga vitunguu kwenye mboga, hataki kusikia hata harufu ya kitunguu illkuwa tafrani!
 
😥😥😥
 
IMG-20250310-WA0000.jpg
 
Tuache utani hawa jamaa wamesepa na hela za watu wengi sana
 
Kampuni ya FIC Imenitapeli – Naombeni Ushauri

Ndugu wanajamii,

Nimejikuta katika hali ngumu baada ya kuwekeza zaidi ya shilingi milioni 1 katika kampuni ya FIC, lakini sasa fedha hizo hazipatikani. Nimejaribu kutoa bila mafanikio, na sijapata majibu ya kuridhisha kutoka kwa kampuni husika.

Naomba ushauri wenu:
  1. Je, kuna mwanajamii mwingine aliyekutana na tatizo kama hili na FIC? Kama ndiyo, ulitatua vipi?
  2. Nini hatua sahihi za kuchukua katika hali kama hii? Je, ni vyema kuripoti kwa vyombo vya sheria au kuna njia nyingine za kutatua suala hili?
  3. Kuna taarifa zozote kuhusu uhalali wa kampuni ya FIC nchini Tanzania? Je, imesajiliwa rasmi na mamlaka husika?
Ningependa kusikia mawazo na ushauri wenu ili kujua hatua gani zichukuliwe katika hali hii.

Asanteni.
Kama uliwatumia hyo pesa kwa njia ya tigo pesa, wapigie tigo wareverse muamala
 
Back
Top Bottom