Kampuni ya IPTL haijawatambua SCBHK kama wadai wake na inahoji mahakamani uhalali wa madai yao

Kampuni ya IPTL haijawatambua SCBHK kama wadai wake na inahoji mahakamani uhalali wa madai yao

KAMPUNI ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), imeiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam itamke rasmi kwamba Standard Chartered Bank (Hong Kong) Limited (SCBHK), si wadai wake na ibatilishe tuzo mbalimbali, ambazo ilipewa huko Ulaya bila kuwepo mhusika mkuu katika migogoro hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa IPTL, Joseph Makandege, kampuni yake inaidai SCBHK fidia ya Dola za Marekani billioni 3.240 (Sh.trilioni 6.5).

Kampuni ya IPTL haijawatambua SCBHK kama wadai wake na inahoji mahakamani uhalali wa madai yao hayo.

Kampuni ya IPTL imeifungulia SCBHK kesi mbalimbali za madai ikiwamo namba 60/2014, namba 801 na 802/ 2016, na kesi za biashara namba 67 na 75/2017 zinazoendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

Imeeleza kustaajabishwa na taarifa zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari nchini, kwamba SCBHK imepata tuzo ya Dola za Marekani 185,449,440 (Sh. 426,533,712,000) dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kesi ya usuluhishi namba ARB/05/04 / 2015 katika Baraza la Kimataifa la Utatuzi wa Migogoro ya Uwekezaji London, Uingereza (ICSID).

Makandege aanasema IPTL pia imepokea tamko la serikali kupitia vyombo vya habari, lililotoa msimamo kwamba Serikali na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) haziwajibiki kuilipa SCBHK fedha hizo; kwamba serikali si mdaiwa bali ni mdhamini tu katika masuala ya IPTL; kwamba mdaiwa anayewajibika kulipa fedha hizo ni IPTL; na kwamba IPTL ilitoa kinga inayoikinga serikali na taasisi zake dhidi ya madai yoyote yatokanayo na IPTL kupewa fedha zilizokuwa katika iliyokuwa “Tegeta Escrow Account” katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kimsingi, IPTL tunakubaliana na msimamo huo wa serikali. Tunatambua kwamba, kama mdhamini wake, serikali haiwajibiki kuilipia madeni yake, jukumu hilo ni lake. Serikali inawajibika tu kusimamia na kuhakikisha kwamba IPTL inalipa madeni yake yote halali inayodaiwa na wadai wake, deni hilo la SCBHK likiwamo, kama kweli ni deni halali la IPTL.

Hata hivyo, madai na tuz0 hiyo ya SCBHK ni miongoni mwa masuala ambayo bado yanabishaniwa na ambayo IPTL bado ina haki ya kuyahoji na fursa ya kuyabatilisha mahakamani. SCBHK pia bado inapaswa kuthibitisha uhalali wa tuzo hiyo katika mahakama za Tanzania. Maamuzi ya Mahakama za Tanzania (Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, kama yeyote atakayekata rufani) ndiyo yatahitimisha mzozo kama kweli SCBHK ni mdai halali wa IPTL au vinginevyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, IPTL hatimaye itashinda katika mashauri yake hayo, SCBHK yaweza kupoteza kabisa uhalali wa kuendelea kuibughudhi IPTL na serikali kwa madai yake au yaweza kukata deni lake hilo Sh. bilioni 426.53 katika Sh. trilioni 6.5 inazodaiwa na IPTL na kuilipa IPTL kiasi kitakachobakia.

Na hatakama hatimaye itashindwa katika mashauri yake hayo, IPTL haitashindwa kulipa deni hilo la SCBHK; kwani kiwanda na rasilimali zake zingine zinatosha kuuzwa na kulipia madeni yake sambamba na hilo la SCBHK. Na hata kama hatimaye, mazungumzo yatahitajika, IPTL (siyo Serikali) ndiyo itazungumza na kukubaliana na SCBHK, kwani IPTL na SCBHK ndiyo wadau katika mashauri husika, wenye haki na wajibu huo.

“Katika muktadha huo, IPTL inakubaliana na inaunga mkono kwa dhati msimamo wa serikali na inaahidi kufanya kila liwezalo kulipa madeni yake, lakini inaomba iwezeshwe kufanya hivyo kwa kulipwa madeni yake na kurudishiwa leseni yake ya kufua na kusambaza umeme wa bei nafuu na wa uhakika kwa maendeleo ya Watanzania na Taifa zima katika uchumi wa viwanda,” ulisema.
Hawa IPTL wanajichanganya bila udhamini wa serikali IPTL isingepata mkopo wa kujunua mitambo ya kuzalisha umeme.Serikali iliahidi kununua umeme toka IPTLndiyo bank ikaona uhakika wa biashara upo
 
Umeelewa kweli?! IPTL wanasema ni wao na hao Hong Kong SB wanawajibika, serikali haihusiki.
Isipkuwa unaotaka serikali iirejeshee leseni yake ya kuendeea kufua umeme.
Umesoma Hukumu na Kuelewa ?
 
