Kampuni ya IPTL haijawatambua SCBHK kama wadai wake na inahoji mahakamani uhalali wa madai yao

Kampuni ya IPTL haijawatambua SCBHK kama wadai wake na inahoji mahakamani uhalali wa madai yao

Ivi ukiweka nyumba kama dhamana benki ukishindwa kulipa nini kinafuata?

Kwanini hawajalipa deni muda wote mpaka leo?

Kwanini Serikali ilituma wawakilishi kwenye kesi ya msingi?

Kwanini Tanesco imelipa pesa za garama za kesi?
Kuna mambo hujaelewa,.
IPTL wanakubali kua wanadaiwa, lakini mdai wao sio SCHB.

Sasa wewe ukikopa hela Exim Bank ukaeka dhamana nyumba kisha CRDB wakaja wakataka waiuze kufidia hilo Deni ambalo ki msingi hukukopa kwao utakubali?
 
IPTL ina idai serikali kwa mujibu wa kipengele cha mwisho

“Katika muktadha huo, IPTL inakubaliana na inaunga mkono kwa dhati msimamo wa serikali na inaahidi kufanya kila liwezalo kulipa madeni yake, lakini inaomba iwezeshwe kufanya hivyo kwa kulipwa madeni yake na kurudishiwa leseni yake ya kufua na kusambaza umeme wa bei nafuu na wa uhakika kwa maendeleo ya Watanzania na Taifa zima katika uchumi wa viwanda,” ulisema
Hu ndio mnatano haswa
 
Kama ulifuatilia sakata la Escrow na mchakato ulivyofika Rugemalira alilipa kodi zote zilizotakiwa, labda kama kosa lake ni kugawa miamala kwa watu mbalimbali.
Kwenye ile hela ya escrow kuna hela nyingi ya serikali

1: Kodi

2: Sbb kulikuwa na disputes juu ya bei halisi ya umeme wa IPTL na Tanesco, kuwa IPTL iliuzia umeme tanesco bei ghali kwa unit 1, hivyo sbb mahesabu rasmi yalikuwa yanaendelea kujua gharama sahihi kwa unit 1 ni kiasi gani ilipaswa Tanesco inunue umeme IPTL, hivyo ingethibitika kuwa tanesco waliuziwa umeme kwa bei ya juu, zile hela za escrow zingelipa kile kiwango ambacho kilizidi na kurudishwa tanesco.. Hivyo hela ya escrow kuna hela nyingi tu za serikali..

3: Money laundering, yaani hela za escrow ilifanyika kwa money laundering ambayo ni hela haramu, kwani huwezi ku track hela hizo ili usijue nani kapokea au zilienda account ipi, nchi gani, banks zipi, kwani zilibebwa kwa sandarusi na malori, hivyo hilo ni kosa kubwa sana kwa mambo ya fedha, money laundering..

Kwa hayo matatu, serikali ina wajibu wa kuwakamata haraka Ruge na Sethi..

Nadhani umepata insights kidogo kwnn serikali inahusika na ina hela yake na makosa ya money laundering waliofanya wahusika

Likewise, serikali haidaiwi na bank ya Hong Kong, serikali ni kama mdhamini tu haijaenda kukopa Standard Chartered ya Hong Kong, so serikali haidaiwi kitu chochote, IPTL wamalizane na SCBHK
 
Serikali inabidi wawe waangalifu na IPTL. Inaoneka hawana nia ya kulipa. Watawaangasha mahakamani hiyo benki mpaka ukija uongozi mbovu serikali ilipe. Watadai hawana uwezo wa kulipa kwa sababu serikali ilivunja mkataba!!
Hisa za IPTL zilizodaiwa kununuliwa na PAP ya yule singasinga aliuziwa na nani?

Inatakiwa akamatwe tena na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.
 
Back
Top Bottom