Kampuni ya GSM imepanga kuiendesha Klabu ya Yanga kisasa kwa kuleta Mtendaji Mkuu (C.E.O)

Kampuni ya GSM imepanga kuiendesha Klabu ya Yanga kisasa kwa kuleta Mtendaji Mkuu (C.E.O)

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
Kampuni ya GSM imepanga kuiendesha Klabu ya Yanga kisasa kwa kuleta Mtendaji Mkuu (C.E.O), mpya wa timu hiyo atakayeifanya kuwa ya kisasa ili kufikia mafanikio yao.

GSM ni kati ya wadhamini wa Yanga ambao hivi karibuni ilishinda zabuni ya kuuza jezi za timu hiyo kwenye msimu huu wakitumia kitita cha Sh Bil. 1 huku ikizishinda baadhi ya kampuni.

Kampuni hiyo, pia ilichangia kitita cha Sh Mil. 300, kufanikisha usajili wa wachezaji katika dirisha kubwa kabla ya dirisha dogo linalotarajiwa kufungwa leo saa sita usiku.

Yanga wamefanikiwa kuwasajili nyota watano ambao ni Haruna Niyonzima, Yikpe Gnamien, Ditram Nchimbi, Tariq Seif na Adeyum Saleh.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, kutoka ndani ya Yanga, matajiri hao wapo kwenye mchakato wa mwisho wa kumpata C.E.O huyo.

Mtoa taarifa huyo, alisema upo uwezekano mkubwa wa C.E.O mpya akatokea nchini Ghana huku jina lake likifichwa ambaye atajulikana baada ya kufikia makubaliano mazuri ya kujiunga na klabu hiyo.

Aliongeza kuwa C.E.O huyo atakayekuja atapewa mipango mikakati ya kuhakikisha anaitengeneza Yanga ya kimataifa ili kufikia malengo yao na kikubwa ni kufikia malengo waliyojiwekea ya kuifanya klabu hiyo ipige hatua kama Zamalek, Al Ahly, TP Mazembe na Kaizer Chiefs zote za Afrika.

“Wanachokifanya GSM ni kutaka kuisuka Yanga ili iwe ya kimataifa na ndiyo maana kwa kuanza walianza katika kusajili wachezaji wenye uwezo na hadhi ya kufikia malengo makubwa Afrika, hasa katika michuano ya kimataifa.

“Baada ya kufanya usajili huo, GSM wakamleta kocha mpya raia wa Ubelgiji ambaye ni Luc Aymael kabla ya kuleta kocha msaidizi na wa viungo kutoka Afrika Kusini, Riedoh Berdien ambao wote wamesaini mikataba ya mwaka mmoja na miezi sita pekee.

“Hivyo, baada ya kukamilisha hilo la usajili na kulisuka benchi la ufundi kwa kuleta makocha hao, hivi sasa wapo kwenye mipango ya kumleta C.E.O atakayefanya kazi pamoja na benchi hilo kuna baadhi ya watu wanafuatilia hilo na wengine tayari wapo nje ya nchi,” alisema mtoa taarifa huyo.

Kupitia kwa Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, injinia Hersi Said hivi karibuni alizungumza na Championi Jumatano na kusema kuwa: “Tupo kwenye mipango mikubwa na mizuri ya kuifanya Yanga iwe ya kimataifa na hayo ndiyo malengo yetu GSM kama wadhamini wa timu.

“Ninaamini tutafanikiwa katika hilo na uzuri, mashabiki wenyewe wanaona kila kitu kinachofanyika kwa uwazi katika timu, hivyo kuna mambo mengi tuliyopanga kuyafanya Yanga kwa kipindi chote tutakachokuwa nacho,” alisema Hersi.

Source: Bin RUWEHY

_______________________________________________________________________________

Je, wana JF kinachofanywa na hawa GSM ni sahihi kama wadhamini wa Yanga SC? Je, wanachokifanya GSM hakiwezi kuingilia au kuathiri mchakato wa yanga SC kubadili mfumo wake wa uendeshaji wa timu toka wa sasa na kuwa wa wawekezaji watakaopewa hisa kadhaa?

Nini maoni? Je nini kifanyike kwa sasa?

Ahsante
 
Wananchi chaliiiiii!!!! hata ukiwambia wachangie timu ssahivi hawawezi tena. walisema MO ni bwana wetu (wanamsimbazi) eti kwa sabbu anaigharamia simba sasahivi na wao wanafuata njia hiyohiyo. kweli hawa jamaa zetu huchukua muda mrefu sana kuelewa jambo....
 