Kama IPTL wanaweza kufua na kusambaza umeme wa bei na fuu wapewe tenda hiyo.
Hapo serikali itakuwa imeiachia mzigo wake wa kulipa hilo deni.
Sasa kama sasa hivi wanaweza kuzalisha Umeme na kusambaza kwa bei nafuu,mwanzo walishindwa nini kuuza kwa bei nafuu!!? Bei nafuu ni IPI hasa.
 
PESA YA ESCROW SIYO YA UMMA.

KWA NINI WALIKAMATWA NA KUWEKWA NDANI?


Kwenye ile hela ya escrow kuna hela nyingi ya serikali

1: Kodi

2: Sbb kulikuwa na disputes juu ya bei halisi ya umeme wa IPTL na Tanesco, kuwa IPTL iliuzia umeme tanesco bei ghali kwa unit 1, hivyo sbb mahesabu rasmi yalikuwa yanaendelea kujua gharama sahihi kwa unit 1 ni kiasi gani ilipaswa Tanesco inunue umeme IPTL, hivyo ingethibitika kuwa tanesco waliuziwa umeme kwa bei ya juu, zile hela za escrow zingelipa kile kiwango ambacho kilizidi na kurudishwa tanesco.. Hivyo hela ya escrow kuna hela nyingi tu za serikali..

3: Money laundering, yaani hela za escrow ilifanyika kwa money laundering ambayo ni hela haramu, kwani huwezi ku track hela hizo ili usijue nani kapokea au zilienda account ipi, nchi gani, banks zipi, kwani zilibebwa kwa sandarusi na malori, hivyo hilo ni kosa kubwa sana kwa mambo ya fedha, money laundering..

Kwa hayo matatu, serikali ina wajibu wa kuwakamata haraka Ruge na Sethi..

Nadhani umepata insights kidogo kwnn serikali inahusika na ina hela yake na makosa ya money laundering waliofanya wahusika

Likewise, serikali haidaiwi na bank ya Hong Kong, serikali ni kama mdhamini tu haijaenda kukopa Standard Chartered ya Hong Kong, so serikali haidaiwi kitu chochote, IPTL wamalizane na SCBHK
 
kama serikali waliidhamini IPTL wapewe mkopo kwa nini serikali wenyewe wasifanye hivyo kwa TANESCO hili wanunue mitambo yao wenyewe
 
kama serikali waliidhamini IPTL wapewe mkopo kwa nini serikali wenyewe wasifanye hivyo kwa TANESCO hili wanunue mitambo yao wenyewe
Serikari aijawahi idhamini IPTL kupewa mkopo iliahidi watanunua umeme tu wakiweza zalisha. Na walifanya ivyo that is enough of an exclusion clause iwapo IPTL walikuwa hawalipi madeni yao wakipata hela it has nothing to do with the government.
 
Umesoma Hukumu na Kuelewa ?
Nimesoma hayo maelezo ya hapo juu nikaelewa, hukumu sijaisoma.
Kama IPTL wanasema deni ni la kwao na wanawajibika kulilipa, ila hawamtambui SCHK, sasa sijui nani anawadai. Mimi nilivyoelewa hawa SCHK wao walinunua madeni kutoka Malaysia huko, sasa hawa IPTL wanakili nani anawadai?!
 
1571759226631.png

(sawa na Sh 426,533,712,000) kwa Benki ya Standard Chartered (Hong Kong) Limited (SCBH) na sio serikali. Imesema inakubaliana na msimamo wa serikali kuwa wao ni wadhamini wa IPTL, na jukumu lao ni kusimamia na kuhakikisha IPTL inalipa madeni yake yote halali inayodaiwa na wadai wake ikiwemo la benki hiyo.

Benki hiyo imeshinda tuzo hiyo katika kesi Usuluhishi namba ARB/05/04 ya mwaka 2015 katika Baraza la Kimataifa ya Utatuzi wa Migogoro ya Uwekezaji huko London, Uingereza (ICSID). Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa IPTL, Wakili Joseph Makandege alisema kampuni hiyo haijashindwa kulipa deni hilo, bali bado inatumia haki yake ya msingi na ya kikatiba kuhoji madai ya SCBHK mahakamani.

Makandege alisema kampuni hiyo itawajibika kulipa deni hilo na serikali italazimika kuiwajibisha kufanya hivyo endapo IPTL itashindwa katika mashauri yake yanayoendelea mahakamani nchini. “Hakuna haja ya Watanzania na wadau wote wa IPTL kutaharuki.

Ingawa hadi sasa hatujarudishiwa leseni ya kufua na kusambaza umeme, bado ni kampuni binafsi iliyo hai na yenye rasilimali lukuki, miundombinu iliyokamilika na uongozi thabiti unaotosha kusimamia haki na maslahi ya kila mdau wa IPTL,” alisema Makandege.

