Na Gianna Amani
Pengine wengi wanaijua Huawei kama kampuni ya kutengeneza simu kutokana na chapa yake kuwepo katika soko kwa miongo kadhaa, lakini Huawei ni zaidi ya kampuni ya kutengeneza simu.
Huawei ni kampuni kubwa ya teknolojia na mawasiliano nchini China na inazidi kuota mizizi katika maeneo tofauti ya dunia kupitia huduma na bidhaa zake ambazo ni muhimu katika ulimwengu wa teknolojia ya dijitali.
Kampuni hiyo hiyo ina lengo la kuleta na kuunganisha kila mtu katika ulimwengu wa kidijitali na kutoa suluhisho la changamoto mbalimbali na hapa wanakumbatia mtandao wa 5G wakisema ni nyenzo muhimu katika hilo.
Wakati wa matembezi ya waandishi wa habari kutoka maeneo tofauti duniani, uongozi wa Huawei ulieleza namna kampuni hiyo inavyotoa suluhisho la kiusalama kwa umma na kurahisha shughuli za usafirishaji na zile za viwandani.
"Kampuni ya Huawei inatoa huduma ya video za moja kw amoja kwa mamlaka za Serikali za mitaa ambayo husaidia endapo yatatokea majanga ya asili au ajali zikiwa na taarifa mbalimbali ikwemo eneo husika lina askari wangapi waliowasili, magari ya uokoaji na magari ya wagongwa,".
Vilevile kupitia taarifa za kimfumo huduma hiyo inaweza kueleza wakati tukio linatokea kulikuwa na watu wangapi katika eneo hilo, taarifa hizo zinawasaidia viongozi wa eneo husika kupanga watu kulingana na uhitaji ili kurahisisha uokoaji wa maisha ya watu sanjari na kujua chanzo.