Kwa hiyo mlitaka tuendelee kupitisha bakuli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Kawa kawaida, Manara katudhalilisha Yanga.
Anadai Yanga imemleta mzee toka majumba ya kutunzia wazee kuja kuishauri kuhusu mfumo mpya wa uwekezaji.
Mshauri mwenyewe ana CV ya kutukuka sio na alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi timu ya Benfica, Ureno. Ni mtu asiye na dhiki na kaja muda mfupi kutoa ushauri wake.

Kusahau Simba iliwahi kuwa na kocha mmoja mzee amekongoroka hasa. Sijui walimtoa jumba lipi la kutunzia wazee huko Ulaya

Au Crystal Palace wamemtoa jumba lipi kocha wao Roy Hodgson mwenye miaka 72? Mzee kuliko mshauri wa Yanga.
 
Mbona amesifia mlichokifanya na amewapongeza, na pia amemsifia huyoo mzee, hiyo alichomekea kama utani tu,nyie Yanga mnapenda kulalamika sana.
 
Mbona amesifia mlichokifanya na amewapongeza, na pia amemsifia huyoo mzee, hiyo alichomekea kama utani tu,nyie Yanga mnapenda kulalamika sana.
Unaona sawa adhalilishe eti ni utani?
Nani analalamika zaidi ya kuweka facts mezani.
 
Wananchi chaliiiiii!!!! hata ukiwambia wachangie timu ssahivi hawawezi tena. walisema MO ni bwana wetu (wanamsimbazi) eti kwa sabbu anaigharamia simba sasahivi na wao wanafuata njia hiyohiyo. kweli hawa jamaa zetu huchukua muda mrefu sana kuelewa jambo....
Swadakta...Taratibu wanaanza kufuata njia ya Simba SC
 
Kwaiyo na nyie mmekubali kuolewa na Gsm angalau sisi tumeolewa na mtu mmoja nyie mmekubali campuni nzima ya Gsm semeni tu mlimkosa wa kuwaoa siku nyingi ndio maana mlitutupia vijembe kumbe hamna lolote
Sio company tu, wameolewa na group of companies.
Yaani wanachezea gangbang
 
Mkuu Mr Misifa na Mkuu kenge 10 nadhani mungaliweza kutumia Lugha ya staha zaidi.

Ahsante
 
Wananchi chaliiiiii!!!! hata ukiwambia wachangie timu ssahivi hawawezi tena. walisema MO ni bwana wetu (wanamsimbazi) eti kwa sabbu anaigharamia simba sasahivi na wao wanafuata njia hiyohiyo. kweli hawa jamaa zetu huchukua muda mrefu sana kuelewa jambo....
MO alianza hivihivi mwisho wa siku akaichukua Simba, inaelekea na GSM nao wanafuata nyayo.

Haya ndio maendeleo tunayoyataka katika kuliendeleza soka letu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio njia sahii kuzibadilisha hizi timu ,naona GSM watafanikiwa na ukidhingatia jamaa wako karibu na Mzee Wa msoga
 
Mkuu Yanga itakapoingia kwenye uwekezaji itakua aibu kwa manara na genge lake,sasa wewe unategemea ataliongelea vizuri jambo litakalokwenda kuwaacha uchi
Kawa kawaida, Manara katudhalilisha Yanga.
Anadai Yanga imemleta mzee toka majumba ya kutunzia wazee kuja kuishauri kuhusu mfumo mpya wa uwekezaji.
Mshauri mwenyewe ana CV ya kutukuka sio na alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi timu ya Benfica, Ureno. Ni mtu asiye na dhiki na kaja muda mfupi kutoa ushauri wake.

Kusahau Simba iliwahi kuwa na kocha mmoja mzee amekongoroka hasa. Sijui walimtoa jumba lipi la kutunzia wazee huko Ulaya

Au Crystal Palace wamemtoa jumba lipi kocha wao Roy Hodgson mwenye miaka 72? Mzee kuliko mshauri wa Yanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaona sawa adhalilishe eti ni utani?
Nani analalamika zaidi ya kuweka facts mezani.
Mkuu ungeweka facts zote mezani nafikiri Ingekua bora zaidi kuliko kuchukua kakipande kadogo tu ambacho alikua anafanya utani!

Manara amezungumzia Yanga vizuri kwamba ni hatua nzuri na akasema bila kuwa na Yanga imara hakuna Smba imara,,na huyo mzee amemsifia
 
Back
Top Bottom