Alieleza kuwa kampuni hiyo ilitoa kinga inayoikinga serikali na taasisi yoyote yatokanayo na kupewa fedha zilizokuwa katika Akaunti ya zake ikiwamo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) dhidi ya madai Tegeta Escrow iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Alisema kwa sasa, IPTL haitambui benki hiyo kama wadai wake na inahoji mahakamani uhalali wa madai yao hayo. “IPTL imewafungulia SCBHK mashauri mbalimbali ikiwemo shauri la madai namba 60 ya mwaka 2014, shauri la maombi namba 801 na 802 ya mwaka 2016 na mashauri ya biashara namba 67 na 75 ya mwaka 2017 yanayoendelea katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,” alifafanua.

Alisisitiza kuwa katika mashauri hayo, pamoja na nafuu nyingine, IPTL inaiomba Mahakama Kuu itamke rasmi kwamba benki hiyo siyo wadai wao na ibatilishe tuzo mbalimbali ambazo ilipewa huko Ulaya bila kuwapo IPTL ambayo ndiyo mhusika mkuu katika migogoro husika. Kwa mujibu wa Makandege, IPTL inaidai SCBHK fidia ya jumla ya Dola za Marekani bilioni 3.240 (sawa na Sh trilioni 6.5).

Alisema madai na tuzo hiyo ni miongoni mwa masuala ambayo bado yanabishaniwa na ambayo IPTL bado ina haki ya kuyahoji na fursa ya kuyabatilisha mahakamani. Alisema benki hiyo bado inapaswa kuthibitisha uhalali wa tuzo hiyo katika mahakama za Tanzania ambako uamuzi ndiyo utahitimisha mzozo kama kweli benki hiyo ni mdai halali wa IPTL au vinginevyo.

“Endapo IPTL itashinda katika mashauri yake hayo, benki hiyo inaweza kupoteza uhalali wa kuendelea kuwabughudhi kwa madai yake au inaweza kukata deni lake hilo la shilingi bilioni 426.5 katika shilingi trilioni 6.5 inazodaiwa na IPTL na kuilipa IPTL kiasi kitakachobakia,” alieleza Makandege.

Alisema kama IPTL itashindwa katika mashauri yake hayo, haitashindwa kulipa deni hilo kwani kiwanda na rasilimali zake nyingine zinatosha kuuzwa na kulipia madeni yake.

Makandege aliwaomba wadau wa kampuni hiyo kushirikiana ili kupata suluhisho la kudumu la migogoro hiyo ili kuipa IPTL fursa ya kuendesha masuala yake yenyewe na kulipa madeni yake yote na kuiondolea serikali adha na usumbufu wa kudaiwa na wadai wa IPTL kila mara.

Hata hivyo, ameomba Tanesco kulipa malimbikizo ya fedha inazoidai kwani kwa kutofanya hivyo, ni kuidhoofisha na kuinyima uwezo na weledi wa kukabiliana na changamoto zake yenyewe. “IPTL inakubaliana na inaunga mkono kwa dhati msimamo wa serikali na inaahidi kufanya kila liwezalo kulipa madeni yake lakini inaomba iwezeshwe kufanya hivyo kwa kulipwa madeni yake na kurudishiwa leseni yake ya kufua na kusambaza umeme wa bei nafuu na wa uhakika kwa maendeleo ya Watanzania na Taifa zima katika kukuza uchumi wa viwanda,” alisisitiza Makandege.
 
Ivi ukiweka nyumba kama dhamana benki ukishindwa kulipa nini kinafuata?

Kwanini hawajalipa deni muda wote mpaka leo?

Kwanini Serikali ilituma wawakilishi kwenye kesi ya msingi?

Kwanini Tanesco imelipa pesa za garama za kesi?
 
Nimesoma hayo maelezo ya hapo juu nikaelewa, hukumu sijaisoma.
Kama IPTL wanasema deni ni la kwao na wanawajibika kulilipa, ila hawamtambui SCHK, sasa sijui nani anawadai. Mimi nilivyoelewa hawa SCHK wao walinunua madeni kutoka Malaysia huko, sasa hawa IPTL wanakili nani anawadai?!
Kasome hukumu
 
sie wanachama wenzio wa JF hatujui nani msema kweli....taarifa ya CAG kwa mwaka 2019/2020 hili likiwepo ndo twaweza jitambua twasimama wapiiii
 
Serikali inabidi wawe waangalifu na IPTL. Inaoneka hawana nia ya kulipa. Watawaangasha mahakamani hiyo benki mpaka ukija uongozi mbovu serikali ilipe. Watadai hawana uwezo wa kulipa kwa sababu serikali ilivunja mkataba!!
 
Kila siku ukisoma au kusikia habari za IPTL unapata ni mpya
 
Hivi mtu akishindwa kulipa anadaiwa mdhamini aliyedhamini au mwenye deni?
 
Back
Top Bottom